Tuesday, May 9, 2017

BIBLIA YATHIBITISHA KUWA YESU NI MUNGU

Image may contain: text
USHAIDI
Isaya 9: 6
Kwa maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume, nao utawala utakuwa mabegani mwake.
Naye ataitwa: Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.
Huu ni ushaidi unatufahamisha kuwa Yesu atazaliwa na ataitwa Mungu mwenye Nguvu.
Katika Agano Jipya, kuna ushaidi ambao unakiri Umungu wa Yesu Kristo.
USHAIDI
Hebu tusome Wafilipi 2: 5-11
5 Tuweni na nia ile ile aliyokuwa nayo Kristo Yesu.
6 Yeye ingawa alikuwa sawa na Mungu, hakuona kule kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho,
7 bali alijifanya si kitu, akajifanya sawa na mtumwa, akazaliwa katika umbo la mwanadamu.
8 Naye akiwa na umbo la mwanadamu, alijinyenyekeza hata mauti, naam, mauti ya msalaba!
9 Kwa hiyo, Mungu alimtukuza sana na kumpa Jina lililo kuu kuliko kila jina,
 10 ili kwa Jina la Yesu, kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, vya duniani na vya chini ya nchi
11 na kila ulimi ukiri ya kwamba YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu comment Baba.
NENO la "Kuwa sawa na Mungu" kwa Kigiriki ni MORPHE-: Ikimanaisha Yesu alikuwa na adhama zote za Kimungu na Mungu. (God's attributes)
Hivyo basi katika ushaidi huu wa katika kitabu cha Wafilipi tunasoma kuwa Yesu hakuwa mtu wa kawaida bali alikuwa ni Mungu pamoja nasi yaani Imanueli.
USHAIDI
WAEBRANIA 1:
Mwana Ni Mkuu Kuliko Malaika
1 Zamani Mungu alisema na baba zetu kwa njia ya manabii mara nyingi na kwa njia mbalimbali, 2 lakini katika siku hizi za mwisho amesema nasi kwa njia ya Mwanawe, ambaye amemweka kuwa mrithi wa vitu vyote, ambaye kwa Yeye aliuumba ulimwengu. 3 Mwana ni mng'ao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi Yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno Lake lenye uweza. Akiisha kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko mbinguni.
NENO: Mfano halisi wa nafsi yake. Katika Kigiriki linamaanisha "CHARAKTER" this is not merely similarity of being, but qualitative identity.
KATIKA aya ya 8 inasema:
Lakini kwa habari za Mwana asema, "Kiti chako cha enzi, Ee Mungu, kitadumu milele na milele, nayo haki itakuwa fimbo ya utawala ya Ufalme Wako.
Hpa tunaona Mungu anamuita Mtoto wake Mungu. Ushaidi huu upo vile vile katika Zaburi 45 aya 6.
Ndugu wasomaji, ushaidi wa Umungu wa Yesu umejaa kwenye Biblia na katika Maagano yote Mawili.
USHAIDI
LUKA 19: 10
Yesu anasema yeye ni MWOKOZI: Kazi ambayo ni ya Mungu Pekee.
Luka 19: 10Kwa maana Mwana wa Adamu amekuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea." Ambayo inalingana na Ezekiel 34:16, 22.
Hapa tusoma kuwa Yesu anasema kuwa yeye ni Mkombozi na amekuja kutafuta walio potea, Madai haya yanamfanya Yesu kuwa ndie MOJA: MKOMBOZI. MBILI: MUUMBA WA WATU.
USHAIDI
MATAYO 26:63-65 Inasema
" 63Lakini Yesu alikuwa kimya. Ndipo Kuhani Mkuu akamwambia, "Nakuapisha mbele za Mungu aliye hai, tuambie ikiwa wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu."
64 Yesu akajibu, "Wewe umenena. Lakini ninawaambia nyote, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mungu Mwenye Nguvu na akija juu ya mawingu ya mbinguni.'' 65 Ndipo Kuhani Mkuu akararua nguo zake na kusema, "Amekufuru! Kwa nini tunahitaji ushahidi zaidi? Tazama, sasa ninyi mmesikia hayo makufuru. 66 Uamuzi wenu ni nini?" Wakajibu, ''Anastahili kufa "
JIBU la Yesu ukilikiliza unaweza kufikiri kuwa Yesu hakukubali kuwa YEYE NI Mungu. Lakini THE REACTION ya Kuhani Mkuu na Mafarisayo na wengine walio kuwepo pale inaonyesha wao walimuelewa kivingine. Biblia inasema Kuhani Mkuu akararua nguo zake.!!! AKASEMA: Yesu amekufuru mbele yetu, kwanini tutafute ushaidi zaidi ya huu?
Kama hii hukumu ya kudai kuwa Yesu amekufuru, basi Yesu hapa alikuwa na nafasi nzuri ya kupinga madai ya huyu Kuhani Mkuu na wengine walio kuwa pale. Lakini Yesu alikubali hii charge ya kujiita yeye Mungu kama Alivyo sema Kuhani Mkuu.
Barikiwa sana.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW