Thursday, April 27, 2017

JE, UNAYO HEKIMA KUTOKA KWA MUNGU?




(a) Solomoni alionyeshaje hekima ya pekee katika kuamua ni nani aliyekuwa mama ya mtoto?
(b) Mungu anaahidi kutupatia nini, na ni maswali gani yanayozuka?
Ilikuwa kesi ngumu sana—wanawake wawili walibishania mtoto mmoja mchanga. Wanawake hao waliishi pamoja, na mmoja wao alijifungua mwana siku chache tu baada ya mwingine kujifungua. Mtoto mmoja alikuwa amekufa, na kila mwanamke alidai kwamba mtoto aliyekuwa hai alikuwa wake. * Hapakuwa na watu wengine walioshuhudia lililotukia. Yaelekea kwamba kesi hiyo ilikuwa imesikilizwa katika mahakama ya chini lakini haikusuluhishwa. Mwishowe, kesi hiyo ilipelekwa kwa Solomoni, mfalme wa Israeli. Je, angefunua ukweli wa mambo?
Baada ya kuwasikiliza wanawake hao wakibishana kwa muda, Solomoni aliomba upanga. Kisha, akaamuru mtoto huyo akatwe vipande viwili na kila mwanamke apewe kipande kimoja. Mara moja mama ya mtoto huyo akamsihi mfalme amkabidhi yule mwanamke mwingine mtoto wake mpendwa. Lakini mwanamke yule mwingine aliendelea kusisitiza mtoto huyo akatwe vipande viwili. Sasa Solomoni akajua ukweli wa mambo. Alijua jinsi ambavyo mama humhurumia na kumpenda sana mtoto wake, naye alitumia ujuzi huo kutatua kesi hiyo. Hebu wazia furaha ya mama huyo Solomoni alipompa mtoto wake na kusema: “Yeye ndiye mama yake.”—1 Wafalme 3:16-27.
Solomoni alikuwa na hekima ya pekee, sivyo? Watu walistaajabu sana waliposikia jinsi Solomoni alivyosuluhisha kesi hiyo, “maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake.” Naam, hekima ya Solomoni ilikuwa zawadi kutoka kwa Mungu. Mungu alikuwa amempa “moyo wa hekima na wa akili.” (1 Wafalme 3:12, 28) Lakini vipi sisi? Je, Mungu anaweza pia kutupatia hekima? Ndiyo. Solomoni aliongozwa kuandika hivi: “BWANA huwapa watu hekima.” (Mithali 2:6) Yehova aahidi kuwapa hekima, yaani, uwezo wa kutumia ujuzi, ufahamu, na utambuzi, wale wanaoitafuta kwa unyofu. Tunawezaje kupata hekima inayotoka juu? Na tutaitumiaje maishani mwetu?
Tunahitaji kushika hekima kwa sababu ni zawadi kutoka kwa Mungu. Solomoni alisema: “Mwanangu, . . . shika hekima kamili na busara.” (Mithali 3:21) Kwa kusikitisha, Solomoni mwenyewe alishindwa kufanya hivyo. Alikuwa mwenye hekima maadamu alitii kutoka moyoni. Lakini mwishowe, wake zake wengi wa kigeni waliugeuza moyo wake kutoka kwa ibada safi ya Yehova. (1 Wafalme 11:1-8) Hali iliyompata Solomoni inaonyesha kwamba tusipotumia ifaavyo ujuzi tulio nao hautatufaidi.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW