Friday, March 21, 2014

Mtume. Rashid Abubakar alionya kanisa juu ya kukimbilia Nigeria.


Mtume. Peter Rashid Abubakar
Mtume Peter Rashid Abubakar ambaye ndiye mwanzilishi wa huduma ya Glory to God Miracle Center(House of Prayer For All Nations) Tanzania jijini Dar es Salaam amelionya kanisa  akiliambia umetokea ujinga wa kutumiana masage zikisema meseji hii tumia watu 12 au 20 imetoka kwa Tb. Joshua!!!??? 
Alihoji Tb. Joshua yeye ni nani!!? Mbona ni mtumishi wa MUNGU kama mimi tu! 
Akiongea huku akinukuliwa na Maisha ya ushindi blog alisema
 watu wengi kanisani hapa kwangu wanafunguliwa wasio na watoto; Kazi; etc wanapata kwa jina la YESU. 
Alisema nimeombea wangapi waliokwenda kwake Tb. Joshua ambao hawakuponywa au kufunguliwa na niliwaombea na YESU KRISTO akawaponya. 
 Aliuliza je YESU wa Tb. Joshua na mimi ni tofauti? YESU KRISTO mwenyewe kwa kauli yake anasema  YEYE HABADILIKI. YEYENI  JANA NA LEO NA HATA MILELE. 
Alisema huo ni USHAMBA WA KIROHO AU NI UKIRO WA KIROHO(UKIRO=U-Ukosefu wa K-Kinga wa R- Roho) ni sawa na UKIMWI= Ukosefu wa kinga za mwilini). 
Alisema Yeremia 17:5-6. Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu na kumfanya kinga moyoni mwake
Kwa imani yenu hiyo alisema Mbona wenye karama ya uponyaji na matendo ya miujiza mbona nipo mimi hapa? Na wengine wengi tu Dar es salaam au Tanzania.
 Hizo pesa nyingi za nauli mnazopoteza kwenda Nigeria na kurudi huko si mniletee mimi nizijengee kanisa? Au pelekeeni wazazi wenu wanaokufa na njaa zikawasaidie? 
Wengine hata uwanja wa kujenga hamna? Alimalizia kwa kusema POLENI WATANZANIA WENYE IMANI HIYO KATIKA JINA LA YESUUU!!! 

KAMA NI TB. JOSHUA NIPO HAPA MBEZI MWISHO JIJINI DAR ES SALAAM NAULI MIA TANO KWENDA NA KURUDI ELFUUU. EMEEEEEEEE!!! Kanisa lote liliitikia Emeeeeeeee!

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW