Saturday, March 2, 2019

MWANADAMU ALITOKEA WAPI?

Image may contain: 2 people, text




Asili ya Mwanadamu

Wazo la kumuumba mwanadamu lilitoka kwa Mungu. (Mwanzo 1:26.) Na wakati anamuumba, alitekeleza wazo lake kwa kuumba watu wawili, mtu mume na mtu mke, akawaita jina lao Adamu. (Mwanzo 1:27; 5:1, 2.)

Mwanadamu aliumbwa kwa udongo na pumzi (Mwanzo 2:7) Vitu viwili vilitengeneza mtu, udongo na pumzi ya uhai. Kilichopatikana kutokana na mwunganiko wa udongo na pumzi kimeitwa nafsi hai, yaani kama tungekuwa tunafanya hesabu, udongo + pumzi ya uhai = nafsi hai. Nafsi hai haiwezi kuwa nafsi hai ikiwa kimojawapo kati ya udongo au pumzi ya uhai kitaondolewa. Kwa hiyo, nafsi hai ni kitu kisichoweza kugawanyika ili kila kipande kibaki na maisha yake )yanayojitegemea peke yake. (cf. Mhu. 12:7)

Katika siku ya mwisho ya uumbaji, Mungu akasema, “Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu” (Mwanzo 1:26). Na hivyo Akamaliza kazi yake kwa “uguzo wake mwenyewe.” Mungu alimuumba mwanadamu kutoka kwa udongo na akampa uhai kwa kumwekea pumzi yake (Mwanzo 2:27). Vilevile, mwanadamu ni kiumbe tofauti katika viumbe vyote alivyoviumba Mungu, vyote vikiwa na mwili wa nyama na wa ndani nafsi/roho.

Aliumbwa kwa sura ya Mungu (Mwanzo.1:26) Viumbe vingine vilikuwa kwa jinsi zake (Mwanzo.1:2, 24, 25). Lakini mwanadamu alikuwa kwa mfano wa Mungu. Na Luka anasema, Adamu ni mwana wa Mungu (Luk.3:38)

Mwanadamu ana hadhi ya juu. Aliumbwa akiwa na hadhi ndogo kuliko malaika lakini alipewa kusimamia uumbaji wa Mungu. (Mwanzo. 1:28; Zaburi. 8:4-9)

Kuwa na “sura” ya Mungu yamaanisha, kwa ufupi, kwamba tuliumbwa tumfanane Mungu. Adamu hakumfanana Mungu kwa kuwa na mwili wa nyama na damu. Bibilia inasema kwamba “Mungu ni roho” (Yohana 4:24) na kwa hivyo anaishi bila kuwa na mwili. Ingawaje, mwili wa Adamu ulidhihirisha maisha ya Mungu vile yalikuwa makamilifu kwa afya na haukutishika na kifo.

Sura ya Mungu yamaanisha mwili wa ndani wa mwanadamu. Unatofautisha mwanadamu kutoka ulimwengu wa wanyama, na kumweka mwanadamu kufaa mamlaka Mungu alimuumbia kuwa nayo katika nchi (Mwanzo 1:28), na kumwezesha kuwa na ushirika na muumba. Mwanadamu anamfanana Mungu, kimawazo, tabia na maisha ya furaha.

Kimawazo, mwanadamu aliumbwa kama kiumbe kiwezacho, kuwa na uwezo wa kuamua. Kwa njia nyingine, mwanadamu anaweza kuwaza na kuchagua. Hii ni taswira ya hekima na uhuru wa Mungu. Wakati wowote mtu anaweza vumbua/gundua chombo (mashine), aandike kitabu, airembeshe picha ya nchi aliyoichora, na afurahie kucheza ngoma, afanye hesabu, ama avipatie viumbe majina, na hivyo anatangaza kuwa tumeumbwa kwa mfano wa Mungu.

Kitabia, mwanadamu aliumbwa kwa utakatifu na ukamilifu ukiambatana na, taswira ya utakatifu wa Mungu. Mungu akaona kila kitu alichokifanya (mwanadamu akiwemo) na akakiita “chema sana” (Mwanzo 1:31). Fikra zetu au “dira ya tabia” ni dalili ya ile hali ya asili. Popote mtu anaandika sheria, na kugeuka kutoka dhambi, kuisifu tabia njema, au kujishuku na hatia, hii inadhibitisha dhana kwamba tumeumbwa kwa mfano wa Mungu.

Udongo: Tafsiri ya udongo haina shida. Ni sehemu ya ardhi.

Pumzi ya Uhai. (Mwa.2:7). Wakati Mungu alipobadili maada ya dunia kuwa kiumbe hai, alipulizia pumzi ya uhai. Alipulizia pumzi ya uhai, pumzi za Mwenyezi (Ayu.33:4), cheche ya uhai.

Mwanadamu - Nafsi Hai . Hesabu ya Maandiko iko wazi. Udongo jumlisha pumzi ya Mungu ni sawa na nafsi hai. Siyo wanadamu pekee waliopewa pumzi ya uhai. Nafsi hai hujumuisha pia wanyama wa baharini, vitambaavyo, na wanyama (Mwa.1:20, 24; 2:19). Siyo kwamba mwanadamu akapokea roho, bali akawa nafsi (roho) hai.
Umoja usiogawanyika- Mwanadamu ni kiumbe kimoja kisichogawanyika. Je, kuna uhusiano gani baina ya nafsi na roho?

1. Maana ya Biblia ya Nafsi.

Katika Agano la Kale, neno la kiebrania lililotafsiriwa nafsi ni nephesh. Ndivyo Mw. 2:7 inavyosema mtu akawa nafsi hai. Kwa jinsi hiyo hiyo kila mtoto mchanga anapozaliwa, nafsi hai huongezeka. Kwa hiyo, nephesh siyo sehemu ya mwanadamu hai bali ni mwanadamu mzima. Anavyokufa binadamu vivyo hivyo na mnyama (Mwanzo.7:20–23) Wakati wa Nuhu vilikufa viumbe vyote isipokuwa Nuhu na waliobaki ndani ya safina. Kwa kuwa roho (nephesh)
ndiyo nafsi hai, roho nayo inakufa (Ezekiel.18: 4).

Katika Agano Jipya lililoandikwa Kigiriki, neno litumikalo kwa nafsi ni psuche. Hutumika kwa wanadamu na wanyama (Ufunuo 16:3) “Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu, kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.”
Kwingine roho ina maana ya uhai (Mat. 2:20, 6:25, 16:25). Kwingine roho inamaanisha watu (Mdo. 7:14, 27:37, Rum. 13:1 1Pet.3:20) Hutumika kwa nafsi (Mt. 12:17. 2 Kor.12:15) Na kwingine humaanisha hisia (Mk.14:34 Luk. 2:35) au akili (nia) (Mdo 14:2, Filipi 1:27) au moyo
(Ef. 6:6)

Katika yote haya, lengo ni kuhitimisha kwamba psuche (roho) haina hali ya kutokufa bali ina hali ya kufa. (Uf. 16:3)

Katika maisha ya ushirika, mwanadamu aliumbwa ili awe na ushirika. Hii inadhihirisha hali ya utatu wa Mungu na upendo wake. Katika Edeni, uhusiano wa mwanadamu ulikuwa na Mungu (Mwanzo 3:8 yamaanisha ushirika na Mungu), na Mungu akamuumba mwanamke wa kwanza kwa sababu “Si vyema huyo mtu awe pekee” (Mwanzo 2:18). Kila wakati mtu anapooa, anatengeza urafiki, kumpusu mototo, au kushiriki kanisa, ni kuonyesha kuwa tumeumbwa kwa mfano wa Mungu.

2.
Maana ya Pumzi ya Uhai

Neno ruach lililotafsiriwa pumzi, hupatikana kwenye Agano la Kale mara 377. Kufuatana na Ayubu 33:4, ni pumzi ya Mungu inayotia uhai, Inaitwa upepo, roho au pumzi (Mw. 8:1) Na kila chenye uhai, Hutumika kuonyesha hali ya kuwa mzima wenye nguvu (Amu. 15:19). Hutumika
wakati mwingine kuonyesha ujasiri (Yosh. 2:11) hasira au kukosa uvumilivu (Amuz. 8:3).

Pia huonyesha hadhi (Isa. 54:6), tabia adilifu (Ez. 11:19) “Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao; nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao, name nitawapa moyo wa nyama.”

Kwa maana ya upepo au pumzi, hakuna tofauti kati ya binadamu na mnyama kwenye kifo (Mh. 3:19 -21). Roho humtoka mwanadamu akifa Zab. 146:4 na humrudia Mungu Mh. 12:7 (Angalia pia Ay. 34:14). Ruach hutumika mara nyingi kumaanisha Roho ya Mungu (Isa. 63:10). Hakuna kwenye Agano la Kale ambako roho (ruach) imepata kuishi kwa kujitegemea nje ya mwili.

Katika Agano jipya, neno lililo na maana ya ruach (Kiebrania) ya agano la kale ni pneuma

(Kigiriki) – kupuliza, kupumua. Kama ilivyo kwa ruach, hakuna chochote ndani ya mwanadamu chenye kuweza kuishi nje ya mwili.

Roho/Moyo (pneuma) imetumika pia kuonyesha mtizamo – (Rum. 8:15, 1 Kor 4:21, 2 Rum. 1:7, 1Yoh.4:6) na hali mbali mbali za kibinadamu kama katika (Gal. 6:1, na Rum. 12:11).

Pneuma hutoka mtu anapokufa (Luk. 23:46, Mdo. 7:59). Kama ruach, pneuma pia inatumika tunaposema Roho ya Mungu (1Kor.2:11, 14, Ef.4:30, Ebr.2:4 1Pet.1:12, 2Pet. 1:21).

3.
Muungano wa mwili, moyo na roho
a) Muungano wa viwili. Biblia haisemi uhusiano uliopo baina ya mwili, moyo na roho.

Wakati mwingine nafsi na roho hutumika kwa kubadilishana “moyo wangu wamwadhimisha Bwana, roho yangu imemfurahia” (Luk. 1: 46, 47). Mara moja, Yesu
amemsema mwanadamu kuwa ni mwili na roho Mt.10:28). Mahali pengine, Paulo anamwona binadamu kuwa ni mwili na roho (1Kor.7:34)

b) Muungano wa vitatu. Paulo ambaye alipata umzungumza mwanadamu kuwa wa muungano wa viwili, amesema kwenye 1Thes.5:23 kuwa mwanadamu ana nafsi, roho na mwili. Hapa, roho yaweza kuwa kanuni ya juu ya akili inayowasiliana na Mungu (Rum. 8:16). Kufanywa upya nia, hutubadilisha (Rum.12:1, 2)

c) Muungano usiogawanyika. Mwili, moyo na roho hutenda kazi kwa kushirikiana ikionesha hali ya mtu kiroho, kiakili na kimwili.

Sehemu ya kuumbwa kwa mfano wa Mungu ni kwamba Adamu alikuwa na uwezo wa kufanya uamuzi. Ingawa alipewa hali takatifu, Adamu akafanya uamuzi wa dhambi na kuasi kinyume na muumba wake. Kwa kufanya hivyo, Adamu akaiaribu sura ya Mungu ndani yake na akaupitisha huo ubaya kwa kizazi chake chote (Warumi 5:12). Hata hii leo bado twaibeba hiyo sura ya Mungu (Yakobo 3:9), lakini bado twavibeba vidonda vya dhambi kimawazo, kitabia, kimaisha ya kawaida na hata kimwili twaonyesha madhara ya dhambi.

Habari njema ni kwamba Mungu anamwokoa mtu binafsi, anaanza kurejesha sura ya kiasili ya Mungu, kuumbwa “mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli” (Waefeso 4:24). Huo wokovu upo tu kwa neema ya Mungu kupitia kwa imani katika Kristo Yesu aliyetuokoa kutoka dhambi ambayo ilitutenganisha na Mungu (Waefeso 2:8-9). Kupitia Kristo tumefanywa viumbe vipya kwa mfano wa Mungu (2Wakorintho 5:17).

Shalom,

Max Shimba mtumwa wa Yesu kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW