Wednesday, October 26, 2016

ALLAH ANASEMA KUWA DUNIA NI KAMA ZULIA, KUMBE ALLAH HAKUUMBA DUNIA


Elewa kuwa namba za aya zinatofautiana kwenye matoleo tofauti ya Kurani. Namba hizi za aya zifuatazo zimetolewa kwenye (toleo lililorekebishwa la) Yusuf ‘Ali. Nimesahihisha matumizi ya herufi kubwa.

ETI DUNIA IPO KAMA ZULIA:
Sura 20:53 "Yeye aliyeiumba dunia kwa ajili yako kama zulia ameisambaza"
VIOJA VINAANZA, ALLAH KAUMBA DUNIA KAMA ZULIA 'CARPET'
Sura 50:7 "Na dunia – tumeisambaza 4946, na tumeweka milima juu yake …"
Rejeo la Yusuf ‘Ali la 4946 chini ya ukurasa linasema, "Linganisha xiii. 3; na xv. 19 na rejeo la 1955.

Sura 67:15 "Ni Yeye aliyeifanya dunia iweze kuthibitiwa 5571…" Tafsiri nyingine zinatumia neno "usawa." Rejeo la 5571 la Yusuf Ali chini ya ukurasa linasema, "Zalul inatumiwa kwenye ii.71 kwa mnyama aliyefunzwa na anayeweza kuthibitiwa: hapa linatumika kuielezea dunia, na nimelitafsiri kama ‘inayoweza kuthibitiwa’…."

ETI MWEZI UNATOA MWANGA
Sura 71:15 "‘Je hamuoni jinsi Allah alivyoumba mbingu saba moja juu ya nyingine ‘NA ALIUMBA MWEZI UWE MWANGA KATI YAO, na aliumba jua liwe taa ing’aayo?" Hata kama ikichuliwa kuwa hii ni lugha ya kufananisha, hakuna kitu chochote chenye kuashiria mafundisho ya kisasa ya unajimu.
ETI MWEZI UNATOA MWANGA KWENYE AYA HAPO JUU YA SURA 71 AYA 15. HUU NI MSIBA.
DUNIA NI ZULIA, ASTAGHAFURILLAH.
Sura 71:19 "‘Na Allah aliiumba dunia kwa ajili yako kama zulia (lililosambazwa),5718…" Rejeo la 5718 la Yusuf ‘Ali chini ya ukurasa linasema, "linganisha xx 53.

Sura 78:6-7 "Sisi [Allah] je hatujaumba dunia pana kama eneo kubwa wazi 5890, na milima kama vigingi?" Rejeo la 5890 la Yusuf ‘Ali chini ya ukurasa linasema, Tazama rejeo la 2038 hadi xvi. 15. Linganisha pia xiii. 3 na xv. 19. Eneo kubwa wazi lenye nafasi pana linaweza kulinganishwa na zulia, ambalo milima ni kama vigingi

Zul-Karnain kwenye Sura ya 18 na Sayansi ya Unajimu
Sura 18:85-86 "Njia (mojawapo) ambayo [Zul-qarnain] aliifuata, hadi, wakati alipofika machweo ya jua, alikuta linazama kwenye chemchemi ya maji meusi na machafu: karibu na sehemu hiyo aliwakuta watu: Sisi [Allah] alisema: ‘Oh Zul-qarnain! (Wewe unayo mamlaka) ama kuwaadhibu ama kuwatendea wema." Neno "Murky" limetafsiriwa pia kama chemchemi ya maji "nyeusi" na yenye "udongo." Msemo "chemchemi ya . . . maji" pia imetafsiriwa kama "chemchemi.". M. H. Skahir ameitafsiri kuwa "bahari nyeusi."
Sura 18:89-90 "Kisha [Zul-qarnain] aliifuata njia (nyingine), hadi alipofika kwenye mawio ya jua, alilikuta likichomoza juu ya watu ambao hatukuwapa kitu chochote cha kujikinga dhidi ya jua."
Watoa maelezo wa Kiislam wanatofautiana juu ya Zul-qarnain (mtu wa pembe mbili) kuwa ni nani hasa. Wengine wanafikiri kuwa ni Alexander Mkuu, wengine wanafikiri ni Cyrus wa Uajemi, na wengine wanafikiri kuwa ni mfalme wa Yemeni. Hata hivyo haijalishi. Vyovyote itakavyokuwa, Zul-qarnain aliweza kwenda mahali halisi ambako jua linachomozea. Jambo hili linathibitisha maoni ya Kurani kuwa dunia ina umbo bapa. Kitu muhimu zaidi ni kuwa alikwenda mahali jua linapozamia, na akakuta kuwa linazama kwenye chemchemi nyeusi na yenye matope.
Ukiwauliza wanajimu endapo jua linazama kwenye chemchemi yenye matope watakwambia "hapana.’
Hitimisho: Kurani inafundisha mambo yafuatayo:
Dunia ina umbo bapa, imeenea kama zulia na imefungwa kuwa bapa kwa vigingi ambavyo ni milima
Dunia ina njia yake ambayo imewekewa mipaka wakati wa mchana, kisha huzama kwenye chemchemi nyeusi na yenye matope wakati wa usiku na huenda kwenye kiti cha enzi cha Allah.
Baadaye jua huchomoza kutoka kwenye sehemu moja maalum
Ukiachia nyota (sayari) tano "zenye kwenda nyuma", nyota zimening’inizwa kama taa
Muhammad aliwafundisha Waislam wa mwanzo jambo hili kama ukweli halisi, siyo sitiari au mlinganisho.
ALLAH AMESHINDWA KUTUTHIBITISHIA KUWA ALIUMBA DUNIA ZAIDI YA KUONYESHA KUWA HAJUI DUNIA INA UMBO GANI.
Kumbe Allah hakuumba dunia.
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW