Sunday, September 10, 2017

OMBA MAOMBI HAYA KILA SIKU ASUBUHI, MCHANA NA USIKU

Image may contain: 3 people, text
Baba umenipa funguo muhimu katika Mathayo 16:19 za kufunga na kufungua. Ninatumia funguo hizo kufunga na kufungua, kuvunja na kubamiza kila kitu ambacho kinazuia kutimizwa kwa mipango yako kamili katika maisha yangu. Ninaamuru na kutangaza kwamba kila mnyororo, kamba, gereza, pingu kwamba zimefunguliwa, zimekatwa, na kuondolewa kutoka kwenye maisha yangu katika jina la Yesu.
Baba, Bwana Nakushukuru, kwamba wewe pekee ndiye hakimu wa maisha yetu, kwa mujibu wa Yeremia 17:9-10 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.
Baba naomba katika jina la Yesu, kwa mujibu wa Zaburi 22:19 Nawe, Bwana, usiwe mbali, Ee Nguvu zangu, fanya haraka kunisaidia. Baba naomba kwamba utusaidie, na kutupa uvumilivu wa kusubiri mapenzi yako kutimizwa.
Baba katika jina la Yesu, neno lako liniasema katika Isa 41:10-12 usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia. Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako.
Baba, ninakubaliana na neno lako lenye nguvu, uweza, uhakika, na la kujiamini, kwamba utawalinda watu wako dhidi ya maadui. Umetuambia kwamba kisasi ni chako asema Bwana, na utawalipa waovu. Bwana Ninakushukuru, kwa ajili ya ulinzi wako, na neno lako la nguvu na la ukombozi. Katika jina la Yesu.
Baba tunakushukuru kwa neno lako linalosema katika Ayubu 5:12 Yeye huyatangua mashauri ya wadanganyifu, Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao. Baba wa Mbinguni, ninachukua mamlaka ya neno lako kufunga, kufuta na kung’oa mipango yote miovu ya adui, nakuifanya kuwa utupu, batili, na kuifuta kwa jina la Yesu.
Baba katika jina la Yesu, umesema katika Zaburi 27:2 "Watenda mabaya waliponikaribia, wanile nyama yangu, watesi wangu na adui zangu, walijikwaa wakaanguka." Asante Bwana kwa ulinzi wako. Asante Bwana, kwasababu unatalnda. Wakati maadui zetu wanakuja kula nyama yetu, tunakuwa dhaifu, tumelala kiroho, tumekata tamaa, lakini uwezo wako katika damu umeruhusu maadui kuanguka ndani ya shimo la kuzimu. Asante Mungu wa huruma na neema, kwa upendo wako wa milele kwa watu wako.
Baba neno lako linasema nami katika Luka 10:19 kwamba “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.” Bwana natumia uwezo wako na mamlaka yako, ili kuvunja, kubamiza, kuponda, kung’oa, kutawanya vipande vipande, kila mipango ambayo shetani ameandaa dhidi ya maisha yangu, familia yangu, huduma yangu, nyumba yangu, uhusiano, fedha, na vitu vyote vilivyo vyangu. Nakushukuru Bwana, na ninadai ushindi kamili katika jina la Yesu.
Baba nasimama sawa sawa na neno lako katika Ayubu 6: 8 linalosema “Laiti ningepewa haja yangu, Naye Mungu angenipa neno hilo ninalolitamani sana!” Bwana Naomba katika jina la Yesu kwamba ombi letu utalijibu kulingana na mapenzi yako na kwa wakati, na utatupa vitu vilivyomo katika mapenzi yako kwa ajili yetu.
Baba katika jina la Yesu kulingana na Wafilipi 4:6 unatuambia “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.” Bwana nakushukuru, kwamba tunaweza kuja kwako wakati wowote kwa maombi ili haja zetu zijulikane kwako.
Baba kama ulivyosema katika Zaburi 23:1 Wewe ni mchungaji wangu, sitapungukiwa au kukosa vitu vyovyote vizuri katika maisha yangu. Wewe ni Mungu ambaye unatupatia mahitaji yetu yote. Nakiri kama ulivyosema, kwamba huwezi kuzuia mambo yoyote mazuri kwa watoto wako. Baba nadai faida zako zote za kiroho, na za kimwili. Katika Jina la Yesu.
Baba umetuambia katika neno lako, katika Luka 17:6 kwamba “Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.” Baba nachukua mamlaka ya neno lako leo, na kung’oa madeni yote ya kifedha, kila mapambano, kila misiba, kila ukosefu, uhitaji, na roho zote zinazoshambulia fedha zetu, afya, ndoa, nyumba, watoto, huduma, kazi zetu, na yote yaliyo yetu. Nazifunga, nakuzing’oa toka kwenye maisha yetu, na kuzitupa katika bahari. Katika jina la Yesu.
Baba umeniambia katika 2 Tim. 4:18 kwamba “Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.” Baba nakushukuru kwa kuwa umeniokoa na kila matendo maovu ya adui, na kunihifadhi kwa ajili ya ufalme wako wa mbinguni. Baba ninasimama sawa sawa na neno lako na kuyafunga kila matendo maovu, yaliyofanywa maishani kwangu, watoto wangu, familia yangu, nyumbani kwangu, huduma yangu, afya yangu, fedha zangu, mustakabali wangu na vitu vyote tunavyomiliki. Ninayafunga toka mashariki, magharibi, kaskazini na kusini, mbingu ya pili, katika maji, kwenye moto, katika hewa, katika ardhi, katika maeneo, katika mazingira, na kila maeneo chini ya jua, mwezi, nyota, na sehemu nyingine zote za siri yanakojificha. Ninaachilia neno lako, damu ya Yesu, na jina lako dhidi yao, katika maeneo hayo yote, kwamba yatakuwa yamefungwa milele na milele amina.
Baba natumia funguo muhimu katika Mathayo 18:18 kwamba “na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.” Ninajifungua, pamoja na kila kitu changu, toka kila mnyororo, vifungo, pingu, na kamba katika jina la Yesu.
Baba kama ulivyosema katika kitabu cha Hesabu 11:1. Nasimama kwenye mamlaka ya neno lako, na amrisha moto ushuke kutoka mbinguni na kuharibu kila roho ya kurudi nyuma ambayo imewekwa na adui katika maisha yetu. Katika jina la Yesu.
Baba, Bwana nasimama sawasawa na neno lako katika Joshua 1:8. Naomba maneno yako yasindoke vinywani mwetu wala mioyoni mwetu, bali tuyatafakari mchana na usiku, ndipo tutakapoifanikisha njia yetu.
Bwana ninaomba mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, niyatafakari hayo sawasawa na neno lako, katika Wafilipi 4: 8.
Baba umeniambia katika 2 Timotheo 1:7 kwamba Mungu hakunipa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. Baba napinga roho ya woga, nakataa kuwa na wasiwasi, au kukatishwa tamaa. Nautumia nguvu yako na mamlaka juu ya kila mipango na miradi ya adui. Nadai ushindi kamili juu ya nguvu zote za giza, katika jina la Yesu.
Baba neno lako linasema katika Yer 23:29 " Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande? Baba katika jina la Yesu, natumia moto wa Mungu kuteketeza kila uovu dhidi yangu, na wapendwa wangu, toka mashariki, magharibi, kaskazini na kusini. Natumia nyundo ya neno la Mungu kuvunja kila uovu wa vifungo vya nafsi, uhusiano wa damu, uchawi na laana zote mababu, uliopitia kwa uzao wetu. Najifunika, pamoja na kizazi cha pili, cha tatu na cha nne, kwa damu ya Yesu. Naachilia baraka za Bwana juu yetu, baraka za kizazi hadi kizazi, baraka za Ibrahimu, na baraka zote. Katika jina la Yesu.
Baba katika jina la Yesu. Navaa silaha zote za Mungu, napokea chapeo ya wokovu, navaa dirii ya haki kifuani, natwaa ngao ya imani, najifunga kweli kiunoni, nafungiwa miguu yangu utayari niupatao kwa injili ya amani na upanga wa roho ambao ni neno la Mungu kwa sala zote na maombi nikisali kila wakati katika Roho kwa mujibu wa Efeso 6: 10-18
Baba kwa mujibu wa neno lako katika Yer 30:17 Ulisema “Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana.” Nakushukuru kwa kutuponya machungu yetu, majeraha, makovu, na maumivu. Nakushukuru kwa ajili ya kuturejesha tena. Katika Jina la Yesu.
Baba katika Isa 53: 4-5, Ulisema “Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona." Bwana nakushukuru kwa neno lako, lina nguvu, linatupatia nguvu, ujasiri, ulinzi, na uponyaji katika jina la Yesu.
Baba nakushukuru, kama ulivyosema katika Zaburi 46:1 kwamba wewe ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Nakushukuru kwa kuwa tunaweza kukuita wakati wa shida.
Baba nasimama sawa sawa na neno lako katika Marko 3:27. Namfunga huyo mtu mwenye nguvu, nakuvunja kila vizuizi, kamba, vifungo, pingu, minyororo, minyororo ya utumwa, kutoka katika maisha yangu, wapendwa wangu, na yote yaliyo yangu. Ninaamrisha mali za mwenye nguvu kuharibiwa, sasa na hata milele. Katika jina la Yesu.
Baba nakushukuru kwa ulinzi wako, ulisema katika neno lako katika Kutoka 23:27 " Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao na kukimbia. Namshukuru wewe Bwana, kwa nguvu iliyopo katika neno lako ambayo husababisha maadui kuonyesha maungo yao na kukimbia. Katika jina la Yesu.
Baba katika jina la Yesu ninafungua machafuko na upofu wa mungu wa dunia hii, kutoka kwenye akili zetu, ambazo zinatuzuia kuona mwanga wa injili ya Kristo. Ninaita kila neno la Mungu linaloingia kwenye akili zetu, na moyo liinuke kwa nguvu ndani yetu.
Baba wa Mbinguni, asante ninakushukuru wewe, ninakutukuza wewe, ninakuabudu wewe, nakushukuru kwa neno lako katika Kumbukumbu 28:7 Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. Asante kwa nguvu yako, ulinzi, na usalama ambao umetoa kwa watoto wako, tukitumia neno, maadui si tu watakimbia, bali watakimbia kwa njia saba kutoka kwetu, katika jina la Yesu.
Baba nakushukuru, kwa mikono yako imara, na mkono wako wa haki wa kulia. Umetuambia, katika 1 Petro 5: 7 Tumtwike yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu. Bwana nakushukuru kwa kujishughulisha na mambo yetu, nakushukuru kwa kuwa tayari kwa ajili yetu wakati tunakuhitaji.
Baba katika jina la Yesu ninaliadhimisha jina lako; nakupa heshima na utukufu wote unaotoka kwenye jina lako takatifu. Neno lako linaniambia katika Joshua 1:5 “Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia kamwe wala sitakuacha.” Asante Bwana kwa ulinzi wako, na baraka.
Baba nakushukuru kwa neno lako katika 3 Yohana 1:2 linasema kwamba mipango yako kwa ajili yetu ni ya kutufanikisha, na kuwa na afya njema kama vile roho zetu zifanikiwavyo. Natumia mamlaka ya neno lako, na kudai ustawi, afya, furaha, mafanikio, amani ya akili, baraka, na kila mambo mema ambayo umepanga tupate, juu ya maisha yangu, wapendwa wangu, mali na vitu vyote nilivyonavyo, katika jina la Yesu.
Baba wa mbinguni neno lako katika Luke 8:11 linatuambia kwamba neno lako ni mbegu, na mioyo yetu ni ardhi. Bwana ninakuomba utayarishe mioyo yetu kupokea neno lako na kulificha katika mioyo yetu, tusitende dhambi dhidi yako, kwa jina la Yesu.

26 comments:

Edson rahl said...

Tunatakiwa tusali yote kwa wakatu mmoja au kuna vipengele?

Edson rahl said...

Je tunatakiwa kuomba yote kwa pamoja au kuna vipengele?

Unknown said...

Aminaa

Unknown said...

AMEN 🙏

Unknown said...

Amen

Unknown said...

Mungu akubariki kea huduma yako njema.

Unknown said...

asante sana kwa maombi mazuri na mungu skybariki sana.

Raymond said...

Asante kwa kuliona hili

Anonymous said...

Amina mtumishi. asante kwa kutupa muongozo mzuri

Anonymous said...

Ameen

3dtechdhs said...

daah amina sana.

hnkuluzi@gmail.com said...

Please send Swahili version

Unknown said...

Amina!
Mzidi kubarikiwa kwa maombi haya🙏🏾

Unknown said...

Amina!
Mzidi kubarikiwa kwa maombi haya🙏🏽

Kaizaly mvango said...

Amina naitwa kaizaly mdemu nimefarijika xana

Anonymous said...

amen

Anonymous said...

Ameen! Barikiwa sana.

Gerd Ulrich said...

Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma

Kwaheri Gerd Ulrich

Unknown said...

Ameen

Unknown said...

Maombi ya kukesha kuvunja

Explore eye said...

Amen🙏

Unknown said...

ameni; mungu aendelee kukupa ufahamu zaidi

Unow22 said...

As with any other shampoo, using too much of it can be very drying for your hair. Fortunately, the Old Style method includes a conditioner, so your hair won't suffer too much. With each wash, it removes toxins from the roots of your hair strands. In our testing, we used the Macujo approach, which yielded positive findings. Do plenty of study before deciding on a home remedy or a mix of home remedies to utilize to ensure that what you're doing is both safe for your hair and effective. When using any method or product, the most important thing is to stop consuming marijuana as soon as possible. Visit: https://www.urineworld.com/

Sam said...

Amen. Na asante kwa maombi mazuri ya kutufungua kiroho

Unknown said...

Amina

Unknown said...

Amina

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW