Monday, March 18, 2019

KWARESMA NA JUMATANO YA MAJIVU NI NINI NA ILIANZIA WAPI?


No photo description available.

Kwenye somo letu la leo, tutajifunza maana ya Kwaresma na Jumatano ya Majivu kama inavyo fuatwa na Kanisa la Katoliki. 

Hii mada ninaifundisha kwa sababu ya swali ninilo ulizwa na sina budi kulijibu kiuwazi. Sio kusudio la hii mada kukosoa wala kukubali, bali ni kueleza na kujifunza maana yake. 

KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku arobaini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya kupakwa majivu kwenye paji la uso (siku ya Jumatano ya Majivu) ikiwa ishara ya kuanza toba. Kujikubali kwamba tu wakosefu na pia kujutia makosa yetu tunayotenda kinyume na mapenzi ya Mungu. 

Jina la Jumatano ya Majivu, lilianza kutumika rasmi mwaka 1099 na Papa Urbani II: mwanzoni iliitwa “Mwanzo wa Mfungo”. Majivu yatumikayo hutokana na matawi yaliyobarikiwa Jumapili ya Matawi ya mwaka uliopita. Kwaresima ni kipindi cha siku arobaini za kufunga, kusali, kutafakari Neno la Mungu na kufanya matendo ya huruma. Ni wakati wa kumwilisha utamaduni wa Injili ya upendo!

Kipindi cha Kwaresma kinawaandaa waumini Wakatoliki kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka yaani ufufuko wa Yesu Kristo. Ufufuko ndio msingi mama wa imani ya Wakatoliki; “…na kama Kristo hakufufuka, basi mahubiri yetu hayana maana na imani yetu haina maana…” (1 Wakaritho15:14). 

Jina hili yaani Jumatano ya Majivu, lilianza kutumika rasmi mwaka 1099 na Papa Urbano II: mwanzoni iliitwa “Mwanzo wa Mfungo”. Majivu yatumikayo hutokana na matawi yaliyobarikiwa Jumapili ya Matawi ya mwaka uliopita. Kwaresima ni kipindi cha siku arobaini za kufunga, kusali, kutafakari Neno la Mungu na kufanya matendo ya huruma. Ni kipindi kinachotualika kumwilisha ndani mwetu utamaduni wa upendo, kwa kufunga na kuwasaidia maskini zaidi. Kipindi hiki cha Kwaresima ni safari ambayo kilele chake ni adhimisho la fumbo la ukombozi wetu yaani mateso, kifo na ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Kipindi cha Kwaresma kinadai mambo makuu matatu: Kwanza, kufunga yaani kubadili aina na kiasi cha chakula ambacho mtu huwa anakula kila siku, kiasi kipungue na aina pia ya chakula. Kama wewe umezoea kula milo mizito yenye kila aina ya mahanjumati basi Kwaresma badilisha na ule kawaida kabisa. 

Kufunga hakuishii tu katika kufunga chakula bali kuzuia mianya yote inayomfanya mtu atende dhambi. Hili ndilo jambo la kuzingatia. Kama tunavyosoma katika Kituo cha 14 cha njia ya msalaba kinachosema kwamba; “Pamoja nawe kaburini, zika dhambi na ubaya wa moyo, Yesu tuwe Wakristo kweli. Twakupa, twakupa sasa mapendo.” 

Ni kipindi cha kujinyima na kujikatalia: Pili, kufanya matendo ya huruma au kutoa sadaka, yaani kile ambacho mtu anajinyima basi akipeleke kwa wenye shida. 

Tatu, kuongeza muda wa kusali hasa kwa kusoma Neno la Mungu, yote haya matatu yanaelezwa vizuri sana katika kitabu cha Nabii Yoel 2:12-18. 

Kwa Wakatoliki, tendo hili la Kwaresma huwa linajionyesha kwa kufuata njia ya msalaba ambayo huwa inafanyika siku ya Ijumaa na sehemu nyingine siku ya Jumanne. Bila ya kujali ni siku ngapi za njia ya msalaba mtu anahudhuria. Kinachozingatiwa zaidi ni kuona kuwa vile vituo vyote kumi na nne vya njia ya msalaba vina maana katika maisha ya ufuasi wa Yesu Kristo au tunahudhuria ibada kwa kutekeleza wajibu wa kuonekana kwamba tunapitia vituo vyote kumi na nne kwa masikitiko ya usoni kumbe moyoni ni mkavu kabisa. 

Vituo vya njia ya msalaba havitukumbushi tu machungu na magumu aliyopitia Yesu bali kikubwa zaidi ni sisi waumini tunakumbushwa kujitoa na kuacha mapenzi na makusudi ya mtu yanayomjengea ubinafsi, ili aweze kumfuata yeye aliyejitoa kwa ajili yetu maskini kwa matajiri. Yesu hadai kwamba mwumini lazima apate adha na mateso ya kimwili, lakini anataka kila mfuasi wake awe tayari kutimiza mapenzi ya Mungu ambayo kwayo yanadai zaidi kutimiza na kuishi amri ya mapendo ambayo imeonekana kupitia kwa Yesu Kristo.

Ushiriki wa njia ya msalaba haumfanyi mtu kumtafuta Mungu au kuwa karibu na Mungu tu, bali ushiriki wa ibada ya njia ya msalaba unatufanya na kutulazimu tukuze mapendo kwa ndugu zetu kwa kukwepa na kuogopa kuwafanyia mabaya. Neno haki linakuza na kudumisha upendo, kinyume cha hapo kunakuwa na magomvi, matabaka yasiyo ya lazima, uonevu, unyanyasaji, udhalilishwaji na ubadhirifu wa kila namna na ndipo ufisadi unajikita kwa sababu haki imepindishwa na kutekwa na wenye nguvu. 

Haki katika safu hii naiweka katika maana mbili; kwa upande mmoja haki ina maana ya usawa, uadilifu au uwajibikaji kuhusu sheria ya mambo ya kawaida ya jumuiya ya mwanadamu. Hii tunaweza inaitwa ‘justice’. Sheria ya kutambua haki hii imeandikwa kwenye moyo wa kila mwanadamu na inaitwa dhamira; “…Mwenendo wao unaonyesha kwamba matakwa ya sheria yameandikwa mioyoni mwao. 

Katika siku za Agano la Kale na pia katika Agano Jipya, kama tulivyosikia katika Maandiko Matakatifu ya kuwa ikiwa mtu alikuwa ametenda dhambi, alivaa nguo za magunia na kujipaka majivu katika mwili wake (Rej. Yer 6:26). Tendo hili tunalofanya leo la kupakwa majivu, linatokana na desturi hiyo ya kiroho ya kufanya toba. Katika ulimwengu wa wayahudi majivu yalikuwa ni alama ya huzuni, masumbuko, uchungu au uduni (Rej. Ayubu 2:8, 30:19; Zab 102:10). Baadaye utamaduni huu wa kupakana majivu ulitumiwa na wakristo wa kwanza kama alama ya toba.

Mwaka 600 hivi, Papa Gregory Mkuu aliifanya siku ya Jumatano ya Majivu kuwa siku ya kwanza ya Kwaresima na akaongeza urefu wa kipindi hiki cha toba hadi siku arobaini. Miaka ya 800 hivi, baadhi ya makanisa yaliadhimisha ibada ya Jumatano ya majivu kwaajili ya wadhambi waliokubuhu katika dhambi na waliojulikana. Sasa pale walipoamua kufanya toba ndio walipakwa majivu. Hivi wakati huu si wote walipakwa majivu ila tu wale waliokuwa wadhambi waliojulikana wazi, kama vile Malaya, wauaji, waasi n.k. Kuanzia karne ya 11, Kanisa lilipanua ibada hii na kuwahusisha waamini wake wote na si wadhambi waliokubuhu tu.

Tendo hili liliambatana na matendo mbalimbali ya kufunga, kusali, kutoa sadaka, kuonesha mapendo kwa wengine na matendo mengineyo ya huruma. Leo hii mwenyezi Mungu kwa kinywa cha Nabii Yoeli, anatuita tumrudie Yeye kwa mioyo yetu yote, kwa kufunga na kwa kulia na kwa kuomboleza. Tunaambiwa tuirarue mioyo yetu, na siyo mavazi yetu. Katika siku za Agano la Kale, watu walikuwa na desturi ya kurarua mavazi yao kama ishara ya kufanya toba. Hata hivyo, walikuwepo wengine waliokuwa wakiyararua mavazi yao kama ishara ya nje tu, na kumbe ndani ya mioyo yao hawakuwa na nia ya kufanya toba ya kweli. Mioyo yao ya ‘jiwe’ haikuweza kubadilika! Watu hawa hawakuwa wameyaacha mambo ya kiulimwengu na kuanza kuyaishi maisha mapya, maisha ya kumcha Mungu.

Nabii Yoeli, anatutaka sisi waamini kumrudia Mungu. Katika hili Nabii Yoeli haiti mtu mmoja mmoja, bali anatoa wito kwa watu wote, akisema, “Pigeni tarumbeta katika Sayuni, takaseni saumu, kusanyikeni kusanyiko kuu; kusanyikeni watu, litakaseni kusanyiko, kusanyikeni wazee kusanyeni watoto na hao wanyonyao maziwa” (Rej. Yoe 2:15). Mtakatifu Paulo, katika Waraka wake wa pili kwa Wakorintho, anatusihi tukubali kupatanishwa na Mungu kwa njia ya Kristo. Mungu Baba alimtuma Mwanawe wa pekee, Yesu Kristo, aje kutukomboa kwa kuteswa na hata kufa msalabani. Mungu asiyejua dhambi alimfanya Yesu Kristo kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye (Rej. 2Kor 5:21).

Yesu Kristo hakujua dhambi, lakini alifanywa kuwa dhambi; vivyo hivyo sisi tusio haki tunafanywa kuwa haki katika Yeye. Sisi wadhambi tulistahili kifo hiki cha aibu nakutisha, kifo cha msalaba lakini Yesu Kristo kwa Upendo aliokuwa nao akakubali kutoa Maisha yake kufa msalabani kwa ajili yetu. Katika Injili Yesu anatuonya kuhusu unafiki wa mafarisayo yaani mtindo wa kufanya matendo mema ili kuonekana machoni pa watu wengine. Yesu anasema ya kuwa Mafarisayo hao wamekwisha kupokea thawabu yao kwa njia ya hao watu wengine wanaowatazama na kuwastaajabia, na pia kuwasifia. Watu wa namna hii, anasema Yesu, hawatapokea tena thawabu mbele ya Mungu Baba aliye Mbinguni. Katika kipindi hiki cha Kwaresima, matendo yetu mema yasiwe yale yanayolenga kujionesha hadharani au kwa watu wengine, bali yawe ni mawasiliano binafsi kati yetu na Mungu yaani kujenga muungano na Mungu wetu Mtakatifu sana kwa sala, sadaka na kufunga.

Dhamira zao zinashuhudia pia jambo hili, maana fikra zao mara nyingine huwashitaki, na mara nyingine huwatetea…” (Warumi 2:15). Sheria kama hizi hazijaandikwa kwenye vitabu bali ziko katika moyo wa mtu, mbali na kuwa haiko katika vitabu lakini bado inambana mwanadamu ajue haki ni nini na apange kanuni ili kuendesha haki katika jamii. Utambuzi wa haki hii haikuandikwa lakini bado unamwezesha mwanadamu afahamu yaliyo sawa au yanakwenda kinyume na Mungu. 

Kipindi hiki cha Kwaresma kinatubana zaidi kuhakikisha tunadumisha upendo kwa kutenda haki katika taasisi zote za kiserikali na dini, kwani sote twahesabika kuwa tu wadhambi twaweza tukawahadaa wanadamu wenzetu lakini Mungu bado anaona mioyo yetu kama Nabii Amosi anavyotuambia; “…maana mimi najua wingi wa makosa yenu na ukubwa wa dhambi zenu; ninyi mwawatesa watu wema, mnapokea rushwa na kuzuia fukara wasipate haki mahakamani.” (Amosi 5: 12). 

Ninawashukuru sana wasomaji kwa ushauri. Nimejisiki niko na watanzania wengi karibu kupitia tafakuri hii. nawapenda sana! Mungu awabariki. 

Shalom,

Max Shimba Ministries Org.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW