Thursday, February 21, 2019

JE, YESU NI MUNGU?

Image may contain: cloud, sky, text, nature and outdoor


Na je, Yesu ndiye Yahova Baba wa Milele? Je, kuna Mungu mwingine zaidi ya huyu Mmoja? Tafadhali Nifafanulie.”
Maswali haya ili kuyajibu kwa kina yanahitaji makala iandikwe ukurasa mzima. Na makala kama hiyo itayaonekana ikiendelezwa kwenye nakala zijazo za Kwanini Yesu ni Mungu http://www.maxshimbaministries.com/…/je-bwana-yesu-anapataj… . Jibu litakalotolewa kwenye kipande hiki cha makala litakuwa ni fupi na litakosa maelezo ya kina kufafanua.
Ndiyo, Yesu ni Mungu, vinginevyo asingeweza kuwa Mwokozi wa wanadamu.1). Iwapo kama Yesu angekuwa ni mwanadamu tu basi kifo chake kingekuwa cha kutoa dhabihu ya kulipa deni la adhabu ya kumfanya mwanadamu mmoja aliyeichukua adhabu ya kosa kwa kuvunja au kuiasi Torati ya kiroho ya Mungu. Kwa kuwa ni Mungu Baba ndiye aliyeumba vitu vyote kupitia kwa Yesu Kristo.
(Waefeso 3:9) na kwa kuwa vimhusivyo mwanadamu vilifanywa na Yesu Kristo (Yohana 1:1-5 pamoja na aya ya 14; na aya ya 10; 1Wakorintho 8:6; Wakolosai 1:12-19). Yeye ndiye Muumbaji na kwa hiyo ni Mungu, na maisha yake aliyoyatoa yana thamani kubwa kuliko kiasi chochote cha mlinganisho wa ya wanadamu wote.
(2). Maisha pekeyake yanaweza kuanzisha maisha mengine. Hii ndiyo kanuni ya ki-Biokemia kwa kuwa Uzima wa Milele ni ZAWADI kutoka kwa Mungu, basi ni Mungu tu mwenye kuwa na uweza wa kutokufa ndiye anayeweza kuutoa uzima huu. Na kama Yesu angekuwa ni mwanadamu tu, basi tusingeweza kuupata uzima wa milele kupitia kwake na asingeweza kuwa Mwokozi. Wanadamu hawezi kuwa na uzima wa milele ndani yake mwenyewe, lakini kama Mungu alivyo kuwa “Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake” (Yohana 5:26 na 1Yohana 5:11-12).
Kwa upande mwingine lakini, Yesu ni mwanadamu pia. Kwa kuwa ni mwanadamu ndiye aliyeziasi Sheria za Mungu ambaye yuhai wakati wote ((Yohana 1:1-2) ndipo kwa kweli alifanyika kuwa mwanadamu katika mwili (aya ya 14). Yeye aliyekuwa Mungu hakika akafanyika kuwa mwanadamu mwenye mwili (1Yohana 4:2-3). Alitungwa mimba na kuzaliwa na bikira Mariamu (Mathayo 1:18, 16, 23; na 2:2). Hakufanyika kuwa mwili tu, bali alifanyika pia kuwa mwanadamu kimwili na damu. (Waebrania 2:14).
Yesu aliijiita mara kwa mara kuwa ni Mwana wa ADAMU, na pia Mwana wa MUNGU, (Mathayo 16:13-17). Yuko SAWA na Mungu (Wakolosai 2:6). Aliitwa Mungu (Yuda 1:24-25; Tito 2:10,13). Kwa hiyo yeye ni Mungu. Biblia ina nukuu nyingi kuhusu jambo hili na zilizo hapo juu ni chache tu kati ya nyingine nyingi zinazoshuhudia.
Ndiyo, Yesu ni “Yehova” ingawaje neno hili limetafsiriwa vibaya kwenye Biblia ya Kiingereza ya Reversed Version. Jina asilia la Kiebrania lina consonanti “YHVH”. Lilipoandikwa kwa Kiebrania, vokali ziliachwa na zilisikika kwenye matamshi tu. Kwa hiyo, jina hasa lilikuwa halijulikani. Bali kwa leo inadhaniwa kuwa lilikuwa ni “Yahwe”. Maana yake kwa Kiingereza ni “WAMILELE” au “MWENYE KUISHI MILELE” au “ANAYE KUISHI NA KUDUMU KWA UWEZA WAKE MWENYEWE PASI KUTEGEMEZWA”. Ilistahili kuwa “Yahwe”, au ni kama ilivyozoeleka kuitwa “Yehova”, au ni kama ilivyoandikwa kwenye Biblia ya Authorised Version “BWANA” wa Agano la Kale ni Mungu Baba wa Yesu Kristo. Haya ni makosa makubwa sana! “Yahwe alikuwa ni Mungu wa Israeli. Na ndiye aliyekuwa anajulikana kuwa ni Mungu pekee kwenye ibada za Israeli. Wao hawakumjua Mungu Baba.
Kwenye Mwanzo 1 jina la Kiebrania lililotumika kutafsiri jina “Mungu” ni “Elohim”. Hili ni jina lenye umoja wenye muunganiko na wengi ndani yake kama tunavyotaja “kanisa” au “familia”. Kanisa na familia vinajumuisha watu wengi ndani yake, zaidi ya mmoja, lakini bado linaitwa kanisa au familia moja. Kwa mtazamo wa aina hii jina “Elohima” linaashiria wote wawili, Mungu Baba na Yahwe ambaye ni “Logos” au NENO la Mungu ambaye kwao Roho anatokea, Roho Mtakatifu ambaye ni UZIMA, KITU HALISI na UWEZA wa Mungu.
Yesu analipokuwa akiliombea Kanisa alisema kwamba waumini wake wote wawe “kitu KIMOJA” (Yohana 17:11, 21). Kanisa ni Mwili MMOJA, lakini limeundwa kwa waumini wengi (1Wakorintho 12:12). Na mume na mke ni MWILI MMOJA, lakini wanaonekana kuwa ni watu wawili walio mbalimbali. Kwa hiyo Kristo na Mungu Baba ni Mungu MMOJA, na sio Miungu miwili, na—“ELOHIM” Mmoja. Na ndio maana Elohim alisema “NA tumfanye mtu kwa mfano WETU” (Mwanzo 1:26).
Yahwe alikuwa ndiye “NENO” au msemaji wa ofisi ya Uungu—mshiriki wa pili. Mara tu baada ya Mungu kuanza KUONGEA na wanadamu, ilikuwa ni yuhu “Yahwe” ndiye aliyekuwa akiongea nao (imetafsiriwa “BWANA” kwenye tafsiri ya Authorised na “Yehova” kwenye tafsiri ya Revised Version). Tazama kwenye Mwanzo 2:16, 18, nk, na pia tazama kwenye Kutoka 20:2, nk—kila mara inasema “Yahwe” kwenye tafsiri asilia ya Kiebrania “NENO” aliyefanyika mwili. Ili kuthibitisha hili kunahitaji masomo ya kina na yatakayogharimu kurasa nyingi kwa mamia ili kuthibitisha hili.
Ili kuthibitisha kiufupi, fananisha na Isaya 6:1-3 na 10 na Yohana 12:39-41; Isaya 8:13 na 1Petro 2:7-8; Isaya 40:3 na Mathayo 3:3 na Marko 1:3. Yohana alitengeneza njia kwa ajili ya “Yahwe” (Isaya 40:3) ambaye ndiye Kristo (Marko 1:12-15) kwenye Ufunuo 1:17, 8 na 22:13, Yesu Kristo (pia tazama Ufunuo 22:16 kwa uthibitisho kuwa alikuwa ni Yesu aliyekuwa anasema) alijiita kuwa yeye ni “Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho, wa Kwanza na wa MWisho”. Kwenye aya zilizo kwenye Isaya 44:6 na 48:11-12, (aya za 17-18 zinaonyesha kuwa ni Yahwe aliyekuwa akinena) na Isaya 41:4, YAHWE ni wa Kwanza na wa Mwisho Kwenye 1Wakorintho 10:1-4 “MWAMBA” wa Agano la Kale ulikuwa ni Kristo. Kwenye Kumbukumbu la Torati 32:3-4; IISamweli 22:2-3, 32; na Zaburi 18:1-2; “MWAMBA” huu huu ni Yahwe. Wakati Musa alipokuwa anaongea na YAHWE, na kumuuliza jina lake, (Kutoka 3:4-5, 13), alimjibu kuwa jina lake ni MIMI NIKO (aya ya 6 na 14) na YAHWE (aya ya 15). Pia tazama Kutoka6:2-3. Kwenye Yohana 18:5-8, mara tu baada ya Yesu kujitambulisha kwa makutano walioongozwa na Yuda kuwa yeye ni “MIMI NIKO” (kiponauni cha “yeye” kwenye uandishi mlalo kimeongezwa pasipo uvuvio, na hakikuwepo kwenye nakala asilia za mwanzoni), ndipo walirudi nyuma na kuanguka chini. Tena kwenye Yohana 8:56-58, Yesu aliijiita mwenyewe “MIMI NIKO”. Pia kwenye Ufunuo 1:10 na mahali pengine.
Mtu mwenye Uungu ambaye ndiye MKOMBOZI wetu ni Yesu Kristo (Yohana 4:42, Wagalatia 3:13, Wafilipi 3:20, Tito 2:10-14, Luka 1:58-59, nk, nk. Yesu Yule ndiye YAHWE, tazama kwenye Isaya 49:7; Isya 60:16; ambapo panasema pia kuwa yeye “Mwenyezi wa Yakobo”—(kwa hiyo, kuwa ni WA Yakobo kunamaanisha mwana, au uzao wa Yakobo)—Mwenyeenzi wa wana wa Yakobo. Pia kwenye Isaya 48:17 inasema YAHWE ndiye Mkombozi, na Mtakatifu wa Israeli—Ndiye aliye Mtakatifu wa Israeli! Ni sawa na ilivyoelezewa kwenye Isaya 43:14. Kumbuka pia aya inayofuatia (15), YAHWE ni Mtakatifu wa Israeli, Muumbaji wa Israeli, Mfalme wa Israeli. Sasa tega usikivu wako kwenye Matendo 3:14 ambako ni Kristo waliomkataa Wayahudi alikuwa ni huyuhuyu “MTAKATIFU—YAHWE! Pia tazama Matendo 2:27 na Marko 1:24.
Je, Daudi mchungaji alikiwa ni nani?—Zaburi 23:1, YAHWE. Kwenye Yohana 10:11, Yesu alisema kuwa yeye alikuwa ni mchungaji. Pia Waebrania 13:20, na 1Petro 2:24-25, na 5:2-4. Ni YESU KRISTO anayekuja tena Kimwili na akiwa Mfalme wa Wafalme kutawala, kuja KUYAFANYA MAMBO YOTE UPYA, (Ufunuo 19:13, 15; 17; 14; 1:5; na Matendo 3:20-21). Mchungaji Mkuu anayekuja KUTAWALA akiwa kama MFALME wa Mfalme wote ni YAHWE—Ezekieli 34:11, 30-31; na sasa weka mtazamo wako kwenye Isaya 2:1-4 na Mika 4:1-4— Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya Bwana [YAHWE] utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi.Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu ‘YAHWE] wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naye atawakemea mataifa wenye nguvu walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake; wala hapana mtu atakayewatia hofu; kwa kuwa kinywa cha Bwana wa majeshi kimesema hivi.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW