Friday, September 2, 2016

WAISLAM WANAMTUKANA MWENYEZI MUNGU KUWA NI KAHABA

Eti Mungu wa Biblia ni Kahaba Kulingana na Isaya 23:17-18
Kama kawaida yao, Waislamu wanaendelea kudanganywa na walimu wao na kujipa matumaini kuwa wako kwenye njia ya uzima kutokana na kile wanachoamini kuwa Biblia si Neno la Mungu bali Quran ndiyo Neno la Mungu.
Kwa sababu wanaonekana ni watu wasiokuwa na utayari wa kuchunguza kile wanachoambiwa, basi wanaamini kila uongo na udanganyifu wanaopewa na kuubeba kama ulivyo na kuutangaza kwa ujasiri kabisa kana kwamba ndiyo kweli halisi!
Mojawapo ya uongo mkubwa na wa wazi unahusu aya zilizoko kwenye kitabu cha Isaya. Aya hizo zinasema hizi:
Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, Bwana ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia. Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa Bwana, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za Bwana, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari. (Isaya 23:17-18).
Waislamu hulishikilia andiko hili kwa nguvu na kwa kejeli nyingi wakisema, “Mnaona ninyi Wakristo’ Mungu wenu ni kahaba. Mungu gani wa kufuata huyu. Njoni kwa Allah.”
Kwa Wakristo wasio makini, maandiko ya aina hii yanawapotosha kabisa na kuwafanya waone Ukristo kuwa ni dini ya uongo kiasi cha wao kuamua kungia kwenye Uislamu – kumbe wasijue kuwa wanatoka uzimani na kutumbukia mautini. Uongo wa namna hii ni mwingi mno miongoni mwa Waislamu na unaenezwa kupitia intaneti, mihadhara, mabishano ya ana kwa ana, vitabu na kadhalika. Kuna mamia ya aya za Biblia ambazo wamezipotosha na ndizo watakazozitumia kukuondoa Yerusalemu Mpya. Je, wewe ni mmoja wa waliodanganywa na kunaswa?

Kama wewe ni Mkristo na unadhani unataka kuacha Ukristo kwa sababu Waislamu “wamekuhubiria Biblia” na ukafikiri Biblia ni uongo, nakushauri uliza kwanza kwa wachungaji, walimu na waumini wengine kabla ya kuamini maneno ya Waislamu kuhusiana na Biblia.
Kati ya jambo moja gumu sana katika uandishi ni kuhamisha maana kama ilivyo kutoka lugha moja hadi nyingine wakati wa kutafsiri. Hii si kwa Kiswahili tu bali kwa lugha zote duniani; na sababu ni kuwa si kila neno au msemo ulio katika lugha moja uko kwenye lugha zingine. Kwa mfano, Kiingereza kina maneno ‘he’ kwa ajili ya wanaume na ‘she’ kwa ajili ya wanawake lakini Kiswahili hakina tofauti hiyo kabisa. Kwa hiyo, mtu akitafsiri kwa Kiswahili sentensi ya Kiingereza yenye neno ‘he’ atatumia neno lilelile ambalo atalitumia anapotafsiri sentensi yenye neno ‘she’. Matokeo yake, anayekuja kusoma tafsiri ya Kiswahili anaweza kuikosa maana iliyokusudiwa. Na pale anapokutana na mdanganyifu ndipo hatari inakuwa kubwa kwa yeye kupotoshwa.
Basi turudi kwenye andiko hili na tulisome tena:
Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, Bwana ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia. Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa Bwana, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za Bwana, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari. (Isaya 23:17-18).
Unaposoma aya hizi, kwa harakaharaka utadhani kana kwamba maneno NAYE na ATAFANYA yanamwongelea Bwana – yaani kwamba Bwana atakapoizuru Tiro basi atapata ujira wake na pia atafanya ukahaba.
Lakini hii ni kwa sababu katika Kiswahili hayabainishi jinsi ya kike au ya kiume. Ukisoma kwa Kiingereza imeandikwa hivi:
And it shall come to pass after the end of seventy years, that the LORD will visit Tyre, and she shall turn to her hire, and shall commit fornication with all the kingdoms of the world upon the face of the earth. And her merchandise and her hire shall be holiness to the LORD: it shall not be treasured nor laid up; for HER merchandise shall be for them that dwell before the LORD, to eat sufficiently, and for durable clothing.
Katika Biblia YOTE Bwana huwa anatajwa kama HE na sio SHE. Tazama mfano ufuatayo kutoka Zaburi 147:12-20.
Praise the LORD, O Jerusalem; praise thy God, O Zion.
For he hath strengthened the bars of thy gates; he hath blessed thy children within thee.
He maketh peace in thy borders, and filleth thee with the finest of the wheat.
He sendeth forth his commandment [upon] earth: his word runneth very swiftly.
He giveth snow like wool: he scattereth the hoarfrost like ashes.
He casteth forth his ice like morsels: who can stand before his cold?
He sendeth out his word, and melteth them: he causeth his wind to blow, and the waters flow.
He sheweth his word unto Jacob, his statutes and his judgments unto Israel.
He hath not dealt so with any nation: and as for his judgments, they have not known them. Praise ye the LORD.
Kwa hiyo, tunaposoma andiko hilo la Isaya kwa Kiingereza, tunakuta kuwa linaongelea Tyre (yaani Tiro) na linasema: “and she shall turn to her hire” na sio “and HE shall turn to her hire”! Pia linasema: “And her merchandise and her hire…” na sio “And HIS merchandise and HIS hire…”
Pia ikumbukwe kuwa ukahaba unapotajwa kwenye Biblia kuhusiana na nchi au watu wote kwa ujumla, una maanisha kumwacha Mungu aliye hai na kwenda kutafuta msaada ama kwa miungu mingine au kwa nchi nyingine. Kwa mfano, katika sura ya 16 ya kitabu cha Ezekieli, Mungu anaongelea taifa la Israeli, kwamba aliwachukua katikati ya mataifa akawafanya kuwa taifa takatifu, lakini wao kama taifa wakawa waasi kwa kumwacha Mungu wa kweli na kufuata miungu mingine. Kitendo hiki Mungu anakiita ni ukahaba:
Neno la Bwana likanijia tena, kusema, Mwanadamu, uujulishe Yerusalemu machukizo yake, useme, Bwana MUNGU auambia Yerusalemu hivi; Asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya Mkanaani; Mwamori alikuwa baba yako, na mama yako alikuwa Mhiti. Na katika habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo, wala hukutiwa katika nguo kabisa. Hapana jicho lililokuhurumia, ili kukutendea lo lote la mambo hayo kwa kukuhurumia; lakini ulitupwa nje uwandani, kwa kuwa nafsi yako ilichukiwa, katika siku ile uliyozaliwa. Nami nilipopita karibu nawe, nikakuona ukigaagaa katika damu yako, nalikuambia, Ujapokuwa katika damu yako, uwe hai; naam, nalikuambia, Ujapokuwa katika damu yako, uwe hai ….. Nikakupamba kwa mapambo pia, nikatia vikuku mikononi mwako, na mkufu shingoni mwako …… Lakini uliutumainia uzuri wako, ukafanya mambo ya kikahaba kwa sababu ya sifa zako, ukamwaga mambo yako ya kikahaba juu ya kila mtu aliyepita; ulikuwa wake. Ukatwaa baadhi ya mavazi yako, ukajifanyia mahali palipoinuka, palipopambwa kwa rangi mbalimbali, ukafanya mambo ya kikahaba juu yake; mambo kama hayo hayatakuja wala hayatakuwako. (Ezekieli 16:1-16).
Tunapata mfano mwingine ulio wazi zaidi kutoka katika kitabu cha Waamuzi. Imeandikwa:
Lakini hawakuwasikiliza hao waamuzi wao, maana walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine, wakajiinamisha mbele yao; wakageuka upesi, na kuiacha njia ile waliyoiendea baba zao, waliozitii amri za Bwana bali wao hawakufanya hivyo. (Waamuzi 2:17).
Hitimisho
Andiko la Isaya 23:17-18 limepotoshwa na ‘wahubiri’ wa kiislamu na kupewa maana ua UONGO isiyokuwapo kwenye Biblia. Mungu wetu si kahaba!!
Huu wanaotoa walimu hawa ni unabii wa uongo; usikubali kudanganywa na kupoteza roho yako. Hautakuja kuwambia Mungu siku hiyo kwamba “Mimi sikujua. Nilidhani wanasema kweli.” Biblia ni Neno la kweli la Mungu na ni chakula cha roho kwa ajili ya uzima wa milele. Usitoke humo kamwe!
Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua. (Mathayo 7:15-20).
Je, utakubali kudanganywa hadi lini?
Tafakari
Hoji mambo
Chukua hatua

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW