Tuesday, December 25, 2018

KRISMASI YA KWANZA ILIFANYWA NA MALAIKA

Image may contain: 2 people, people sitting and text
KRISMASI YA KWANZA ILIFANYWA NA MALAIKA
KUZALIWA KWA YESU NA KUSHEREHEKEWA NA MALAIKA
Ni muhimu kwa kila mmoja wetu kufahamu kuwa wa kwanza kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu - (KRISMASI) ni Malaika watakatifu wa Mungu
(Luka 2:8-15) 8 Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku. 9 Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. 10 Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; 11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana. 12 Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe. 13 Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema, 14 Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. 15 Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha Bwana.
Kama Malaika watakatifu wa Mungu walisherehekea kuzaliwa kwa Yesu, basi si dhambi kwa yeyote kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu, Malaika hawa walishuka kutoka mbinguni, wakimsifu Mungu kwa ajili ya tendo la Yesu Kristo kuzaliwa, kama malaika wa Mungu walimsifu Mungu, mimi na wewe hatuna budi kumsifu Mungu kwani kwa malaika kumsifu Mungu kunaonesha waziwazi jambo hilo limekubaliwa na Mungu,sio hilo tu kuzaliwa kwa Yesu kunatajwa na malaika kuwa ni furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote.
Maana yake Mwanadamu yeyote anapaswa kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu, na kuzaliwa huko kwa Yesu kuwe ni furaha kwake. Na kwasababu furaha hii kuu inatajwa kuwa itakuwa kwa watu wote, maana yake kila anayeitwa mtu, furaha hii ya kuzaliwa kwa Yesu inapaswa iambatane nae na kama hafurahii kuzaliwa kwa Yesu, huyu bila shaka, atakuwa sio mtu labda ni jini, maana jini hawezi kuwa na furaha ya kuzaliwa kwa Yesu, kwani kuja kwa Yesu kunamuondolea yeye mamlaka ya kuwatesa watu.
Sasa niwakumbushe maana ya Krismasi:
Christ na neno mass, ambayo yakiunganishwa yanazaa neno moja linaloitwa Christmas ambalo maana yake ni ibada ya Kristo.
Ibada hii ya Kristo duniani ilianza rasmi pale Yesu alipozaliwa na wakwanza kufanya ibada hiyo walikuwa ni malaika (Luka2:13). Malaika walishangilia na kumsifu Mungu kwa kuzaliwa kwake Kristo, hivyo basi kama malaika walimsifu Mungu kwa kuzaliwa kwa Kristo, na kwa mara ya kwanza walifanya ibada duniani yaani ibada ya Kristo, ambayo kwa kiingereza ndio Christmas.
Sisi nasi hatuna budi kufanya hivyo kwani tendo linalofanywa na maalaika watakatifu ni lazima tujue ni tendo takatifu, hivyo mwanadamu akisherehekea kuzaliwa kwa Yesu vilevile anafanya jambo takatifu na tujue pia jambo hilo linakuwa linampendeza Mungu.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW