Monday, July 11, 2016

TOFAUTI KUMI (10) KATI YA ISA WA KWENYE QURAN NA YESU WA KWENYE BIBLIA.



ISA WA QURAN KAZALIWA CHINI YA MTENDE WAKATI YESU WA KWENYE BIBLIA KAZALIWA KWENYE ZIZI LA NG'OMBE
TOFAUTI KUMI (10) KATI YA ISA WA KWENYE QURAN NA YESU WA KWENYE BIBLIA.
Taarifa za Malaika kabla ya kuzaliwa kwao, kadiri ya Qurani na Biblia.
Jibrili alivyomtokea Mama wa Isa == Gabrieli alivyomtokea mama wa Yesu:
A. MARYAM ALIKUWA MSIKITINI vs. MARIAM ALIKUWA NYUMBANI KWAKE:
1. WAISLAM-JIBRIL Alienda kwa Mariamu aliyekuwa Msikitini Qurani 19:16-17
2. WAKRISTO-GABRIEL Alienda kwa Mariamu aliyekuwa nyumbani kwake - Lk 1:26-28
B. MARYAM HAJULIKANI ANAISHI WAPI vs MARIAM ANAYE ISHI NAZARETI:
1. WAISLAM-Mariamu Mama wa Isa haijulikani aliishi kijiji kipi wala mji gani wala hata nchi haijulikani. Isitoshe Quran inasema kuwa Jibril ndiye aliyemletea utume Muhammad asiwapelekee Mayahudi (hana kosa) Sura 2:97
2. WAKRISTO-Lakini Mariamu Mama yake Yesu alitokewa na Malaika Gabriel akiwa katika kijiji cha Nazareti mji wa Galilaya nchi ya Israeli (Lk 1:26) Mariamu Mama wa Yesu ni Myahudi.
C. JIBRIL HAKUMSALIMIA MARYAM vs GABRIEL ALIYE MSAMILIA MARIAM:
1. WAISLAM-Jibrili hakutoa salamu kwa Mariamu mama wa Isa ila alijimithilisha kwa umbo la binadamu aliye kamili - Sura 19-17
2. WAKRISTO-Malaika Gabrieli alimsalimia Mariamu Mama wa Yesu – Luka 1:28
D. JIBRIL ALISEMA YEYE NDIE ANATOA MTOTO vs . GABRIEL ALIYE SEMA KUWA MARIAM ATACHUKUA MIMBA:
1. WAISLAM-Jibril alimwambia Mariamu kwamba mimi ni mjumbe wa mola wako ili nikupe mwana mtakatifu - Sura 19-19
2. WAKRISTO-Lakini malaika Gabrieli alimwambia mama wa Yesu kuwa utachukua mimba – Luka1: 31
E. JIBRIL HAKULIJUA JINA LA MTOTO vs. GABRIEL ALIYE SEMA KUWA MTOTO ATAITWA YESU:
1. WAISLAM-Jibrili alisema kwa Mariamu kuwa ili tumfanye mtoto muujiza kwa wanadamu – Sura 19: 21. Isitoshe Jibrili hakutaja jina la mwana kwa Mariamu. Bali alisema ili nikupe mwana mtakatifu.
2. WAKRISTO-Malaika Gabrieli alisema kwa Mariamu mama ya Yesu kuwa mtoto jina lake utamwita Yesu (Luka 1:31; 2:21) Gabrieli hakusema kuwa atampa mwana Mariamu. Bali alisema, Roho mtakatifu atakujilia juu yako, yaani motto atazaliwa kwa uwezo wa Mungu.
TOFAUTI YA KUZALIWA KWA ISA NA YESU
Isa bin Mariam vs. Yesu Kristo
F. ISA KAZALIWA CHINI YA MTENDE vs YESU KAZALIWA KWENYE HORI LA NG'OMBE:
1. WAISLAM-Isa alizaliwa katika shina la Mtende –Quran 19:23
2. WAKRISTO-Yesu kazaliwa katika hori la kulishia ng’ombe. Luka 2:7
G. MIMBA YA ISA HAIJULIKANI ILKUWA YA MUDA GANI vs. YESU ALIYE ZALIWA KWA SIKU ZAKE ZILIPO KAMILIKA:
1. WAISLAM-Kuzaliwa kwa Isa haijulikani mimba ya mama yake ilichukua muda gani maana malaika Jibrili alisema nikupe mwana mtakatifu mara akachukua mimba na kuzaa. (19: 22-23)
2. WAKRISTO-Lakini Mariamu Mama wa Yesu siku zake za kuzaa zilitimia. (Luka 2:6-7)
H. ISA HAKUTABIRIWA KWENYE QURAN vs. YESU ALITABIRIWA KWENYE BIBLIA:
1. WAISLAM-Qurani haionyeshi kama Isa alitabiriwa na manabii kuwa atazaliwa
2. WAKRISTO-Lakini Biblia inatuthibitishia kuwa Manabii walitabiri kuzaliwa kwa Yesu, (Isaya 7: 14; 9:6) utabiri huu ulitolewa na Nabii Isaya miaka 750 kabla ya Yesu kuja kuzaliwa nao ulitimia (Mathayo 1:18-23)
I. ISA HAJULIKANI ALIZALIWA WAPI AU KIJIJI KIPI vs. YESU ALIYE ZALIWA BETHLEHEM:
1. WAISLAM-Isa haijulikani alizaliwa katika kijiji gani wala mji, wala nchi aliyozaliwa Qurani haikueleza.
2. WAKRISTO-Biblia inatujulisha kuwa Yesu alizaliwa Bethelehemu ya Uyahudi katika Mji wa Daudi umbali wa maili 5 toka kusini mwa Yerusalemu nchi ya Israeli (Lk 2:8-16). Kuzaliwa kwake mahali hapo pia ni kutimiza unabii uliotolewa na nabii Mika miaka 750-686 kabla ya kristo kuja wakati wa wafalme hawa wakitawala – Jotham, Ahaz na Hezekia wafalme wa Yuda. Yesu mwenyewe alizaliwa kama mwaka wa 4 wakati wa Mfalme Herode.
J. ISA ALIONGEA AKIWA MTOTO MCHANGA vs. YESU HAKUONGEA AKIWA MTOTO MCHANGA:
1. WAISLAM-Isa aliongea na watu akiwa mototo mchanga, na kusema kuwa yeye ni mja wa Mungu amepewa kitabu na amefanywa Nabii (Sura 19:30-33)
2. WAKRISTO-Yesu hakuongea na mtu akiwa mtoto mchanga. Alianza kuwauliza maswali na kutoa majibu akiwa na wazee Hekaluni akiwa na miaka 12. (Luka 2: 42-49)
Hivyo tunaona kwamba tuna tofauti nyingi tu kati ya Bwana Yesu na Isa. Swali kwako mfuatiliaji je, Isa bin Maryamu ndiye Bwana Yesu Mwokozi? Tafakari.
Mungu awabariki sana na tuendelee kujifunza tofauti za Isa wa Quran na Yesu wa Biblia.
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
Max Shimba Ministries Org.

1 comment:

Anonymous said...

Wewe bado haujaisoma biblia kama ianavyotakiwa Bali unaisoma kama gazeti ndiomaana hujapaona wapi yesu alipoongea wakati akiwa mtoto kwasababu mambo mengi humu nimeyaona umeyaboronga mengi sana kajifunze tena

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW