Friday, December 7, 2018

JE, YESU KRISTO NI MUNGU?

No automatic alt text available.

Mungu maana yake nini?
Mungu siyo jina bali ni sifa na hakuna mtu anayeitwa jina (Mungu). Nisawa sawa na kusema "Raisi". Hili neno Raisi sio jina bali ni wasifa wa mtu. Yeye ndiye Chanzo cha habari njema inayopatikana katika Biblia. (1 Timotheo 1:11) Kwa kuwa Mungu ndiye aliyetuumba, tunapaswa kumwabudu yeye peke yake.​—Soma Ufunuo 4:11.
Mungu ni Mmoja, lakini Yeye yupo katika nafsi tatu-Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu (Mathayo 3: 16-17). Mungu hana mwisho (1 Timotheo 1:17), hawezi kulinganishwa (2 Samweli 7:22), na hawezi kubadilika (Malaki 3: 6). Mungu yupo kila mahali (Zaburi 139: 7-12), anajua kila kitu (Mathayo 11:21), na ana nguvu zote na mamlaka (Waefeso 1; Ufunuo 19: 6).
Je , Yesu anazo hizo sifa za kipekee za Mungu?
Mungu akawa mwili (Yohana 1:14). Mwana wa Mungu akawa Mwana wa Mtu na hivyo ni "daraja" kati ya Mungu na mwanadamu (Yohana 14: 6, 1 Timotheo 2: 5). Kwa njia ya Mwana tu tunaweza kuwa na msamaha wa dhambi (Waefeso 1: 7), upatanisho na Mungu (Yohana 15:15, Warumi 5:10), na wokovu wa milele (2 Timotheo 2:10). Katika Yesu Kristo "ukamilifu wote wa Uungu huishi katika hali ya mwili" (Wakolosai 2: 9). Hivyo, kwa kweli kujua Mungu ni nani, tunapaswa kufanya ni kuangalia Yesu.
Mungu wetu tunayemwabudu jina lake ni YEHOVA, yeye ni Mungu wa Biblia Takatifu.
Kutoka 6:2, 3
Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.
Mwana tunayemwamini ni Yesu ambaye ni Kristo.
Yohana 3:36
Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
Roho tunayoiamini ni Roho ya Kristo ambayo ni nguvu za utendaji kazi ya Mungu.
Isaya 1:25; 40:10, Ezekieli 3:14.
Pia Yesu akiri akisema hivi katika injili yake kama alivyoandika mtume Luka:
Luka 11:20
Lakini, ikiwa mimi natoa pepo kwa kidole cha Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia
KWANINI TUNASEMA YESU NI MUNGU?
Matamshi ya Yesu mwenyewe na mitume wake kuhusu Uungu wake.
Tuanze kuangalia uthibitsho wa aya za Biblia zinazomtaja Yesu kuwa Mungu:
Mathayo 1:23-25
“Tazama; bikra atachukua mimba; naye atazaa mwana; nao watamwita jina lake Emanueli; yaani Mungu pamoja nasi”.
Tabia ya Yesu inaonyesha kuwa kama mwanadamu, kuzaliwa kwake kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Hapa tunaona jinsi alivyo na uwezo tofauti na wanadamu akiwa anafahamu mambo mengi kabla yatokee, hiyo ni sifana uwezo kama wa Mungu..
Mathayo 18:20
“Kwa kuwa walipo wawili watatu, wamekusanyika kwa jina langu, mimi nipo papo hapo katikati yao”.
Mwenye uwezo wa kukaa mahali pote ni Mungu.
1 Yohana. 5:20
“Nasi twajua kuwa Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli., yaani ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye MUNGU WA KWELI NAUZIMA WA MILELE”.
Yohana 20:26-29
“basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu na milango ilikuwa imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu. Kisha akamwambia Tomaso lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu; wala usiwe asiyeamini; bali aaminiye. Tomaso akajibu akamwambia, BWANA WANGU NA MUNGU WANGU.
Tito 2:13
Tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu
Warumi 9:5
“Na katika hao alitoka KRISTO KWA NJIA YA MWILI, NDIYE ALIYE JUU YA MAMBO YOTE, MUNGU, MWENYE KUHIMIDIWA MILELE.AMINA.
Yesu Kristo ni mtawala juu ya vyote, hii ni moja kati ya sifa za Uungu Wake.
Yohana 3:30
“Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya vyote. Yeye aliye wa dunia asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani,yeye ajaye kutoka mbinguni yuu juu ya yote” (Yohana 13:13) “Ninyi mwaniita , Mwalimu, na Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo“. ( WARUMI 14:9 ) “Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii,awamiliki waliokufa na walio hai pia”. Neno kumiliki ni kutawala sifa ya kutawala ni sifa ya Mungu.
Yesu Kristo ni zaidi ya mtu awayeyote, manabii au mitume wote.
(Waebrania 3:1-7)“Mustari 3 unasema, Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile yeye atengenezaye nyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba”.. Anayezungumziwa hapa ni Yesu Kristo Mungu muumbaji. YESU, ameketi mkono wa kuume wa ukuu huko mbinguni (Waebrania 1 :3-4).
Matamshi ya Yesu mwenyewe na mitume wake kuhusu Uungu wake.
Yohana 10:30-33
“Yesu akawajibu, kazi njema nyingi niwewaonyesha zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe? Wayahudi wakamjibu, kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru,na kwasababu wewe uliye. mwanadamu wajifanya kuwa Mungu.
Wafilipi 2:5-6
“Ambaye yeye mwanzo alikuwan yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho, bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu”.
Yesu anaitwa Neno la Mungu Yohana 1:1, Ufunuo 19:13 “Kwahiyo Neno ni Mungu” .. na huyo ndiye aliyevifanya kuwako vitu vyote.Aliyeshuka kutoka juu na kufanyika mwili ni Yesu pekee aliyezaliwa na bikira Mariamu bila mbegu ya kiume kama inavyotokea kwa wanadamu wengine..Katika yeye vtu vyote viliumbwa (Wakolosai 1:13-16) vinavyoonekana na visivyoonekana; vya mbinguni na vya duniani. Maandiko yako wazi kabisa kwa mtu mwenye Roho wa Mungu anaelewa kwa urahisi.
Hapa ni baadhi ya sifa za Yesu Mungu Mkuu kama ilivyofunuliwa katika Biblia:
Mungu ni wa haki (Matendo 17:31), mwwenye upendo (Waefeso 2: 4-5), mwenye kweli (Yohana 14: 6), na mtakatifu (1 Yohana 1: 5). Mungu anaonyesha huruma (2 Wakorintho 1: 3), huruma (Warumi 9:15), na neema (Warumi 5:17). Mungu anahukumu dhambi (Zaburi 5: 5) lakini pia hutoa msamaha (Zaburi 130: 4).
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW