Je? Mungu anasema nini kuhusu wao wanao
tafsiri nyota kuweza kujua jinsi maisha yao yatakavyokuwa? Imo katika Biblia,
Isaya 47:13-15 "Umechoka kwa wingi wa mashauri yako basi nawasimame hao
wajuao falaki, wazitazamao nyota watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo,
wakakuokoe na mambo yatakayokupata. Tazama watakuwa kama mabua makavu; moto
utawateketeza hawatajiokoa na nguvu za mwali wa moto; hautakuwa kaa la kukota
moto, wala moto wa kukaa karibu nao ndivyo itakavyokuwa mambo hayo
uliyojitaabisha nayo; wale walio fanya biashara nawe tangu ujana wako
watatanga-tanga mbali nawe, kila mtu akienda zake; hapatakuwa na mtu
wakukuokoa."
Unajimu ni imani ambayo yafundisha kuwa uwambatano wa mwezi, nyota na jua
waweza kuleta tukio katika maisha ya mtu. Katika lugha ya kiebrania neno
unajimu ni kutabiri mbingu, kuweza kutoa siri, kutabiri jambo litakalotokea.
Imo katika Biblia, Walawi 19:26 "...... Msifanye kuloga, wala kutumia
utambuzi."
Kabla ya wana waisiraeli kuingia katika nchi ya ahadi, walionywa kutofanya unajimu,
imo katika Biblia, Torati 18:9, 12, 14 "Utakapokwisha ingia katika nchi
akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa
yale 12- kwamaana yule atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu
ya hayo Bwana Mungu wako anawafukuza mbele yako 14 maana mataifa haya
utakaowamiliki huwasikiliza wanao shika nyakati mbaya na kutazama bao; bali
wewe Bwana, Mungu wako, hukupa ruhusa kutenda hayo."
1Samueli 15:23 "Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, na ukaidi ni kama ukafiri
na vinyongo; kwa kuwa umelikataa neno la Bwana yeye naye amekukataa usiwe
mfalme
Wakati mfalme Nebukadreza alipo ota ndoto aliwaita wagana, wachawi, wasihiri na
wakaldayo waweze kutafsiri ile ndoto. Imeandikwa Danieli 2:10 "Wakaldayo
wakajibu mbele ya mfalme, wakasema hapana mtu duniani awezaye kulionyesha neno
hili la mfalme kwa maana hapana mfalme, wala bwana wala liwali aliyetaka neno
hili kwa mganga wala kwa mchawi wala kwa mkaldayo."
Imo katika Biblia, Danieli 2:27-28. "Danieli akajibu mbele ya mfalme
akasema ili siri aliyoiuliza mfalme; wenye hekima hawawezi kumfunulia mfalme;
wala wachawi, wala waganga, wala wanajimu. Lakini yuko Mungu Mbinguni afunuaye
siri naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayo kuwa siku za
mwisho."
In His Service
Max Shimba
No comments:
Post a Comment