Tuesday, August 1, 2017

DHAMBI ZILIZOSABABISHA KIFO CHA MOHAMMAD (SEHEMU YA 2)

Image may contain: text

Huu ni mwendelezo wa sehemu ya kwanza. Hizi ni nukuu mbalimbali kutoka kwenye Hadith zinazoelezea kuhusu kilichosababisha kifo cha Mohammad.
Bukhari's Hadith 3.786:
Imesimuliwa na Anas bin Malik: mwanamke wa Kiyahudi alitia sumu nyama ya kondoo iliyopikwa na kumpa Mtume ambaye aliila. Kisha akaletwa kwa mtume na wakamuuliza, “tumuuwe?” Akasema, “Hapana.” Niliendelea kuona madhara ya sumu kwenye kaa la mdomo wa mtume wa Allah.
Kutoka kwa Ibn Sa'd ukurasa 249:
Hakika mwanamke wa Kiyahudi akaletea mtume wa Allah nyama (iliyotiwa sumu) ya mbuzi jike. Akakata kipande kudogo cha nyama, akaweka mdomoni na kutafuna na kisha kukitupa. Kisha akasema kwa wafuasi wake: “Subiri! Hakika paja lake linaniambia imetiwa sumu.” Kisha akaagiza huyo mwanamke aletwe mbele yake na kumuuliza, “nini kimekusukuma ufanye ulichofanya?” Nilitaka nidhibitishe kama kweli wewe ni mtume, na katika hiyo Allah atakuonya, kama wewe ni mtume wa oungo nitanusuru watu kwa kukuondoa kabisa.”
Kutoka kwa Ibn Sa'd kurasa 251, 252:
Bishir hakunyanyuka kutoka kwenye kiti chake, rangi ya ngozi yake ilibadilika ikawa ya kijani. Mtume wa Allah akaagiza Zeynab bint Al-Harith aletwe mbele yake na akamuuliza, “Nini kimekusukuma ufanye ulichokifanya?” Akajibu umewafanyia watu wangu ulichowafanyia, Umeua babangu, umeua mjombangu na mume wangu, hivyo nikasema, kama kweli wewe ni mtume huo mguu wa mbuzi utakujulisha kuwa nimekuwekea sumu, kama wewe ni mwongo nitakuangamiza niwanusuru watu wangu.”
Mtume wa Allah aliishi tu miaka mitatu kutokana na maumivu na madhara ya ile sumu kisha akaaga dunia. Katika kuugua kwake alikuwa anasema, “Nilishinda nikihisi madhara ya kile kipande cha nyama nilichokula kule Khaibar na niliugua mara nyingi kutokana na maumivu mengi. Lakini sasa nahisi wakati umefika wa kukata mshipa mkuu wa moyo wangu.”
Ibn Sa'd ,Ukurasa 250:
Mwanamke wa Kiyahudi wa Khaibar akampa mtume wa Allah nyama ya mbuzi iliyowekwa sumu. Kisha akatambua kuwa ilikuwa imetiwa sumu, akaamuru aletwe mbele yake na kumuuliza, “nini kilichokusukuma ufanye ulichofanya?” akasema, “Nilitaka nidhibitishe kuwa kama wewe ni mtume wa kweli, Mungu atakuonya, na kama wewe ni mnafiki, nitanusuru watu kutokana na maovu yako.” Mtume wa Allah alipoumwa alitolewa damu kwa kuchomwachomwa ngozi yake.
Tabari Juzuu 8, Ukuras 124:
Mtume wa Allah, akiwa kitandani akiumwa kutokana na ugonjwa wake ambao alikufa kutokana nao – mamake Bishr alikuwa amekuja kumjulia hali – “Umm Bishir, wakati huu ninahisi ni kama mshipa mkuu wa moyo wangu unadhuriwa sana kutokana na chakula nilichokula na kijana wako kule Khaibar.”
TATHMINI:
Mohammad alivamia, kupigana, kuua, kuiba bidhaa, kuangamiza, kufanya mateka Wayahudi wa Khaibar. Wayahudi hawakuwa na nia ya kupigana na genge lake. Mwanamke wa Kiyahudi, Zeynab bint Al-Harith ambaye familia yake iliangamia kutokana na vita vya kikatili vya Mohammad, aliamua kutia sumu kwenye nyama ya mbuzi iliyochomwa na kumpa Mohammad na Waislamu wenzake. Mohammad alikula kipande cha mnofu wa mbuzi na kuanza kuhisi madhara yake. Alikufa baada ya miaka mitatu kutokana na hiyo sumu.
***SEHEMU YA TATU ITATOA UCHAMBUZI, MASWALI NA TATHMINI YA MOHAMMAD NA VITA VYA KHAIBA NA UHALALI WA UTUME WAKE***

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW