Thursday, July 27, 2017

UTHIBITISHO KWAMBA MUNGU YUPO (SEHEMU YA NNE)

Image may contain: one or more people and text


Ulimwengu ni sanaa iliyobuniwa. Tupia macho nyota za angani au maua ya kondeni. Ni nini mbele yako? Si uzuri huo? Aidhaa uzuri huo umebuniwa na mbuni aliyejipanga au umeibuliwa na mlipuko usiokusudiwa (wanafizikia wauita, “big bang”).
Lakini, iweje mlipuko usiopangilika uzue maumbile yaliyopangilika? Waweza kuamini herufi hizi usoni mwako ni matokeo ya wino uliojimwagikia badala ya binadamu aliyefikiria? Daima, sanaa hubuniwa na kubakia mali halali ya msanii. Kufurahia uvumbuzi na kutomtambua mvumbuzi ni nini kama si ubakaji wa sanaa, ukatili kwa msanii, na ukiukwaji wa haki ya msanii kutambulika? “Kwa sababu mambo yake [Mungu]….yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru” (Warumi 1:20;)
UNABII KUHUSU BABELI
Katika enzi ya manabii wa Israeli (Kama 850-560 K.K) kuliinukia dola mbili kuu katika maeneo yanayoizunguka mito ya Frati na Tigrisi, katika Iraki ya sasa.
Ya kwanza ilikuwa dola ya Ashuru iliyokuwa na makao makuu Ninawi. Kwa karne mbili, Waashuru walivamia ardhi ya mataifa waliowazunguka: kusini wakawatawala Wakaldayo na makao makuu yake Babeli; Magharibi wakaikalia Shamu, na kuendelea chini katika pwani ya Bahari ya Kati, kupitia Israeli mpaka Misri. Sera yao ilikuwa ya kigaidi. Lengo lao lilikuwa kuwatisha wakazi wa maeneo hayo watii na kulipa kodi kwa mwaka. Kufanikisha hili waliiswaga miji kiuporaji na kuichoma moto, wakavibamiza vijiji, na kuua wakazi na kuchukua maelfu ya mateka Ashuru.
Katika nusu ya pili ya karne ya saba (K.K), nguvu ya Ashuru ilipungua na Babeli ikaanza kupanda. Katika mwaka 612 (K.K), Ninawi uliangushwa.
Nebukadreza, mfalme wa Wakaldayo, haraka akaanzisha dola mpya. Mataifa madogo madogo Mashariki ya Kati yalipokuwa yanashangilia uhuru wao kutoka Ashuru, mara yakajikuta wakivamiwa na majeshi ya Babeli. Na hasa Nebukadreza akaivamia Israeli akaiteka Yerusalemu, akalichoma hekalu lake na kuchukua maelfu ya mateka Babeli. Akaendelea kusini zaidi na kuivamia Misri.
Dola ya Babeli ilikuwa ni awamu ya pili ya utawala huu wa kijeshi. Ulikuwa katika eneo la Frati.Na hasa Nebukadreza, mfalme wake mkuu kabisa aliujenga mji mkuu wa Babeli kuwa fahari ya dunia katika Mashariki ya Karibu. Alijenga Mahekalu makubwa na majumba ya kifalme, na kuzungushia jiji hilo ukuta mkubwa sana kuulinda. Babeli ukawa utukufu na fahari kuu kwa Nebukadreza mwenyewe na Wakaldayo wake.
Ni vigumu kwetu sisi kwa sasa kutambua athari za utawala kama huo wa kimabavu na uharibifu wa mali kwa wakazi wa mataifa madogo. Kwao dola za Ashuru na Babeli zitakuwa zilionekana tishio na zisizoshindwa.
=== USIKOSE SEHEMU YA TANO ========= MAANGUKO KAMILI
La ajabu, miaka 100 kabla Babeli haijafikia kilele cha ukuu wake, nabii Isaya alishatabiria kuangushwa kwake kwa maneno thabiti sana.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW