Friday, December 7, 2018

NENO IDI MAANA YAKE NINI?

Image may contain: 4 peopleWAISLAM WENGI HAWAJUI MAANA YA NENO IDI.
NENO IDI MAANA YAKE NINI?
“Wakristo wengi husilimishwa kwa sababu ya kutojua lugha ya kiarabu”
Najua pengine unaweza usinielewe, Ila huo ndiyo ukweli, na mimi mwenyewe kabla sijaachana na Uislamu, nilishawahi kushuhudia, mke wa mchungaji wa Kanisa la BAPTISTI, akisilimishwa katika viwanja vya Mkanyenye Mwanza, kwa sababu ya kukuta neno Eid (عيد) Ndani ya BIBLIA, katika Tafsiri ya kiswahili cha zamani, ambacho katika Kumbukumbu la torati, 16:14 Kiliandika Idi.
Kumbukumbu 16: 14 nawe utafurahi katika Idi yako, wewe, na mwanao, na binti yako, na mtumwa wako, na mjakazi wako, na Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako.
👉Aliposomewa andiko hilo, akaulizwa kwamba, “Wanaosherehekea Sikukuu ya Idi ni watu wa dini gani?” akajibu “Waislamu” akaambiwa, Biblia inautambua Uislamu, akasilimu!
👉Siyo huyo tu Kuna mwingine, pia, alisilimishwa, kwa sababu ya neno Shehe ndani ya Biblia.
Nehemia 5:17 Pamoja na hayo wakawako mezani pangu, katika Wayahudi na mashehe, watu mia na hamsini, zaidi ya wale waliotujia kutoka kwa makafiri waliotuzunguka.
Mtu anaulizwa, Masheikh ni watu wa dini gani? Akijibu kwamba ni waislamu, basi hutakiwa kusilimu, ili aungane na Masheikh katika Uislamu.
👉Leo nataka nikifundishe, ili kukutoa kwenye huo utata! Ili hata kama watakakuja kukudanganya, basi uwaumbue, kwa sababu utakuwa umeshaelewa. nikianza na neno Idd.
👉Neno Iddi, ni neno la Lugha ya Kiarabu, kiswahili, kimechukua maneno mengi ya lugha ya Kiarabu, wakati wa kutafsiri, waliliweka kama lilivyo, yaani Iddi.
Katika kiswahili, Idi ni sikukuu, iliposemwa utafurahi katika Idi yako, maana yake utafurahi katika sikukuu yako.
Ukisoma katika Biblia ya Kiarabu, kila palipotajwa sikukuu kumeandikwa Iddi. Mfano Yohana 14:6
انجيل يو حنا
6: 4 وَكَانَ الْفِصْحُ عِيدُ الْيَهُودِ قَرِيباً.
Hapo nimenukuu Injili ya Yohana katika Lugha ya kiarabu, inasema:-
وَكَانَ الْفِصْحُ (Wakaana Al’fisuhu)
Nayo Pasaka 👆
عيد اليهود
Sikukuu ya Wayahudi (Eid al’yahuud)
قريبا
ilikuwa Karibu. (Qariiban)
Katika Kiarabu limetumika neno عيد (Idi) Likimaanisha sikukuu, kama katikaTafsiri ya kiswahili lingewekwa kama lilivyo, ingesomeka “Nayo Pasaka Iddi ya Wayahudi, Ilikuwa karibu,
Sikukuu yo yote kiarabu ni Idi, Sikukuu ya Muungano, ni Idi ya muungano, Unaweza kusema:-
👉Iddi ya Muungano
👉Iddi ya wapendao
👉Iddi ya Uhuru
👉Iddi ya Krismasi
Kwa sababu Neno Idi lina maana ya sikuu, na ndani ya Quran hakuna sehemu kumeandikwa, Sherehekeni Sikukuu ya Iddi, maana ni sawa na kusema, Sherehekeeni Sikukuu ya Sikukuu, hapo inakuwa haijakaa sawa, maana ni neno moja. Kwa hivyo usiyumbishwe, hakuna sikukuu ya Idmdi bali Idi ndo sikukuu.
Hata Waislamu wenyewe, Iddi (Sikukuu) Wamezipa majina yao.
👉Eid El fitry (Sikukuu baada ya mfungo wa mwezi ramadhani)
👉Eid El hajj (sikukuu ya kuchinja)
Tuje kwenye Neno Sheikh (Shehe) Neno hilo pia halina mahusiano kabisa na Dini, maana neno Sheikh, ni neno la Kiarabu, likiwa na maana ya mzee (شيخ)
Kwani hata ndani ya Quran neno hilo Sheikh (شيخ) Limetamkwa mara moja tu, na tena mtamkaji akiwa ni mwanamke, Sara akimsemea mumewe, katika.
Quran 11 SURATUL HUUD
ﻗَﺎﻟَﺖْ ﻳَﺎ ﻭَﻳْﻠَﺘَﻰ
ﺃَﺃَﻟِﺪُ ﻭَﺃَﻧَﺎْ ﻋَﺠُﻮﺯٌ ﻭَﻫَـﺬَﺍ
ﺑَﻌْﻠِﻲ ﺷَﻴْﺨًﺎ ﺇِﻥَّ ﻫَـﺬَﺍ
ﻟَﺸَﻲْﺀٌ ﻋَﺠِﻴﺐٌ
72. (Mkewe Ibrahim)
akasema; Ee mimi we! Je,
nitazaa na hali mimi ni
mkongwe na huyu rnume wangu
ni mzee sana hakika hili ni
jambo la ajabu.
Sara katika kiarabu amesema:-
ﻭَﻫَـﺬَﺍ
ﺑَﻌْﻠِﻲ ﺷَﻴْﺨًﺎ
Na Mume wangu ni mzee, neno Hilo mzee kiarabu limetamkwa ﺷَﻴْﺨًﺎ yaani Sheikh
Ndilo neno pekee la Sheikh ambalo linapatikana ndani ya Quran, likiwa na maana ya mzee na siyo kiongozi wa Msikiti, au Kiongozi wa Dini, Kwani hata katika Biblia, kila palipotajwa mzee, Kiarabu ni ﺷَﻴْﺨًﺎ (Sheikh) Ushahidi huu hapa:- 👇
Walawi 19:32 Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee; nawe mche Mungu wako, Mimi ndimi Bwana.
Katika kiswahili limetumika neno mzee, Kiarabu 👇🏻
19: 32 من امام الاشيب تقوم و تحترم وجه الشيخ و تخشى الهك انا الرب
Hapo kumetajwa, وجه الشيخ Uso wa Sheikh (mzee) Sheikh inatafsiri ya Mzee, na pia katika ushahidi mwingine, ni kwa Nikodemo.👇
Yohana 3:4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
Katika Kiswahili, Kumetajwa neno mzee, katika Kiarabu kumeandikwa hivi.👇
3: 4 قال له نيقوديموس كيف يمكن الانسان ان يولد و هو شيخ العله يقدر ان يدخل بطن امه ثانية و يولد
Hapo kumetajwa و هو شيخ Nae ni mzee yaani Sheikh, yaani Sheikh anawezaje kuingia tumboni kisha akazaliwa mara pili? Sheikh hiyo haina maana ya kiongozi wa dini, bali Sheikh kwa umri mkubwa. Mtu mzima asiweze kuingia tumboni.
Pia hata Wazee wa Kanisa, nao pia katika Kiarabu ni Masheikh.
Yakobo 5:14 Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.
👆Hapo ni Kiswahili wametajwa wazee wa kanisa, Kiarabu 👇
5: 14 امريض احد بينكم فليدع شيوخ الكنيسة فيصلوا عليه و يدهنوه بزيت باسم الرب
Hapo kumesemwa, شيوخ الكنيسة
Masheikh wa Kanisa, Kumetumika uwingi, شيو خ Masheikh المكنسة wa makanisa.
Kwa hivyo usiyumbishwe na Lugha, kwa kusikia au kusoma neno liliotaja Neno Sheikh au shehe, ukadhani ni kiongozi wa kiislamu, hapana, bali limetumika kwa maana ya mzee. Nehemia kukaa na mashehe, inamaana ya Wazee, na siyo Waislamu.
BY USTADH MHUBIRI WA INJILI, ABEL SULEIMAN SHILIWA
Shalom

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW