Monday, March 18, 2019

ALLAH KATEREMSHA AYA NA KUSEMA WATAKAOINGIA PEPONI NI WATU WENYE CHUKI

Image may contain: 23 people
Sura Al-Nahl 16:28
[Kuhusu wale wanaoingia mbinguni] – Malaika watasema kwa wale ambao watawafanya wafe katika usafi (utakatifu), ‘Amani na iwe juu yenu. Ingieni paradiso kutokana na matendo yenu.’
LAKINI, QURAN HIYO HIYO INASEMA:
Sura Al-Hijr 15:45-47
Wenye haki (watakatifu) watakaa kwenye bustani na chemchemi za maji, kwa amani na usalama wataingia humo. Nasi tutaondoa chuki yote ndani ya mioyo yao.
Maswali:
1. Katika 16:28, inaonekana kwamba watakaiongia peponi ni watu walio safi kwa sababu malaika wamesababisha watu hao wafe wakiwa safi. Lakini 15:45-47 inaonyesha kuwa wataingia peponi wakiwa na chuki mioyoni mwao. Je, chuki ni sehemu ya usafi?
2. Je, aya hizi zimetoka kwa mtoaji yule yule?
3. Kama chuki ni mbaya kiasi cha kuhitajika kuondolewa mioyoni mwa Waislamu wanaoingia peponi, iweje wakiwa duniani wanaagizwa kuwachukia wale wasio Waislamu (kama tulivyoona kwenye 4:101)?
HITIMISHO
Hizi ni baadhi tu ya aya ambazo zinaonyesha kuwa quran au Allah anasema jambo moja hapa, kisha anajipinga mwenyewe katika sehemu nyingine.
Na ukweli huu, ninavyodhani,unamaanisha kuwa, ama:
1. Si kila aya iliyo kwenye quran ni maneno ya Mungu muumba vyote – maana Mungu huyo hawezi kufanya mambo kama hayo; au
2. Quran haitokani na Mungu bali imetokana na chanzo kingine, ndiyo maana inaonyesha tabia za viumbe za kujisahau au kutojua mambo yote, hususan yajayo.
Nadhani siku ya mwisho Muhammad atawakana watu wote wanaomwamini maana atakuja kusema kwamba, “Mimi niliwaambia kuwa wakitaka kujua kama quran inatoka kwa Allah waangalie kama quran inajikanganya. Sasa waliona kuwa inajikanganaya, lakini wao wakendelea tu kuiamini.
Pia Muhammad atawakana wale wote wanaomwamini na kumfuata kwa sababu yeye mwenyewe anasema wazi katika sura Al-Ahqaf 46:9,
... nor do I know what will be done with me or you. I follow only what is revealed to me.
Yaani,
... na wala mimi sifahamu kile nitakachotendewa wala kile ninyi mtakachotendewa. Mimi nafuata tu kile ninachofunuliwa.
Swali ni kwamba, je, kama mtu mwenyewe anakiri kuwa hajui hatima yake wala hatima ya wale wanaomfuata, je, kama ni kweli Mungu wa mbinguni ndiye aliyempatia quran, je, angekaa kimya kweli juu ya suala la HATIMA za wanadamu? Yaani jibu la mtu atakuwa wapi MILELE lingeachwa hewani tu hivihivi? Na kama Muhammad hajui hili na bado anataka watu wamfuate, je, ni hilohilo tu asilolijua au yapo na mengine asiyoyajua? Bila shaka hii inaashiria kuwa yako mengi asiyoyajua.
Sijui kwa kweli! Kama nilivyosema, mimi kwa mambo haya ni maamuma tu. Kwa hiyo, inawezekana niko nje kabisa ya kile kinachomaanishwa. Nitafurahi kama ndugu zangu Waislamu mtanisaidia kujua mambo haya.
Lakini kwa ule upande ambao mimi naufahamu zaidi, yaani Ukristo, Bwana Yesu anasema: Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. (Yohana 14:6). Yaani, hakuna namna ya kwenda mbinguni isipokuwa kwa kumwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi. Hiyo ndiyo namna pekee ya kufika mbinguni. Tafakari!

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW