KUUFAHAMU UANAJESHI WA KIISLAMU ULIOINUKA TENA
Mahojiano na Mama yake Kijana aliyejilipua kwa
MABOMU YA KUJITOA MHANGA
GAZETI MOJA la kila siku litolewalo kwa lugha ya Kiarabu huko Uingereza liitwalo Al-sharq Al-Awsat lilichapisha mahojiano na Umm Nidal, mama yake shahidi (mfia dini) Muhammad Farhat. Wakati wa Intifada ya kwanza Umm Nidal alimficha ‘Imad ‘Aql, kamanda wa kikosi cha jeshi la Hamas “Izz Al-Din Al-Qassan Brigedia” kwenye nyumba ya familia kwa zaidi ya mwaka. Ifuatayo ni dondoo kutoka katika mahojiano:
Swali: Ni kwa vipi wazo la kujihusisha na operesheni ya Fidaai (kujitoa mhanga) lilivyo jengeka ndani ya nafsi ya mwanao, Muhammad?”
Umm Nidal: “Jihad ni amri ya kidini iliyoamriwa kwetu. Ni lazima tuliingize wazo hili katika nafsi za watoto wetu, muda wote... Kile tukionacho kila siku - mauaji ya kinyama (ya watu wengi wasiokuwa na hatia); ulipuaji (wa) nyumba kwa mabomu, - hayo yaliimarika katika mioyo ya watoto wangu wa Kiume, hasa Muhammad, kupenda Jihad na kujitolea mhanga”
Swali: “Je, ulikuwa na wajibu wowote katika kupandikizia roho hii kwa Muhamad?”
Umm Nidal: “Allah asifiwe, mimi ni Mwislamu na naamini katika Jihad. Jihad ni msingi mmojawapo wa imani yetu na hili ndilo lililonitia moyo mimi kumtoa dhabihu Muhammad katika Jihad kwa ajili ya Allah. Mwanangu hakuharibiwa, hajafa, anaishi maisha ya furaha zaidi yangu. Kama mawazo yangu yangekuwa yamefungwa na mpaka wa dunia hii, nisingemtoa dhabihu Muhammad.”
“Mimi ni mama mwenye huruma kwa watoto wangu, nao wananihurumia na kunitunza. Kwa vile nampenda mwanangu, nilimtia moyo afe kifo cha mashujaa wafia dini kwa ajili ya Allah….Jihad ni wajibu uliowekwa juu yetu, na ni lazima tuuchukue. Nilimtoa dhabihu Muhammad kama sehemu ya wajibu wangu.”
“Hili ni jambo rahisi. Hakuna kutokukubaliana (mioyoni mwa wanazuoni) katika mambo haya. Furaha iliyoko katika dunia hii ni furaha ambayo haijakamilika; furaha ya milele ni uzima katika ulimwengu ujao, kupitia kujitoa mhanga. Allah asifiwe, mwanangu ameipata furaha hiyo.”
Swali: “ ‘Imad ‘Aql aliishi pamoja na wewe, na aliuwawa nyumbani mwako. Je,haiba yake ilimshawishi Muhammad?”
Umm Nidal: “Muhammad alikuwa na miaka saba wakati mfia dini ‘Imad ‘Aql alipoishi pamoja nasi nyumbani. Muhammad alijiunga na kikosi cha (Izz Al -Din) Brigedia ya Al-Qassan akiwa na miaka saba. Kuachilia mbali umri wake mdogo alikuwa (ni) msaidizi wa ‘Imad ‘Aql, kamanda wa Al-Qassan katika Ukanda wa Gaza. Wakati ambapo kaka zake hawakuwepo, angechungulia barabarani na kupeleka ujumbe kutoka kwa Aql kwenda kwa Majahidina. Mfia dini Muhammad alikuwa mwanafunzi wa Imad. Muhammad angemsikiliza ‘Imad na kumwangalia akipanga mikakati yake ya mashambulizi.”
“Imad aliishi pamoja nasi kwa miezi 14, na alikuwa na chumba katika nyumba yetu ambapo alipangia mashambulizi yake. Majahidina walikuwa wakija kwake na kupanga kuweka tayari kila kitu na kijana mdogo Muhammad akiwa pamoja nao, akiwaza na kupanga. Hii ikawa chanzo cha Muhammad kupenda kujitoa mhanga.”
“Hii ndiyo hali iliyoendeleza upendo wa kujitoa mhanga katika nafsi ya Muhammad. Mimi kama mama, kwa asili nilichochea upendo wa Jihad katika nafsi ya Muhammad na katika nafsi ya wanangu wote, ambapo wote ni wa kikosi cha Brigedia ya Al-Qassan. Mwanangu mkubwa Nidal (31), anatafutwa sasa na Waisraeli. Mwanangu wa pili alitegeshea shambulizi la kujitoa mhanga, lakini aligunduliwa akawekwa ndani na kuhukumiwa miaka 11 jela. Ninaye mwana mwingine (Mu’min Farhat) ambaye ni mlinzi wa Sheikh Ahmad Yassin.”
“Hali ya hewa ambapo Muhammad alikuziwa ilikuwa imejaa imani na mapenzi ya kujitoa mhanga. Ninashikilia kwamba imani ya mtu haitafikia ukamilifu hadi achukue hatua ya kutoa dhabihu nafsi yake…”
Swali: “Muhammad alisemaje kwa heri kabla ya kuchukua hatua ya shambulizi?”
Umm Nidal: “Muhammad alikuwa tayari kuchukua shambulizi lolote la kujitoa muhanga…Aliniapia mimi kwamba sababu yake pekee ya kupenda maisha ni kwa sababu ya Jihad. Alikuwa akiniambia kama zamu yake ya Jihad isingefika angeachilia mbali vuguvugu la mkono wa kijeshi la kikosi chao, achukue silaha yake na kuingia kwenye uwanja wa vita akapigane kivyake vyake.”
“Alijaribu mara nyingi, alikuwa akienda nje kwenye barabara ya Al-Muntar akiwa amebeba bunduki yake na mabomu, lakini nafasi ikawa haijatokea. Alikuwa akirudi damu yake ikichemka kwa sababu hakufanikiwa kufanya shambulizi. Alikuwa akitia tahabibusilaha yake na kuniambia: ‘Mama, huyu ni bibi arusi wangu’ Aliipenda sana bunduki yake.”
“Alikuwa akiniambia, ‘Nakwenda nje sasa( kwenye shambulizi). Siwezi kuizuia tena nafsi yangu’ Nilikuwa namjibu, ‘Bado hujawa na fursa kubwa ya kutosha. Kuwa mvumilivu, panga vizuri ili kwamba usitoe nafsi yako sadaka bure bila kitu. Tenda kwa dhamira sio kwa msisimko…”
“Siku ile ya shambulio alinijia akaniambia: ‘Sasa mama, ninajipanga kwenda nje kwa ajili ya shambulio langu. Alijiandaa kwa shambulio siku mbili kabla; wakati wa kuchukua mkanda wa video aliniambia nipige picha pamoja nae, na wakati picha zinachukuliwa alikuwa akitia tahabibu bunduki yake. Mimi binafsi niliambiwa kuchukua video pamoja nae kama ukumbusho.”
“Alitoka nje kufanya shambulizi, na alipofika kwenye eneo alikaa usiku mzima na rafiki zake pale. Nilikuwa nawasiliana nae na nikamuuliza juu ya msisimko wake. Aliniambia alikuwa na furaha sana, Kwa kweli niliuona uso wake ukiwa na furaha kuliko nilivyowahi kuona.”
“Aliondoka kwenda kwenye shambulio lake akiwa baridi kabisa, mtulivu sana na mwenye kujiamini, kana kwamba alishawishika kuwa shambulizi litafanikiwa.”
“Lakini niliogopa na kuhofia sana kuwa shambulizi lisingefanikiwa na hivyo angekamatwa. Nilimwombea alipoondoka nyumbani na kumwambia Allah alifanikishe shambulizi na ampe kuwa shujaa mfia dini. Alipoingia kwenye makazi kaka zake walioko jeshini kikosi( cha) Hamas walinitaarifu kuwa alifanikiwa kupenyeza ndani. Kisha nikaanza kumwomba Allah kwa ajili yake.”
“Niliomba kutoka katika kina cha moyo wangu kwamba Allah alifanye shambulizi lifanikiwe. Nikamwambia Allah anipe (Waisraeli )10 kwa Muhammad, na Allah akanikirimia sawa na maombi yangu na Muhammad akatimiza ndoto zake kwa kuua Waisraeli 10, walowezi na maaskari, Mungu wetu alimheshimu zaidi sana, katika hilo kulikuwa na Waisraeli wengi waliojeruhiwa.”
“Shambulizi lilipomalizika, vyombo vya habari vilitangaza habari hizo. Halafu kaka yake Muhammad akanijia na kunipasha habari za ushujaa wake . Nilianza kulia, Allah ni mkuu kuliko wote; na kuomba na kumshukuru Allah kwa mafanikio ya tukio hilo.Nikaanza kutoa kilio cha furaha na tulitangaza kwamba tulikuwa na furaha. Vijana walianza kupiga risasi hewani kwa furaha juu ya ushindi wa shambulizi kwani hivi ndivyo tulivyotumaini juu yake.”
“Baada ya shambulizi moyo wangu ulikuwa na amani kuhusu Muhammad, niliwatia moyo watoto wangu wa kiume wote wafe kifo cha kujitoa mhanga, na nilitamani hili hata kwa nafsi yangu mwenyewe. Baada ya haya yote, nilijiandaa kuupokea mwili wa mwanangu, shahidi mkamilifu, ili kumwangalia mara moja ya mwisho na kuwapokea wapongezaji waliokuwa wamekuja kwetu kwa idadi kubwa na kushiriki katika furaha yetu juu ya kujitoa mhanga kwa Muhammad.”
MAONI YA MHARIRI: Ni aibu kwamba roho ya uanajeshi ya kujitoa dhabihu kweli imeondoka kutoka kwenye Ukristo. Wazazi wa Kikristo walikuwa wakiwatoa dhabihu watoto wao (na nafsi zao) kwenye utume wa kimisheni sehemu mbalimbali duniani kinyume na mafundisho ya Kiislam ya Jihad (vita takatifu) ambayo inachochea chuki na vurugu.
Wanafunzi wengi wasio na idadi wa Yesu waliyatoa maisha yao kwa tumaini la kuzileta roho zilizopotea kwa Kristo na kuwanyakua kutoka katika umilele Jehanamu. Kweli Yesu aliweka wazi wakati aliposema kwamba kama yeyote akitaka kuwa mwanafunzi wake, ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake na amfuate.
Yesu hataki sisi tufe hata mara moja kama hawa Waislam wanao jilipua kwa mabomu, lakini anatutaka tufe katika nafsi zetu siku kwa siku ili utukufu wake uweze kutimizwa ndani yetu.
Je, tutakufa kwa ajili ya Mwokozi wetu kwa ari ileile kama hawa Waislam? Au tuta kazania kuishi maisha yetu ya raha, yaliyojaa kujijali? Tutakuwa na furaha tu ya kwenda kanisani?
Je, unampenda Bwana kwa kiasi gani? Je, waweza kufa kwa ajili yake? Alikufa kwa ajili yako. Kama ungependa kuunganisha nguvu zako pamoja nasi katika vita ya kuziokoa nafsi zinazopotea, tafadhali wasiliana nasi kwa anuani zilizopo mwishoni mwa makala haya.
Kifo cha Al-Masih (Yesu) msalabani kinafunua kina cha upendo wa Mungu, kwani kwa dhabihu hii, wokovu ulifanywa kupatikana kwa watu wote wa jamii zote ambao wanaiweka imani yao kwa Al-Masih.
Waislam wanamuona Allah kama Mungu mwenye nguvu.
Wakristo wanamuona Mungu kama Mungu wa upendo.
KWA UJUMLA, Allah alionekana kwa wenye dini kamilifu wa Kiislam, kama Mungu mwenye nguvu. Kati ya majina 99 ya Allah, majina yanayoonekana maarufu ni majina yale yanayozungumzia nguvu ya Allah, kama vile Al-Jabbar,Al-Qabar, Al-Azim,Al-Kabirna Al-Muntaaqim. Zaidi ya yote mkusanyiko wa vilio ambao umezoeleka sana kwa Waislam duniani mwote ni Allahu Akbar,Allah Akbar; (Mungu ni mkubwa); mkubwa kuliko kitu chochote mtu yeyote angeweza kukifikiria. Allah milele ni mkubwa kwa sababu yeye ana nguvu kuliko wote. Kutokana na mtazamo huu kwamba Allah ni zaidi, ni Mungu mwenye nguvu unakuja mtazamo kwamba Allah ni zaidi ya ufahamu wa wanadamu, zaidi ya mahali panapoweza kufikiwa na wanadamu, na zaidi ya mwingiliano wa kila siku wa wanadamu.
Allah = mungu mwezi
BIBLIA INASEMA
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee ili kila amwaminie asipotee bali awe na uzima wa milele.” Yohana. 3:16
UPENDO WA HALISI NI NINI?
Yohana, anayejulikana kama “mtume wa upendo” anaongeza Mungu ni upendo. Yeyote aishiye katika pendo anaishi ndani ya Mungu; na Mungu ndani yake. 1Yohana 4:16.
TUNATOA AINA nyingi za vijitabu, vipeperushi, kanda za video na kaseti zinazofunua na kuthibitisha kuwa mafundisho yale makuu ya Kiislam ni ya uwongo. Masomo kama Jihad, Utumwa, Wanawake katika Uislam, Majaliwa ya Muasi. Mwanzo wa Koran, na Maisha binafsi ya Muhammad, mbali ya shuhuda za mageuzi; yana uhakika wa kujibu maswali unayoweza ukawa nayo juu ya Uislam. Saidia kueneza ukweli kuhusu mafundisho ya uongo ya mapepo yaitwayo Uislam. Vitu vyote vinatolewa bure ukiagaiza.
OMBA
Mpendwa Mungu, najua kwamba dhambi zangu zimenitenga nawe,nataka kukiri dhambi zangu. NASIKITIKA. Najua kwamba unanipenda na kwamba ulimtuma Yesu msalabani, kwa ajili yangu, akachukua adhabu ya dhambi zangu. ASANTE. Sasa hivi nakuomba uje ndani yangu na uyatawale maisha yangu. Ninakupa nafsi yangu. Tafadhali anza kuyaongoza maisha yangu. NAKUHITAJI. Asante kwa kunipa uzima wa milele. Katika jina la Yesu naomba, Amen.
Kwa maelezo zaidi kuhusu ACMTC TANZANIA, au jinsi utakavyoweza kujihusisha, wasiliana na Meja Frank & Elina Materu: S.L.P. 7579 Dar es Salaam, Tanzania. Barua pepe: materufrank@yahoo.com
|
No comments:
Post a Comment