Jamani huu ni Msiba
katika taifa la Islam kwa kushindwa kusoma aya hii ambayo ipo wazi (Quran
40:60).
Katika mada hii,
nitawawekea aya kutoka Koran na simulizi za Muhammad ambazo zinatushuhudia
kuwa, Waislam wote wataingia Jehanamu.
Hebu tumsome kwanza Allah katika aya
aliyo iteremsha kwa Mtume wake Muhammad (Pbuh).
Quran 40: 60. Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike.
Mungu wa Waislam ajulikanaye kwa
Jina la Allah amesema kiuwazi kabisa kuwa “wale wote ambao wanajivunia Uislam
na kumuabudu Allah wataingia Motoni”
Ndugu zanguni, huu ni Msiba, tena msiba mkubwa sana
katika dini na taifa la Kiislam. Allah amesha toa hukumu kwa wamfuatao na
inafahamika fika kuwa, Wale wote waingiao Jehannam, hao walikuwa hawafanyi
Mapenzi ya Mungu wa Biblia. Allah anasema kuwa, ukifanya
mapenzi yake, basi wewe utaingia Jehannam. Huu ushaidi ndio tulio usoma katika
Quran 40:60.
Sasa tuwasikilize
na maswahiba wa Mtume Muhammad.
Simulizi:
Pia imesimuliwa
na Ibn Jarir, iliyosimuliwa na Abu Kurayb, imesimuliwa na Ibn Yaman,
imesimuliwa na Ibn Malik Maghul, imesimuliwa na Ibn Ishaq ambaye alisema,
"Kila mara Abu Maysarah anapo kwenda kulala na akiwa kitandani kwake yeye
husema, 'Mimi nasikia Uchungu kuzaliwa na Mama yangu. 'na kisha anaanza kulia
kwa Machozi. Alipoulizwa kwa nini alikuwa akilia, alijibu ayafuatayo,'
Tuliambiwa kwamba SISI WAISLAMU tutaingia Jehannamu, LAKINI HATUKUAMBIWA kwamba
TUTATOLEWA HUKO JEHANNAMU NA HATUKUAMBIWA NI KIVIPI TUTATOKA HUKO'"
Mfuasi huyu wa
Muhammad anaoneka kupatwa na mshtuko mkubwa, pale alipo ambiwa kuwa, Waislam
wote wataingia Jehannam. Mshtuko huu umemfanya ailaani siku ambayo alizaliwa.
Kitu cha kujiuliza, kwanini Allah ambaye ni mungu wa Waislam anatoa ahadi ya Jehannam
na si Akhera kama wafundishavyo Waislam?
Ndugu zanguni, ningependa mfahamu kuwa, utakapo ingia Jehannam, kutakuwa
hakuna tena njia nyingine ya kutoka huko. Pale Jehannam ndio mwisho wa maisha
ya walio tenda dhanb. Allah anasema kuwa, ukifanya mapenzi yake, basi wewe utaingia Jehannam. Je,
kufanya mapenzi ya Allah ni sawa na kutenda dhanb? Je, Uislam ni dini ya haki,
kama wanavyo sema wafundishaji wa dini hiyo? Jiulize tena, kwanini Allah anatoa
ahadi ya Jehannam kwa wafuatayo mafundisho yake?
Lakini
Yesu anasema haya:
Yohana 14: 6 Yesu
akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa
njia ya mimi.
Ndugu
zanguni, mwamini Yesu ili uwe na uzima wa milele. Yesu anakupenda. Yesu Ndie
Njia Pekee. Yesu Ndie Uzima. Dini haita kupeleka kwa Baba aliye Mbingu, lakini
Yesu anasema Yeye NDIE NJIA.
Mungu
awabariki sana,
Katika
Huduma Yake,
Max
Shimba
For Max
Shimba Ministries
Copyright © Max Shimba Ministries 2013
No comments:
Post a Comment