Thursday, May 18, 2017

PANDA KWA MACHOZI UTAVUNA KWA FURAHA

Image may contain: one or more people, text and outdoor
Zaburi 126:5-6
“Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha. Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.”
Kupanda siku zote ni kazi ngumu. Kwanza ni lazima uamke asubuhi na mapema, ubebe mbegu na jembe, utembee kwenye baridi kuelekea shamba ambalo limejaa matope maana watu hawapandi wakati wa kiangazi, uiname shambani siku nzima au siku kadhaa ukipanda mbegu zako. Sio zoezi la kufurahia au kuchekelea lakini ni la muhimu sana kama unataka kuvuna.
Siku ya kuvuna ni siku ya furaha, siku ya kuhesabu utajiri, siku ya kuhesabu matunda ya jasho, siku ambayo taabu ya kupanda inazaa matunda, pamoja na kwamba utachoka lakini unakuwa umejaa furaha maana sasa mavuno umeyapata. Lakini huwezi kuvuna bila kupanda, lazima upande ili utazamie kuvuna. Usione wengine wanapanda ukavuta shuka halafu ukasubiri nawe ukavune.
Leo nakutia moyo wewe uliye kwenye hatua ya kupanda, Usikate tamaa jua ipo siku utavuna kwa kelele za furaha. Unaweza kuwa unapanda kwenye elimu, biashara, ujasiriamali, ufugaji kazini kwako, uwekezaji, ujenzi, huduma n.k. wewe endelea kupanda kwa bidii, panda mbegu nyingi kadiri uwezavyo wala usiwe mvivu. Mbegu siku zote ni chache na mavuno ni mara 100, hivyo panda, panda, panda. Na wewe unayesubiri kuvuna wakati hutaki kupanda kwa machozi tambua kuwa hakuna kuvuna bila kupanda. Ukitaka siku ya mavuno nawe ushangilie chukua mbegu shika njia nenda shambani ukapande.
Mbarikiwe.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW