Friday, March 17, 2017

KWANINI YESU ALIKUFA MSALABANI?

Image may contain: cloud, sky and text
“Basi Mungu wa amani, ambaye kwa damu ya agano la milele alimleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Yesu, yule Mchungaji Mkuu wa kondoo, awafanye ninyi wakamilifu mkiwa
mmekamilishwa katika kila jambo jeama ili mpate kutenda mapenzi Yake, ili atende ndani yetu kile kinachompendeza machoni Pake, kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye utukufu una Yeye milele na milele” (Waebrania 13:20-21).
Mungu Baba alipanga kifo cha Bwana Yesu na pia alipanga kufufuka kwake. Hii ndiyo sababu Biblia inasema kwamba Mungu alimleta tena kutoka kwa wafu “Kwa damu ya Agano la milele” (Waebrania 13:20-21).
“Damu ya Agano la milele” inamaanisha damu ya Yesu Kristo. Yesu alisema, “Hii ndiyo damu yangu ya agano” (Mathayo 26:28). Biblia inatufundisha kwamba ili Yesu atuokoe ilimbidi akufe na afufuke. Yesu hangefufuka, basi hatungeokolewa. Kifo cha Bwana Yesu Kristo kilileta msamaha wa dhambi, kuoshwa kwa dhambi na wokovu kwa watu wa Mungu. Kufufuka kwa Yesu Kristo lilikuwa ni dhihirisho kwamba Mungu Baba amekubali dhabihu yake ya kifo msalabani.
Wakati Yesu alikufa msalabani alijitoa kuwa sadaka kwa watu wake ili awalipie fidia ya dhambi zao. Wakati Mungu Baba alimfufua kutoka kwa wafu lilikuwa dhihirisho kwamba Mungu alifurahishwa na kifo cha Yesu. Mungu Baba alikuwa anasema kwamba kifo cha Yesu kimetosheleza fidia ya dhambi za watu wake.
Biblia inasema, “Kama Kristo hajafufuka, imani yenu ni batili, nanyi bado mko katika dhambi zenu” (1 Wakorintho 15:17). Hii inamaanisha kwamba kufufuka kwa Yesu Kristo lilikuwa hakikisho kwamba Mungu Baba alikubali kifo cha Yesu Kristo kama malipo yanayokubalika kulipia dhambi za watu wake. Yesu hangefufuka kutoka kwa wafu basi kifo chake hakingemfaidi yeyote. Ni baada tu ya kufufuka ndipo angeweza kuwaokoa watu wake kutoka kwa dhambi zao.
Biblia inasema, “Kristo alifufuka kutoka wafu kwa utukufu wa Baba” (Warumi 6:4). Tukija kwa Yesu Kristo kwa imani na kumwamini yeye pekee kwa wokovu, basi dhambi zetu zitaondolewa na tutasamehewa na kupewa wokovu.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW