Monday, October 24, 2016

KUMBE ALLAH ATAWALISHA CHAKULA NA KUWAPA MAJI WAISLAMU WAKIWA JEHANNAM?


CHAKULA CHA WAISLAM WAKIWA MOTONI
Vyakula vyao vimetajwa kua ni:
1-Dhari’i: Hii ni miba ichomayo koo na imetajwa katika Suratul Ghaashiyah aya ya 6.
2-Ghisliin: Amesema Allah kuhusiana na Ghisliin “ Hawatokua na chakula humo ila Usaha”. Suratu Haaqah aya ya 36. Hivyo ghisliin ni usaha ambao utawatoka wenyewe watu wa motoni kutokana na adhabu kali na kisha watakula usaha wao huo.
3-Zaquum: Ni mti mchungu huu ambao unaota katika jahannam, umoto wake umefananishwa na shaba iloyayushwa ambayo itachemkia tumboni. Matunda yake yanatisha kama vichwa vya mashetani. Umetajwa katika Suratu-Dukhaan aya ya 43-45 na Suratu Swaaffaat aya 62-66 na Suratul_Waaqiah 52-53
4-Ghuswah: Ni aina nyengine ya chakula cha watu wa motoni. Allah amekitaja katika suratul-Muzammil “Na chakula kikwamacho na adhabu iumizayo” 13
VINYWAJI VYA WAISLAMU WAKIWA MOTONI
Kabla ya kutaja vinywaji vya watu wa motoni, tukumbuke kua baada ya watu wa motoni kuingizwa Jahannam watashikwa na kiu kali kutokana na joto la Jahannam, hivyo watawapigia kelele watu wa peponi na kuwaambia kama anavyotusimulia Allah “Watu wa motoni watawanadia watu wa peponi: Tumiminieni maji au kile alichokuruzukuni Allah watasema (watu wa peponi kuwajibu): Hakika Allah ameviharamisha kwa kwa makafiri.(50) Ambao waliifanya dini yao kua ni upuuzi na mchezo,na yakawadanganya maisha ya dunia. Basi leo tutawasahau (na kuwaacha humohumo motoni)kama walivyosahau mkutano wa siku hii(51)” (Suratul Aaraf).
Baada ya joto la jahannam kuzidi wataoneshwa maji yachemkayo, kisha watayaendea lakini hawatoweza kunywa kwa umoto wake, watataka kurudi tena mahali walipokua na wakirudi, watazidiwa na kiu watataka kwenda kwenye yale maji na huo ndio utakua mzunguko wao. Amesema Allah katika suratu Rahman aya ya 44 “Watakua wakizunguka baina ya (Jahannam)na baina ya maji ya moto yachemkayo”. Amesema Allah kuhusiana na maji hayo katika Suratu-Muhammad aya ya 15“……na kunyweshwa maji yachemkayo yatakayokata chango zao” na wapo ambao maji hayo yatatoa ngozi zao na yalokuwemo kwenye matumbo yao kama anavyosema Allah katika Suratul-Hajj aya ya 20 “Kwa maji hayo vitayayushwa viliomo matumboni mwao, na ngozi zao pia”.
Ama vinywaji vyengine ni:
1- Maji ya usaha. Amesema Allah katika Suratu –Ibrahiim aya ya 16-17“ Na atanyeshwa humo maji ya usaha. Awe anayagugumiza na asiweze kuyameza. Na mauti yatamjia kutoka kila mahali na hatokufa”. 16-17.
2- Maji ya shaba. Amesema Allah kuhusiana na maji haya katka Suratul-Kahfi “ Na watakapoomba msaada (kutokana na kiu kali)watapewa maji kama ya shaba iliyoyayushwa itakayounguza nyuso zao, kinywaji kibaya kilioje hicho”
Ama kwa upande wa hadithi: Inasimuliwa kua watu wa jahannam wakiyasogelea maji kwa ajili ya kuyanywa basi itatoka ngozi ya uso na kuingia katika chombo chenye maji yale kutokana na shida ya vuke la moto.
SWALI:
Kwanini Allah atawapa watu wa Jehannam chakuna na vinywaji?
Na pia Mtume swalla Allahu alayhi wasalam amesema” Ameoneshwa moto na akawakuta wengi wao walokuwemo humo ni wanawake..”hivyo akawataka wazidishe kutoa sadaka.
Ili mtu aepukane na Jahaanam ni muhimu kuzidisha amali zifuatazo:
Kuzidisha kutoa sadaka kwani amesema Mtume wa Allah “Sadaka huondoa makosa kama moto unavyokula kuni.(Hadith sahih).
Natanguliza pole kwa Wanawake wa Kiislam maana Allah ataijaza Jehannam na wanawake.
Karibuni kwa Yesu ambaye anawapenda na amesha wasamehe dhambi.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW