Friday, July 14, 2017

KWANINI TUNAKULA NGURUWE? (SEHEMU YA KWANZA)

Image may contain: one or more people and text


Kwa taarifa yako Allah ameruhusu kula Nguruwe.
* Mafundisho ya Quran Kuhusu Nyama ya Nguruwe;
Pamoja na kuwa waislamu wanatushutumu sana wakristo kuwa tunakula Nguruwe Quran inajikanganya sana katika swala zima la kuliwa ama kutokuliwa kwa mnyama huyu ni muhimu kuangalia, kwa ufupi hakuna aya maalumu katika Quran inayoharimisha na kukataza kula Nguruwe.
Quran inasemaje kuhusu nyama ya nguruwe;-
Quran inaeleza wazi kuwa Mungu aliharimisha Vitu vizuri (akiwemo Nguruwe) kwa Wayahudi kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao, yaani Mwenyezi Mungu aliwakataza kula nyama hii kama sehemu ya kuwahukumu Wayahudi na si vinginevyo soma (Surat an-nisaa 4;160).
Quran inasema hivi katika aya hiyo “Basi kwa dhulma yao hao Mayahudi tuliwaharimisha vitu vizuri walivyohalalishiwa na vilevile kwa sababu ya kuzuiliwa kwao watu wengi na njia ya mwenyezi Mungu”
ni aya iliyo wazi kuwa wayahudi walizuiliwa vitu vizuri kwaajili ya dhuluma Mungu alitaka kuwahukumu kwa kuwanyima baadhi ya vitu vizuri Quran inakiri wazi kuwa Nguruwe ni kitu kizuri Umeona?
Quran inafundisha kuwa Yesu alikuja kuhalalisha yale yaliyo harimishwa (Surat al-Imran 3;50).
Quran inasema haya katika aya hii “ Na nitakuwa Msadikishaji way ale yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati na nimekuja ili NIKUHALALISHIENI yale MLIYOHARIMISHWA na nimekujieni na hoja Kutoka kwa Mola wenu kwa hiyo mcheni mwenyezi Mungu na NITIINI”
Hayo ni meneno ya Yesu Ndani ya Quran ikionyesha wazi kuwa Yesu alikuja kuhalalisha yale yaliyoharimishwa katika Tourati na anatuamuru kumtii, ni wazi kuwa Yesu ameruhusu kula Nguruwe na Quran pia
Quran imehalalisha kula vilivyo vizuri walavyo waliopewa kitabu (Al-maida 5;3-5).
Sura hii almaida maana yake maswala ya meza inasema hivi “……..Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha wale waliopewa Kitabu ni Halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao…”
Hii ni aya iliyo wazi inayoruhusu kila muislamu kula vyakula vya wakristo na wayahudi na sisi kula vyao umeona!
Quran ina kigugumizi kwa vile hakuna katazo la moja kwa moja kuhusu kutokula Nguruwe yaani inakataza kula Nguruwe na wakati huohuo inaruhusu endapo utashurutishwa na njaa (Al-baqara 2;173) au kama una dharula waweza kula hapa ndipo quran inapojikanganya ni muhimu kujiuliza imekataza au imeruhusu? Na dharula hii ni ipi? Quran inajibu kuwa dharula hii ni njaa (Al-an nam 6;145)Quran inasema kula bila kupita kiasi hili ni jema kwani Biblia inafundisha kuwa hata kama una njaa kiasi gani kula kupita kiasi hata kama si nguruwe chakula chochote ni ulafi ni dhambi (Galatia5;21)
Quran inafundisha kuwa Mungu hakuharimisha chochote ila wazee wa kiyahudi waliharimisha kwa mapokeo yao tu (Al-an nam 146).
Quran inatahadharisha kuwa makini kumzulia Mungu uongo kuwa ameharimisha kitu kumbe hakuharimisha chochote (An Nahl 16;116).
Quran inaamuru uletwe Ushahidi kuwa ni wapi Mungu ameharimisha wanyama? Soma (Al an- am 6;150).
Hivyo ukisoma kwa makini Quran utaona hakuna kilicho haramu ndugu zangu waislamu kula nguruwe ni ruksa ila kiasi tu usizidishe ndivyo Quran inavyofundisha kama husadiki pale uwanja wa sabsaba Tanga kwa Minchi waislamu wenzenu hujumuika kula kiti moto kila iitwapo leo kwani wameelimika na wamegundua siri hii. Mimi sikushawishi ila nina kuweka huru kama mwalimu wa kweli ya Mungu “….. Mtaifahamu kweli nayo kweli itawaweka huru.
Mafundisho ya Agano jipya kuhusu vyakula (Nguruwe).
Biblia inasema mafundisho yoyote yanayokataza mtu kula vitu Fulani ni mafundisho ya Mashetani (1Timoth 4;1-5). Ndio maana waganga wa kienyeji mtu anapokwenda kuaguliwa hukatazwa kula baadhi ya vitu Mungu sio Mganga wa kienyeji. Na wanaomwamini hawana sheria ya kuwazuia nini cha kula au kutokula.
Biblia inasema hakuna kitu najisi kwa mtu asiye najisi lakini kitu Fulani ni najisi kwake yeye aliye najisi (Rumi14;14)Biblia inafundisha kuwa kula au kutokula hakuongezi utakatifu wala hakuzuii tamaa za mwili (Kolosai 2;16-23) hivyo hatupaswi kujitia katika mambo ya kutunga tu ya mtu,au akilizake na maono ya wanao abudu malaika kumuabudu Mungu hakuji kwa kula au kutokula aina fulani ya vyakula bali katika moyo safi (Math 5;8).
Biblia inafundisha kuwa unajisi wa mtu hautoki nje bali ndani ya mtu pia Yesu alitakasa vyakula vyoote (Marko 7;14-16,17-19)
Paulo mtume alifundisha kuwa chakula ni kwa tumbo tu na si mambo ya rohoni.
(1Koritho 6;13). Hoja ya Pepo waliotolewa na Yesu kuwaingia nguruwe je ina maana gani?
USIKOSE SEHEMU YA PILI........
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Shalom.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW