Swali la Yesu ni Mungu na nani alikuwa anamwomba, huwa linaleta utatanishi mkubwa sana na kama usipo kuwa makini, unaweza kuanza kuuliza maswali katika imani yako ya Ukristo. Katika mijadala mbali mbali ya kidini, wanadhuoni wa Kiislam na hata Mashahidi wa Yehova huwa wanauliza:- Yesu alipo kuwa katika Bustani ya Gethemane, alikuwa anamwomba nani? Tena zaidi ya hapo, wanauliza, tokea lini Mungu akaomba msaada? Hakika maswali haya yanahitaji majibu thabit tena yenye aya za Biblia.
Ili umwuelewe Yesu kama Mungu duniani akiomba kwa Baba yake mbinguni , tunahitaji kutambua kwamba Mungu Baba na Yesu “Mwana” walikuwa na uhusiano wa milele kabla ya Yesu kuuchukua mwili wa mwanadamu. Zaidi ya hapo, itakupasa uelewe kuwa, Yesu alipo kuwa duniani alikuwa na asilia mbili, yaani Yesu alikuwa Mungu na wakati huo huo alikuwa Binadamu (Rejea katika Kijarida cha “Asilia mbili za Yesu Kristo”). Tafadhali soma Yohana 5:19-27, hasa mstari wa 23 ambapo Yesu anafundisha kwamba Baba alimtuma Mwana (pia tazama Yohana 15:10.
Katika Isaya 9:6 inatuambia kwamba Mwana alipeanwa na mtoto alizaliwa. Yesu alikuwa daima sehemu ya utatu, pamoja na Roho Mtakatifu. Utatu ulikuwa kila mara, kama, Mungu Baba , Mungu Mwana, na Mungu Roho, si miungu mitatu, lakini Mungu ni mmoja anajidhihirisha kama watu watatu. Yesu alifundisha kwamba Yeye na Baba yake ni kitu kimoja (Yohana 10:30), kumaanisha kwamba Yeye na Baba yake ni wa kiini kimoja na asili moja. Baba, Mwana na Roho ni watu watatu walio na ushirikiano sawa wakiwepo kama Mungu. Hawa watatu walikuwa, na wataendelea kuwa na uhusiano wa milele. Hawa watatu walikuwepo kabla ya mwanzo kuwepo na wataendelea kuwepo milele na milele yote.
Wakati Yesu, mwenye asili mbili kwa wakati mmoja, yaani Mungu na Binadamu, (Isaya 9:6) aliuchukua ule mwili wa mwanadamu usio na dhambi Yeye pia alichukua namna ya mtumwa, kupeana utukufu wake wa mbinguni (Wafilipi 2:5-11). Yesu Kama “Mwanadamu”, alikua na kujifunza utiifu (Waebrania 5:8) kwa Baba yake hasa wakati wa kujaribiwa na Shetani, alishitakiwa uongo na wanadamu, kukataliwa na watu wake, na hatimaye alisulubiwa. Kuomba kwa Baba yake mbinguni kulikuwa kwa kumwomba nguvu (Yohana 11:41-42) na hekima (Marko 1:35, 6:46), HAYO YOTE ALIFANYA KAMA MWANADAMU. Kuomba kwake kulionyesha utegemezi wake kwa Baba yake katika ubinadamu wake ili atekeleze mpango wa ukombozi wa Baba yake, kama ilivyoshuhudiwa katika Yohana 17. Kuomba kwake kulionyesha kwamba Yeye hatimaye alijisalimisha kwa mapenzi ya Baba yake, ambayo ilikuwa ni pomoja na kwenda msalabani kulipa adhabu (kifo) kwa kuvunja kwetu sheria Mungu (Mathayo 26:31-46). Bila shaka, Alifufuka katika mwili kutoka kaburini, akishinda msamaha na uzima wa milele kwa wale ambao watatubu dhambi zao na kumwamini kama Mwokozi.
Hivyo basi, hakuna tatizo kwa Mungu Mwana kuomba au kuzungumza na Mungu Baba. Kama ilivyotajwa, walikuwa na uhusiano wa milele kabla ya Kristo awe mwadamu. Uhusiano huu ni taswira katika Injili ili tuweze kuona ni jinsi gani Mwana wa Mungu katika ubinadamu wake ulitekeleza mapenzi ya Baba yake, na katika kufanya hivyo, kulinunua ukombozi kwa ajili ya watoto wake (Yohana 6:38). Kwa kuendelea kujiwasilisha kwa Baba yake mbinguni Kristo daima aliwezeshwa na kutiwa nguvu na akabaki kuwa na lengo katika maisha yake ya maombi. Mfano wa Kristo wa maombi ni wetu kuufuata.
Yesu Kristo hakuwa chini ya Mungu duniani wakati anaomba kwa Baba yake mbinguni, kumbuka kuwa, Yesu alikuwa na asilia Mbili, -Mungu na Binadamu. Alikuwa anaonyesha jinsi hata katika ubinadamu wa dhambi ni muhimu na maisha ya maombi ili kufanya mapenzi ya Baba yake. Kuomba kwa Yesu kwa Babaye kulionyesha mfano wa uhusiano ulioko katika Utatu wake na mfano kwetu sisi, kwamba ni lazima tumtegemee Mungu kwa nguvu na hekima tunahitaji kwa njia ya maombi. Tangu Kristo, kama Mungu -mwanadamu, alihitaji kuwa na maisha mahiri ya maombi, hivyo ndivyo inavyowapasa wafuasi wa Kristo hii leo.
Hivyo basi, Yesu kuomba kwa Baba yake, alifanya hivyo kama Binadamu (Yohana 17), ingawa wakati huohuo, yeye alikuwa ni Mungu (Rejea katika Kijarida cha “Asilia Mbili za Yesu Kristo http://maxshimba.blogspot.com/…/asilia-mbili-ya-yesu-kristo… ”). Huu ni uthibitisho tosha kuwa, tokea Dunia hii iumbwe, hakujawai tokea mtu kama Yesu Kristo. Yesu Anaombwa/prayed (Matendo ya Mitume 7:59), wakati huo huo tunasoma kuwa Yesu Anamwomba Mungu Baba (Yohona 17)
Hakika Yesu Ni Mungu.
Kwa Maswali zaidi wasiliana nasi katika
maxshimbaministries@gmail.com
maxshimbaministries@gmail.com
Imeletwa kwenu na Max Shimba
Kwa Max Shimba Ministries Org.
@2015, April.
No comments:
Post a Comment