Tuesday, December 25, 2018

KWANINI WAKRISTO TUNASHEREHEKEA KRISMAS? = SEHEMU YA PILI =

Image may contain: text
SOMO:-UKWELI KUHUSU SIKUKUU YA KRISMASI
NA
SABABU ZA MSINGI KI-BIBLIA ZINAZOTUFANYA WAKRISTO KUSHEREKEA KRISMASI .
Ili rahisi kwetu kulielewa vizuri somo hili. Tutajifunza somo hili kwa kuligawa katika vipengele vinne ambavyo ni:-
1. MAANA YA NENO KRISMASI
2. HISTORIA YA KRISMASI NA TAREHE 25/ DESEMBA
3. MAMBO YA KUYAELEWA NA KUYAZINGATIA KUHUSU HISTORIA YA KRISMASI
4. SABABU ZA MSINGI KI-BIBLIA ZA KUWAFANYA WAKRISTO TUSHEREKEE KRISMASI
Mistari muhimu ya kukumbuka :-
L U K A 2:9-11:-"Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana."
Z A B U R I 118:22-24:"Jiwe walilolikataa waashi Limekuwa jiwe kuu la pembeni. Neno hili limetoka kwa BWANA, Nalo ni ajabu machoni petu. Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA, Tutashangilia na kuifurahia."
Amen!.
INAENDELEAA sehemu ya pili..........!
4/ KIPENGELE CHA NNE
SABABU ZA MSINGI KI-BIBLIA ZA KUWAFANYA WAKRISTO TUSHEREKEE KRISMASI
Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu.
Katika sehemu ya kwanza ya somo hili lilopita tulichambua sana kwa undani kuhusu krismasi na pia tuliona sababu kuu sita (6) ki-biblia zinazotufanya wakristo kusherekea sikukuu ya Krismasi.
Leo katika somo letu tunamalizia kuendelea pale tulipoishia.
Sijui kama ulishawahi kujiuliza swali kama hilo, au sijui kama ulishawahi kuulizwa swali kama hilo. Au sijui wewe mwenzangu unasherekea sikukuu hii kwa sababu unajisikia kusherekea.
Tunasherekea sikukuu hii kwa sababu nyingi mno, ambazo hata kama nikizieleza mahali hapa, basi hakika hapatatosha kabisa.
Lakini nataka nimalizie tena Leo nikuambie baadhi ya sababu tano tu za msingi zinazotusukuma sisi sote wakristo ulimwenguni kusherekea sikukuu hii ya christmas. Na Sababu hizo ni kama zifuatazo;
??(7) Tunasherekea sikukuu ya Christmas kwa kukumbuka kuzaliwa mwokozi, masihi wetu yaani Yesu Kristo wa Nazareti.
Biblia inasema katika LUKA 2:10-11:-" Malaika akawaambia, msiogope; kwakuwa Mimi nawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; MAANA LEO katika mji wa Daudi, AMEZALIWA KWAAJILI YENU, MWOKOZI, NDIYE KRISTO BWANA".
Haleluyaaaa?
Kama tulivyotangulia kuona kwamba Kumbukumbu za kuzaliwa kwake Yesu Kristo hazimaanishi kwamba alizaliwa tarehe 25 Disemba exactly.
Ikumbukwe kwamba hatusherekei tarehe bali tunasherekea kumbukumbu ya tukio la kuzaliwa kwa Mwokozi, nimesema hivyo maana wako watu wengine waliochanganywa na misongo ya ki-maisha wakidhani tunasherekea siku, au tarehe fulani. La hasha!
Watu wa namna hii, sikukuu ya christmas imewachanganya hata kutafuta kujua kwamba ni siku gani au terehe gani aliyozaliwa Bwana Yesu.
Siku wala tarehe haitusaidii sisi chochote kabisa, tena tarehe kwetu ni ya nini basi!?
La msingi hapa Tunachotaka kujua ni kuwa na kumbukumbu tu ya ujio wa Bwana na kwa hiyo tunasherekea.
Nabii Isaya alitabili kuzaliwa kwa Yesu ( takribani miaka 700 iliyopita kabla ya kuzaliwa kwake Bwana Yesu Kristo ) akisema;
"...bikira atachukua mimba,atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli." (ISAYA 7:14).
Tabiri hii ya Nabii Isaya ni hakika na kweli. Zipo tabiri nyingi zilizowahi kutolewa, lakini tabiri ya nabii Isaya imekamilika maana hakika Bwana amezaliwa. Kuzaliwa kwa Bwana Yesu ni muujiza ambao haukuwai kutokea wala haitegemewi kutokea, sababu kuzaliwa kwake kulitokana na UWEZA wa Roho Mtakatifu. Tena angali Bwana Yesu amezaliwa alikuwa tayari amekwisha vikwa uwezo, uweza na nguvu ndani yake.
Sasa waweza kufikiria kwamba ni mtoto gani anayezaliwa akiwa na utiisho wa ki-Mungu kama huo, kwa sababu Biblia inaanza kumuelezea kwamba alipozaliwa tu aliitwa mtoto mwanamume, yaani si mtoto wa kiume bali ni mwanamume ikionesha tayari alikuwa na nguvu za kipekee tena Yeye ni Imanueli Mungu pamoja nasi
[ Mathayo 1:23 ]
(8)Tunasherekea kukumbuka ujio wa wokovu kwa mwanadamu.
Biblia inasema katika WAEBRANIA 2:3:-"SISI JE! TUTAPATAJE KUPONA, TUSIPOUJALI WOKOVU MKUU namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana Yesu, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia".
Sote twafahamu kwamba mwanadamu alipotea baada ya lile anguko la dhambi ya Adamu na Hawa pale bustanini Edeni. Mwanadamu alikuwa amehesabiwa kutokuwa na maisha ya raha ya umilele. Lakini kwa kuwa Mungu aliupenda ulimwengu, yaani Bwana Mungu alikupenda wewe na mimi ndipo akamtuma mwanaye wa pekee Yesu Kristo ili kila amuaminie awe na uzima wa milele ( Yoh.3:16 ). Kwa lugha nyepesi ni kwamba tunasherekea siku hii kukumbuka WOKOVU aliouleta Bwana Yesu, maana ndani yake ndimo kuna maisha halisi ya umilele.
YOHANA 1:4:-" Na ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, na ule uzima ulikuwa Nuru".
(9) Tunasherekea kwa kukumbuka ushindi wa Mungu ndani ya Yesu Kristo dhidi ya mamlaka mbovu ya shetani chini ya jua hili.
SIKIA;
Biblia inasema;
" Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana." (WAGALATIA 4:4-5).
Kumbe kabla ya ujio na kumpokea Bwana Yesu Kristo sisi tulikuwa chini ya sheria. Tukiitumikia miungu ya baba zetu, tulikuwa watu tusiokuwa na Mungu duniani. Hivyo basi hatukuweza kufanyika wana wa Mungu, bali ingawa tulikuwa ni watu wa Mungu tu.
Kwa kuliona hili, Bwana Mungu akamtuma mwanaye azaliwe chini ya sheria ili atukomboe sisi sote na tupokee hali ya kuwa wana wa Mungu. Mungu akarejesha ushirika wa Roho wake kwa mwanadamu, ushirika uliokuwa umepotea pale bustanini baada ya dhambi.
YOHANA 1:12-13:-" BALI WOTE WALIOMPOKEA ALIWAPA UWEZO WA KUFANYIKA WATOTO WA MUNGU, ndio wale walioaminio jina lake; waliozaliwa, sio kwa damu, wala sio kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu".
1 YOHANA 3:1-2:-"Tazameni , ni pendo la namna gani alilotupa Baba, KWAMBA TUITWE WANA WA MUNGU; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu hautambui, kwakuwa haukumtambua yeye . Wapenzi , SASA TU WANA WA MUNGU, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa , tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo ".
Unajua kama Bwana Yesu asingezaliwa, basi tungebakia kuwa ni watu wa miliki ya shetani, watoto wa Ibilisi milele.
Lakini ashukuruliwe Mungu kwa kuzaliwa kwake Yesu Kristo duniani, tumepokea neema na upendo wa kufanyika watoto wa Mungu aliye hai.
(10) Tunasherekea sikukuu hii kwa kukumbuka ujio wa injili duniani.
Biblia inasema katika MARKO 1:1:-" Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu".
Yesu mwenyewe ndio injili.
Yeye alipozaliwa, njili ndio ilizaliwa kwa mara ya kwanza chini ya jua.
Maana Yeye ni neno, INJILI NI HABARI NJEMA ZILETAZO WOKOVU, hivyo ni neno la Mungu liletalo wokovu kwa kila aaminiye. Biblia imeeleza vizuri sana jambo hili, inasema:-
" Malaika akawaambia, msiogope; kwakuwa Mimi NAWALETEA HABARI NJEMA YA FURAHA KUU itakayokuwa kwa watu wote" ( LUKA 2:10).
Malaika wa Bwana anatambulisha kuwa ujio wa Yesu Kristo duniani ni ujio wa habari njema ya furaha kuu. Yaani ni ujio wa Injili, maana injili ina furaha ndani yake katika kumbadilisha mtu aliyekuwa mwovu na katili ,kumfanya awe mtu mpya mwema, mwuungana, mwenye ukarimu na upendo.
WARUMI 1:16:-" Kwa maana siionei haya INJILI; KWA MAANA NI UWEZA WA MUNGU ULETAO WOKOVU, kwa kila aaminiye, kwa myahudi kwanza, na kwa myunani pia."
(11) KWA KUZALIWA KWAKE YESU KRISTO, TUMEIPATA IMANI ILIYO BORA ZAIDI
Mpaka hapo tumeona sababu kuu kumi (10) za msingi .
Zipo sababu nyingi mno, nyingi sana zinazotufanya wakristo tusherekee sikukuu hii ya Krismasi kwa furaha tele. SIKU YA KUZALIWA MASIHI NI SIKU KUBWA SANA, maana ni kumbukumbu tosha ya ujio wa Ukristo duniani kote. Biblia inasema juu ya hilo katika
WAEBRANIA 12:2:-" TUKIMTAZAMA YESU, MWENYE KUANZISHA NA MWENYE KUITIMIZA IMANI YETU; ambaye kwaajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa Mungu".
2 PETRO:-" Simon, Petro mtume na mtumwa wa Yesu Kristo, KWA WALE WALIOPATA IMANI MOJA NA SISI, YENYE THAMANI, katika hali ya Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo".
IMANI YA UKRISTO TULIYOIPOKEA NI IMANI BORA ZAIDI kupita imani zoote duniani. Na Hakuna mtu bora, wa maana mno na wa muhimu sana duniani kama kuwa mkristo. Mkristo ni mtu wa muhimu sana duniani, maana yeye ndiye ofisi /wakili wa ufalme wa Mungu duniani.
Sasa basi kama Yesu asingezaliwa wala hata imani yetu hii ya Ukristo iliyobeba ndani yake: Neema na kweli, baraka na rehema, uweza, mamlaka na nguvu zote za Mungu aliye hai; Isingekuwapo duniani (Yohana 1:16-17; 1 Petro 5:10-12; Waefeso 1:3; 1 Korintho 2:4-5; Mathayo 16:18-19; Luka 10:17-19).
Lakini KWA KUZALIWA KWAKE YESU KRISTO , TUMEIPATA IMANI ILIYO BORA ZAIDI.
NB.
Ngoja nikuambie siri hii , hivi unajua kwamba hakuna msalaba pasipo kuzaliwa kwake Yesu Kristo wa Nazareti. Msalaba ulimuhitaji Yesu azaliwe kwanza chini ya dhambi ingawa Yeye hakutenda dhambi kabisa (Waebrania 4:15).
Sasa unisikilize ndugu; sherehe hii haina maana kwako kama bado Bwana Yesu Kristo hajazaliwa ndani yako. Umaana halisi ni ule Yesu kuzaliwa ndani yako. Kuzaliwa Yesu ndani yako ni kumpa maisha yako, NI KUOKOKA TU.
WARUMI 8:37:-" Lakini KATIKA MAMBO YOTE TUNASHINDA, NA ZAIDI YA KUSINDA, kwa yeye aliyetupenda".
1WAKORINTO 15:57:-"Lakini Mungu na ashukuruliwe ATUPAYE KUSHINDA kwa Bwana wetu Yesu Kristo".
Tazama hatuna njia nyingine ya ushindi isipokuwa njia hiyo tu kwa Yesu Kristo.
Hivyo tunapomalizia kusherekea kumbukumbu zote hizi ni sawa na kusherekea ushindi dhidi ya kila neno la maisha yetu ya kiroho hata kimwili pia, tunapokuwa ndani ya Bwana Yesu, tumeokoka.
Nakuambia hivi, mtu aliyeokoka siku hii ya Leo ya Krismasi anabubujika machozi ya furaha kwa ujio wa Bwana Yesu mkombozi wetu, na hawezi akakuelezea vyote akamaliza, kwa sababu mambo ya rohoni yana upana mkubwa mno hayaelezeki yakamalizika (Zaburi 119:96).
Tumesema ziko sababu nyingi mno ki-biblia zinazotufanya kusherekea sikukuu hii ya Krismasi.
Lakini ikumbukwe kuwa mambo ya rohoni, HUTAMBULIKANA KWA MTU WA ROHONI, lakini mtu wa mwilini siku hii ya Leo ya kumbukumbu ya ujio wa Bwana Yesu, kwake ni upuuzi tu tena kwake ni jambo la kawaida kabisa tena ndiyo siku ya kwake ya kupanga kufanya maasi. KUMBUKA MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI ; bali zawadi ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu ( WARUMI 6:23; YOHANA 10:9-10).
Baada ya kufa ni hukumu tu ndugu yangu ( Waebrania 9:27).
Kwanini usiutumie wakati huu kutafakari maisha yako yakojee mbele za Mungu ?
Hivi utaendelea kufanya dhambi zako mpaka lini jamani ?
NJOOOOO KWA BWANA YESU KRISTO LEO, mlango wa neema bado upo wazi kwa ajili yako. Bwana Yesu anakuhitaji awe Bwana na mwokozi wa maisha yako.
Ukihitaji msaada zaidi wa kiroho . Basi usisite kunipigia simu yangu hii hapa chini, ili Bwana Yesu mwenyewe akuhudumie siku hii ya Leo.
Nakutakia sikukuu njema. Na ubarikiwee.
I WISH YOU A MERRY CHRISTMAS AND HAPPY NEW YEAR.
Ukipenda kuwasiliana nami kwa ushauri , maombezi na mafundisho zaidi ya masomo ya neno la Mungu. Karibu :-
Mtumishi wa Mungu aliye hai.
MWL, REV:-ODRICK BRYSON
SIMU:- 0759 386 988; 0717 591 466
Email:- Odrick16@gmail.com.
Whatsapp group.
"KWELI YOTE YA NENO LA MUNGU ISIYOGOSHIWA"
[ 2 WAKORINTO 2:17 ]
SHALOM SHALOM SHALOM,
Max Shimba Ministries Org

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW