Friday, June 19, 2015

UTATA NA SHAKA KATIKA QURAN WA MUHAMMAD KWENDA MSIKITI WA AL-AQSA

Ndugu zanguni,
Leo ningependa tujifunze kidogo kuhusu utata na uongo ulio wekwa kwenye Qurana kuhusu safari ya Mtume wa Allah aitwaye Muhammad ya usikU kwenda Msikiti wa Al Aqsa ambao upo Jerusalem. Hebu kwanza angalia aya wanayo itumia kusaidia madai yao.
Sura Al israai 1. SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.
Historia inatuambia kuwa Jeshi la Waislam liliuchukua Mji wa Jerusalem panapo Mwaka 637 AD na Msikiti wa Al Aqsa ulimalizika kujengwa mwaka 705 AD.
Tatizo linaanza namna hii: Inafahamika kuwa Muhammad Mtume wa Allah alifariki Mwaka 632 AD tarehe ya 8 na Mwezi wa 6, ambao ni Miaka 5 kabla ya Jeshi la Waislam kufika Jerusalem na ni miaka 73 kabla huo Msikiti wa Al Aqsa kujengwa. Jamani huu ni uongo wa wazi kabisa unao semwa kila siku na hawa Waislam kwa kupitia Allah wao ambaye sasa tunaweza sema kuwa ndie baba wa uongo.
Ndugu wasomaji, hivi ni kwanini Allah anashindwa kuziweka hesabu zake vyema mpaka asema uongo wa namna hii?
Kama kweli Allah alimtuma Muhammad kwenda Jerusalem katika Msikiti wa Al Aqsa, kwanini alishindwa kuutengeneza huo Msikiti kabla ya kufariki kwa Muhammad?
Hakika kuna sababu nyingi sana ambazo zilimfanya Allah akiri katika Quran kuwa, Wakristo na Wayahudi ni watu wa Kita’ab, akimaanisha kuwa ni watu wenye elimu kuliko Waislam na Waarabu.
Surat Yunus 94. Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wenye shaka.
MASWALI:
1.    Kwanini Allah alidanganya kuhusu safari ya Mtume Muhammad ya kwenda Al Aqsa?
2.    Kwanini Waislam wanashindwa kufanya hesabu rahisi za tarehe ulio jengwa huo Msikiti wa Al Aqsa?
Hakika Msingi wa Dini ya Uislam ni Allah ambaye amesha pokea sifa ya kuwa ni Baba wa Uongo. Hebu rejea na soma hii aya kutoka Biblia kitabu cha Mungu:
Yohana 8: 44 Ninyi ni watoto wa baba yenu Ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli maana hamna kweli ndani yake. Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo.
Biblia imesha kujibu kuwa baba wa Uongo ni Ibilisi na husema yaliyo yake mwenyewe. Kumbe basi, ndio maana Allah wa Waislam nayeye anasema yaliyo yake.
Nakukaribisha kwa Mungu Mkuu ambaye yeye sio Baba wa Uongo bali ndie Muumba wa kila kitu na alikufa kwa ajili ya dhambi zako.
Mpokee Yesu leo na upate Uzima wa Milele.
Mungu awabariki sana.

Max Shimba Ministries Org.
Max Shimba Ministries org ©2015. ALL RIGHTS RESERVED

Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW