Saturday, January 5, 2019

AMINI KWA KURATARAJIA YASIYOWEZA KUTARAJIWA

Image may contain: sky, cloud, nature and outdoor
Katika maisha ya kawaida mwanadamu yeyote anataka awe na usalama wa maisha, kwa mfano awe na nyumba nzuri na mali za kutosha na labda biasha kubwa inayo muingizia kipato kizuri; Lakini, matakwa haya ya binadamu si mara zote yanakuwa kama tupendavyo na wakati mwingini maisha yanaweza kuwa magumu kiasi cha kujiuliza, hivi Mwenyezi Mungu yupo wapi?

Mambo yasiyowezekana kwa wanadamu yanawezekana kwa Mungu.” (Luka 18:27)

Yesu anatuambia katika Luka 18 aya ya 27 kwamba, yote yasiyo wezekana kwa Mwanadamu, yanawezakana kwa Mungu. Je, ni jambo gani basi tufanye ili tuweze kupokea baraka za Mungu?

Hebu tumsome Abraham na tujifunze yeye alifanya nini mpaka akawa na Isaka ambaye alimpata uzeeni.

Warumi 4: 18 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
19 Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara.
20 Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu;
21 huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.
22 Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.

Abraham aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa. Aliamini ahadi ya Mungu na hakusita kwa kuto kuamini ingawa alikuwa umri karibia miaka mia moja na Mkewe Sara alikuwa amekufa kizazi.

Mwanzo 18: 9 Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani.
10 Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.
11 Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake.
12 Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee?

Abrahamu aliamini yote yalio semwa na Bwana kwa hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi. Warumi 4:21.

Neno la Mungu linasema katika Isaya 55: 11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.

Hakika Neno la Mungu litokalo kwenye kichwa chake halitarudi bure, bali litatimiza mapenzi yake na ndio maana Abraham aliamini kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyo ahidi.

Je, ni ahadi gani ulipewa na Mungu na bado unasubiri mpaka hii leo? Je, bado unaamini kuwa Mungu kamwe Neno lake haliwezi kurudi bure bali litakamilisha na kutimiza mapenzi yake?


Basi anza kuamini Neno la Mungu kama jinsi Baba yetu Abrahamu alivyo amini. Mambo yasiyowezekana kwa wanadamu yanawezekana kwa Mungu.” (Luka 18:27)

Shalom,

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW