Saturday, August 8, 2015

YESU NI MUNGU KUTOKANA NA QURAN (SEHEMU YA TATU)

Ndugu msomaji,
Quran inasema kuwa Allah ni Al-Malik al-Mulk, ikimaanisha kuwa ni mmiliki wa kila kitu. Je, hii sifa ya Al-Malik al-Mulk inapatikana kwa Yesu aliye hai?

Hebu tuanze utafiti wetu kwa kusoma Quran na tujionee wenyewe kama kweli Yesu ni Mungu au la.
Moja ya sifa au adhama ya Mungu kutokana na Quran: ni Al-Malik al-Mulk, ikimaanisha MMILIKI WA KILA KITU. Hii sifa ya Al-Malik al-Mulkh ni moja ya Majina 99 ya Allah wa Quran.

Je, Yesu anayo hiyo sifa ya MMILIKI WA VYOTE "Al-Malik al-Mulkh"? Haya tusome kwanza Quran na tuone kama Allah anayo hii sifa ya Al-Malik al-Mulkh.

Surat YA-SIN 83. Basi Mtukufu ametakasika na kila kisicho laiki na dhati yake, yule ambaye katika kudra yake upo Ufalme wa kila kitu, kwa kuumba, na kupanga, na kuendesha - Kwake Yeye peke yake mtarejeshwa, akuhisabuni kwa a'mali zenu.

Allah anasema kuwa yeye ni Mmiliki wa vyote kwenye Quran iliyo andikwa miaka mia 632 AD baada ya Yesu. Je, Yesu anayo hii sifa ya Mmilikiwa vyote?

YESU ANASEMA HIVI:Matayo 11: 27“Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu:
hakuna mtu amjuaye Mwana ila Baba, wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana na ye yote ambaye Mwana anapenda kumdhihirisha Baba kwake.’’

Ikimaanisha kuwa Yesu ndie aliye kuwa wa kwanza kukiri haya maneno kuwa yeye ni mmiliki wa vyote kutokana na ushahid wa Biblia iliyo tangulia miaka 632 kabla ya Quran. YESU ANASEMA KUWA "AMEKABIDHIWA VITU VYOTE". Ikimaanisha hata Muhammad sasa yupo chini ya Yesu.

YESU ANAEDELEA KUSEMA katika Yohana 16 aya ya 15 Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu. Ndiyo maana nimesema Roho atachukua yaliyo Yangu na kuwajulisha ninyi.
Yesu anasema kuwa kila kitu ambacho ni cha Baba yake ni chake. Hapo teyari tumemaliza kazi maana hakuna atakaye bisha kuhusu hii aya iliyo kamilika na kuto kuwa na shaka ndani yake. YESU NI MMILIKI WA KILA KITU.

Sasa kati ya Yesu aliye sema haya maneno miaka mia 632 kabla ya Allah, na Allah aliye kuja baadae na Quran iliyo jaa shaka, nani tutamwamini? Wakwanza ambaye ni Yesu au Allah ambae anaigizia kwa Yesu?
Ndugu zanguni, huu ni ushahid tosha kuwa Yesu ni Mungu, maana leo tumejifunza kuwa Yesu alisema na kuitwa MMILIKI WA VYOTE MIAKA 632 kabla ya Kuandikwa kwa Quran.

Sasa kati ya Biblia iliyo kuja kabla ya Quran na Quran iliyo kuja baada ya Biblia, wewe utafuata kitabu kipi? Watafiti wa mambo mbali mbali huwa wanatumia data za awali katika kuhakiki na kuthibitisha jambo. Na data tuliyo nayo kuhusu MMILIKI wa vyote ambayo ni ya awali ipo kwenye Biblia na inasema kuwa MMILIKI WA VYOTE NI YESU.

Leo nimejibu hoja ya Waislam kuwa, Je, Yesu ni Mungu? Koran pamoja na Allah wanasema kuwa Yesu ni Mungu kwa kuwa Yesu anazo adhama zote na/au sifa zote za Mungu na moja ya sifa hizo ni AL-MALIK AL MULK.
Katika huduma yake,
Max Shimba
Copyright © Max Shimba Ministries 2015

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW