WAISLAM MTUWIE RADHI KWA MWILI KUWEKWA KWENYE SANDUKU KAMA WAKRISTO
TAARIFA ZA SAFARI YA MWILI WA MAREHEMU AFIDA SALIM ALI
Assalam Aleykum ndugu zetu wote popote pale mlipo.
Kwanza kabisa tunatoa shukran za dhati kabisa kwa watu wote nchini Luxembourg , Germany Uk Belgium na nyumbani Tanzania kwa ushirikiano wenu mkubwa mpaka kufanikisha safari ya mwenzetu AFIDA aliyefariki nchini Luxembourg kuelekea nyumbani kisiwani Zanzibar.
Pili nawapa taarifa rasmi leo tarehe 23.11.2021 majira ya 19hr usiku mwili wa marehemu AFIDA SALIM ALI utaruka kutoka Zaventem International Airport nchini Ubelgiji kuelekea nyumbani Tanzania kwa shirika la ndege la Turkish Airlines na utawasili AMANI ABEID KARUME INTERNATIONAL AIRPORT saa nane usiku siku ya kesho.
Kesho asubuhi tarehe 24.11.2021 asubuhi mume wa marehemu ataondoka saa tano asubuhi kuelekea nyumbani Zanzibar.
Ifahamike vizuri kwamba mwili wa marehemu AFIDA utakapotua Zanzibar na mume wa marehemu ndio atakaotoka nao nje ya Airport.
Tunawaomba ndugu zetu wa nyumbani Zanzibar muupokee mwili wa marehemu AFIDA usiku huo wa saa nane na nusu.
Shukrani za dhati kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Diaspora Tanzania nchini Ubelgiji, Watanzania nchini Luxembourg, Ubelgiji,Watanzania nchi Uingereza, Watanzania nchini Ujerumani na watanzani wote kwa ujumla walioshiriki kwa namna moja au nyingine kufanikisha zoezi zima,Mungu atawalipa kwa wema wenu.
Mwisho,
Shukrani kwa mashekh wetu wote na mashirika ya dini yaliofanikisha shughuli nzima ya usafirishaji wa mwenzetu AFIDA.
Tutatoa taarifa rasmi ya kikao siku zijazo kwa kuwapa ripoti na taratibu zilivyokwenda.
Asanteni sana na Mungu awabariki nyote.
Mwenyekiti,
M.One.
No comments:
Post a Comment