Jeni za nguruwe zimeimarishwa kisayansi ili kuweza kusaidia kumaliza ukosefu wa viungo vya mwili katika upandikishaji , watafiti wa Marekani wamesema.
Wanasayansi walioondoa virusi ndani ya jeni za nguruwe 37 hatua ambayo imeondoa pingamizi kuu kupandikisha viungo vya nguruwe katika binaadamu.
Kundi hilo la watafiti wa eGenesis limekiri kuwa imekuwa changamoto kubwa kuweza kuzuia viungo vya nguruwe kukataliwa na mwili wa binadamu, Lakini wataalam wanasema kuwa hatua iliopigwa inafurahisha.
Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la sayansi ulifanya utafiti wa seli za ngozi za nguruwe.
Vipimo vilibaini kuna takriban virusi 25 aina ya Porcine vilivyojificha katika jeni ya nguruwe.
Jaribio la kuchanganya seli za nguruwe na zile za binaadamu pamoja lilibani kuwa virusi hivyo vinaweza kutoroka na kusababisha maambukizi katika tishu za binaadamu.
Lakini watafiti hao baadaye walitumia teknolojia ya kubadilisha jeni ili kuviondoa virusi hivyo.
Walibidi watumie teknolojia ya kusambaza sawia na iliotumika kumtengeza kondoo wa Dolly ambapo jeni zinatolewa katika seli na kuwekwa katika yai la nguruwe ili kutengeza kiini tete.
Mpango huo hauwezi kuzalisha matokeo sahihi ,lakini nguruwe 37 walio na afya nzuri wamezaliwa.
Hao ndio nguruwe wa kwanza ambao hawana virusi , Dkt Uhan Yang, mmoja ya watafiti hao kutoka chuo kikuu cha Havard na kundi hilo la eGenesis waliambia BBC.
Wao ndio nguruwe walioimarishwa kijeni kulingana na idadi ya wanyama waliomarishwa jeni.
Iwapo upandikishaji wa kutumia viungo vya viumbe wengine utafanikiwa basi hatua hiyo itakabiliana na ukosefu wa viungo vya upandikishaji miongoni mwa binadamu.
Zaidi ya watu 100,00 wanahitaji viungo vya upandikishaji nchini Marekani pekee.
Kuna takriban watu 6,500 nchini Uingereza wanaosubiri viungo .
Dkt Yang aliambia BBC: Tunatambua tuko katika hatua za kwanza za utafiti na maendeleo.
''Tunajua tuna maono ya ulimwengu ulio na ukosefu mkubwa wa viungo, hiyo ni changamoto kubwa, lakini pia ni lengo letu kupunguza vizuizi vilivyopo.
Nguruwe wana mafanikio katika upandikishaji wa viungo vya viumbe tofauti kwa kuwa ukubwa wake ni sawa na ule wa binadamu mbali na kwamba wanyama hao wanaweza kufugwa kwa idadi kubwa.
Lakini kuondoa virusi hivyo ni nusu tu ya changamoto, kwa sababu hata viungo vilivyotolewa kutoka kwa watu wengine vinaweza kukataliwa na mwili vinavyowekwa.
Wanasayansi hao wa Marekani wanachunguza zaidi kuhusu uimarishwaji wa jeni ili kuweza kuvifanya viungo vya nguruwe kukubalika kwa urahisi na kinga ya binadamu.
Source: BBC
No comments:
Post a Comment