Friday, January 21, 2022

MAASI YA BAADHI YA MASWAHABA WA MTUME MUHAMMAD (saww) NA KURUDI KWENYE UKAFIRI!

 



MAASI YA BAADHI YA MASWAHABA WA MTUME MUHAMMAD (saww) NA KURUDI KWENYE UKAFIRI!

Waislamu wengi wa Madhehebu nyingi ambazo siyo wa Shia Ithna'ashry Wanakataa kuwa Wapo Maswahaba wa Mtume (saww) ambao walitenda mabaya mengi kiasi kuwa matendo yao yaliwarudisha kwenye Ukafiri!

Waislamu hao, wamekuwa hawajui ukweli wa mambo waliyoyafanya hao maswahaba ambao wamefikia kutukuzwa sana kuwashinda hata Mtume Muhammad (saww) Mwenyewe na Watu wa Nyumba Yake Waliotakaswa na kutoharishwa ama kwa kutosoma vitabu au kufichwa na kupotoshwa na mashekhe wao!

Kufuatana na rejea hii ya kutoka kwenye Sahih Bukhari ambacho ndicho kinanadiwa kuwa ni Sahih kabisa baada ya Qur'aan Tukufu, Abu Huraira amesimulia hadith inayosema kuwa: Watakuja maswahaba wa Mtume (saww) kwenye Haudh ya Kawthar ili wapewe yale maji Matamu na ya Kuburudisha ya kule Peponi kupitia mikono ya Mtume (saww) Mwenyewe, Lakini Malaika watawafukuza hao maswahaba mahala hapo, kisha Mtume (saww) Atasema: Musiwafukuze hao walikuwa maswahaba wangu!
Itatokea Sauti ya Mwenyezi Mungu Akisema: Ewe Muhammad! Hujui hawa walifanya nini baada ya kufariki kwako, Walirudi kwenye Ukaffir!

Haya enyi munaowatetea Maswahaba kuwa wote walikuwa wabora na watukufu, Hiyo hadith huyo Abu Huraira alidanganya au alitunga hadith ya kuwadhalilisha hao maswahaba?

Sisi Mashia tunapowaambieni kuwa Abubakar, Umar, Uthman, Muawiyyah, Khaleed bin Walid na wengine wengi walifanya Maovu na Udhalim mkubwa munapinga na munafikia kutukufurisha na kusema sisi tunawatukana maswahaba.

Je huyo Abu Huraira Ametukana?

Kama ametukana, mbona basi hamusemi kuwa Abu Huraira Alikuwa Kaffir na hamuzichomi hivyo vitabu vyenu?


No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW