Friday, December 7, 2018

JE, MLIMA SINAI UPO MAKKA KAMA WANAVYO DAI WAISLAM?

Image may contain: one or more people and textSwali la Waislam kwa Wakristo: Kwenye Kutoka 19:11, Mlima Sinai ulikuwa Makka, kwa sababu Wagalatia 4:25 inasema ilikuwa Arabuni?

Jibu: Mlima Sinai upo kwenye rasi ya Sinai; isipokuwa Musa angekuwa na magari makubwa au matreni, Makka pangekuwa mbali mno. Mambo manne ya kuzingatia katika jibu hili.

1. Haidhuru: Kama Mlima Sinai ungekuwa Makka, pasingekuwa na tofauti yoyote kwa Wakristo, isipokuwa hatua za safari za Waisraeli zisingeeleweka. Hata hivyo, inaonekana kuwa ingekuwa muhimu kwa baadhi ya Waislam kwani kungelifanya wazo la kuwa Maka ilishiriki kwenye kazi ya Mungu kabla ya Muhammad la kuaminika. Hata hivyo, Waislam wengine, kama rejeo chini ya ukurasa 2504 kwenye Kurani Takatifu: Toleo la Kiingereza la Maana na Ufafanuzi (Holy Quran: English Translation of the Meanings and Commentary) linalinganisha Mlima Sinai na Jabal Musa, sawa na wengi wa Wakristo.

2. Arabuni tofauti: Katika Wagalatia 4:25 "Arabuni" si nchi ya leo ya Kiislam ya Saudi Arabia, bali jimbo la Kirumi la Arabuni. Jimbo la Kirumi la Arabuni lilikuwa ni rasi ya Sinai, sehemu ya kaskazini magharibi ya Jordan ya leo, na sehemu ndogo ya Syria. Tazama ama The Roman World uk.107 au Encyclopedia Britannica sehemu ya Historia ya Rumi ili kuiona ramani inayoonyesha hili. Kama rejeo la pembeni, Warumi hawakuwahi kutwaa sehemu ya karibu na Maka , kwa hiyo jimbo la Kirumi la Arabuni halingeweza kuhusisha Maka.

3. Siyo Makka: Watu wenye kondoo na ng'ombe wangeweza kutembea maili 6 tu kwa siku; hata kama wangekuwa na ngamia tu kwa kawaida wangeweza kwenda maili 12 kwa siku. Safari ya siku 11 umbali wa karibu maili 800 kutoka Maka kwenda Kadesh Barnea kwa miguu, pamoja na ng'ombe na kondoo, na watoto wadogo, ingekuwa ya kasi kubwa sana, isipokuwa kama wangekuwa na magari wakati huo. Tazama ama The Roman World uk.107 au Encyclopedia Britannica sehemu ya Historia ya Rumi ili kuona ramani.

4. Kwenye Rasi ya Sinai: Rasi ya Sinai ni pembetatu inayotazama kusini yenye milima upande wa kusini ambayo Kutoka 19:2 na Hesabu 3:14; 9:1,5; 10:12 vinaiita Nyika ("Jangwa") la Sinai. Jangwa la Sin linaitenganisha Elim na Sinai. Hesabu 33:3-50 inataja kila sehemu walipopiga kambi Waisraeli. Kwa bahati mbaya hatujui maeneo ya sehemu hizi za kambi, lakini kwa kuziangalia, tunaweza kuona ipi ipo kati ya wapi.

Ndani ya nyika ya Sinai, kuna milima miwili iliyo karibu karibu, yenye kulingana na mlima Sinai.

Gebel Musa/Mousa (futi 7,363) Haya ni maoni yaliyotokea zamani, angalau kuanzia karibu mwaka 500 B.K. Ina miteremko mirefu sana. Nyumba kubwa ya utawa ya Mt. Catherine ipo sehemu ya chini ya mlima huu. Wengi wa Waislam, lakini siyo wote, wanaona kama huu ndio mlima Sinai pia. New International Dictionary of the Bible uk.674 ina picha ya Jebel Musa.

Ras es-safsafeh (futi 6,540 mita 1993) ipo maili mbili (km 3.2) kaskazini mwa Gebel Musa kwenye mgongo huo huo. Ina uwanda mpana chini.

Gebel Serbal (haielekei kuwa hivyo): Eusebius (mwaka 325 B.K.) alidhani hivi. Lakini New Bible Dictionary (1978) uk.1193-1194 inaeleza kuwa hakuna nyika karibu na sehemu yake ya chini.

Kwa muhtasari, wakati ambapo Wakristo na hata baadhi ya Waislam wanaafiki kuwa mlima Sinai upo Sinai, tunaweza kuwa karibu na Mungu sehemu yoyote ile, na hatuhitaji mahali maalumu, sanamu za vyuma, au hata mawe meusi ili kuweza kuwa karibu naye.

Source Muslim Hope

Shalom,

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW