Saturday, May 13, 2017

MANABII WA KIKE WA BIBLIA

No automatic alt text available.


Je, unawajua kwa majina Manabii wa Kike wa kwenye Biblia?
Je, Biblia inaruhusu kuwa na Manabii wa Kike?
Yoeli 2: 28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;
Nukuu zaidi soma 1 Wakoritho 11:5, Matendo 2:17-18, Matendo 21:9, Phl 4:3,
Baada ya kusoma hiyo aya, swali linafuata, nionyeshe Nabii wa Kike kwenye Biblia? Hili ni swali nililo ulizwa na Muislam. Bila ya kupoteza muda naweka uthibitisho wa aya.
NABII MIRIAM, DADA YA HARUNI NA MUSA:
Miriam = Soma Kutoka 15 aya 20. Naye Miriamu nabii, dada ya Haruni, akachukua tari mkononi mwake; na wanawake wote wakaanza kutoka pamoja naye wakiwa na matari na kucheza dansi
NABII DEBORA, MKE WA LAPIDOTHI:
Debora = Soma Waamuzi 4:4-5 Basi Debora, nabii wa kike, mke wa Lapidothi, ndiye aliyekuwa akihukumu Israeli wakati huo.
NABII HULDA, MKE WAS SHALUMU:
Hulda = Soma 2 Wafalme 22 na 2 Mambo ya Nyakati 34:22 Kwa hiyo Hilkia pamoja na wale wengine mfalme aliowatuma 34:22 Kiebrania hakina aliowatuma. walimwendea nabii Hulda, mkewe Shalumu, mwana wa Tokathi, mwana wa Hasra, mtunza mavazi yaliyotumika hekaluni (alikuwa anaishi Yerusalemu katika mtaa wa pili); nao walizungumza naye juu ya mambo yaliyotokea.
NABII ANNA BINTI YA FANUELI:
Anna = Soma Luka 2: 36 Basi kulikuwako Nabii Anna, binti ya Fanueli, wa kabila la Asheri (mwanamke huyu alikuwa amesonga sana katika miaka, na alikuwa ameishi pamoja na mume kwa miaka saba kutoka ubikira wake,
MKE WA NABII ISAYA:
Mke wa Isaya soma Isaya 8:3. Ndipo nikamkaribia yule nabii wa kike, naye akapata mimba na baada ya muda akazaa mwana. Mungu sasa akaniambia: “Mwite jina lake Maher-shalal-hash-bazi,
MABINTI WATATU WA FILIPO:
Na Mabinti Watatu wa Filipo Soma Matendo 21.8 Kesho yake tuliondoka tukaenda Kaisarea. Huko Kaisarea tulikwenda nyumbani kwa mhubiri Filipo. Yeye alikuwa mmoja wa wale saba waliochaguliwa kule Yerusalemu. 9 Alikuwa na binti watatu ambao walikuwa na kipaji cha unabii.
Leo tumejikumbusha kuhusu Mnabii wa Kike wa Biblia. Watu wengi hii leo wanapiunga Kipaji hiki cha Unabii kwa Wanawake, lakini Biblia inatuthibitishia kuwa Wnanawake wana haki sawa na Wanaume mble ya Mungu weu.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW