Thursday, May 4, 2017

USITAZAME NYUMA KAMA MKE WA LUTU

Image may contain: one or more people and text
Lutu (kwa Kiebrania לוט - [lōṭ]; kwa Kiarabu لوط - [lūṭ]) alikuwa mtoto wa Haran, mdogo wa Abrahamu kadiri ya Biblia, ambaye alimfuata kutoka Mesopotamia hadi Kanaani.
Lutu akaitazama nchi. Akaona sehemu ya nchi iliyo nzuri sana yenye maji na majani mazuri mengi ya wanyama wake. Hiyo ilikuwa Wilaya ya Yordani. Basi Lutu alipeleka jamaa yake na wanyama huko. Mwishowe wakakaa katika mji wa Sodoma.
Watu wa Sodoma walikuwa wabaya sana. Lutu alisumbuliwa, maana alikuwa mtu mzuri. Hata Mungu alisumbuliwa. Mwishowe, Mungu alituma malaika wawili wakamwonye Lutu kwamba Mungu ataharibu Sodoma, na Gomora mji wa karibu, maana ni miji mibaya.
Malaika hao wakamwambia Lutu hivi: ‘Fanya haraka! Chukua mke wako na binti zako wawili mwondoke huku!’ Malaika mmoja alisema: ‘Kimbieni mponye uhai wenu! Msitazame nyuma. Kimbieni kwenye milima msiuawe.’
Lutu na binti zake walitii, wakatoka Sodoma. Lakini mke wa Lutu hakutii. Walipokwisha kutembea mwendo fulani kutoka Sodoma, mke alisimama akatazama nyuma, akawa nguzo ya chumvi.
Tunaweza kujifunza somo zuri kwa hayo. Yanatuonyesha kwamba Mungu anaokoa wale wanaomtii, lakini wale wasiomtii watapoteza uhai wao.
Mwanzo 13:5-13; 18:20-33; 19:1-29; Luka 17:28-32; 2 Petro 2:6-8.
Tafakari yetu inatutadharisha na matendo yetu ya kuangalia Nyuma; Tumeagizwa tuangalie mbele ili tuweze kufuzu kuingia katika nyumba ya Mungu; lakini kwa kuangalia nyuma kama mke wa Lutu tunakuwa tumejiondoa wenyewe katika kushiriki utukufu wa Mungu; tukisoma Luka 9: 61-62 Mtu mwingine pia akamwambia, Bwana, nitakufuata; lakini, nipe ruhusa kwanza nikawaage watu wa nyumbani mwangu.
Yesu akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu. Hatutakiwi kabisa kuangalia nyuma tunapoutafuta ufalme wa Mungu;
Kuangalia nyuma hapa maana yake ni nini?
Tunayaangalia maisha yale ya zamani, ya ulevi, uzinzi, uwongo, wizi, chuki, na kadhalika; tukumbuke kuwa hakuna maisha ya baadae bila mipango hiyo kupokea maelekezo ya
Mungu ndani ya Mioyo yetu. Agizo ambalo tunapata leo hatutakiwi kugeuka nyuma na kuyarudia maisha yaliyojaa dhambi. Tumepata Baraka ya kukombolewa na damu ya Yesu jukumu letu sasa ni kusonga mbele na kamwe kuto geuka Nyuma.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW