Mtu Mmoja Alileta Kesi Kwa Yesu Akihitaji Msaada Juu Ya Tatizo La Ugonjwa Wa Kifafa Lililokuwa Linamtesa Mwanae Tangu Utoto Wake, Na Alikuja Na Kauli Za “HURUMA HURUMA” Naye Alimwambia BWANA Yesu, “Ukiweza Neno Lolote, Utuhurumie Na Utusaidie” (Marko 9:22)
Na Yesu Hakuanza Kumwambia Maneno Yaliyojaa AKILI ZA KIBINADAMU NA THEOLOJIA Bali Alizungumza Kwa UHAKIKA, Tena Kwa Mshangao, “Ukiweza! YOTE Yawezekana Kwake Aaminiye” (Marko 9:23)
Yesu Alikuwa Anamaanisha, “HAKUNA JAMBO LOLOTE AMBALO MTU WA IMANI HAWEZI KUFANYA; YOTE YANAWEZEKANA KWAKE AAMINIYE”
Mathayo 19: 26 Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.
Yeremia 32:27 '' Tazama, mimi ni BWANA, MUNGU wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza? ''
Mpendwa, labda umejaribu kufanya yote kwa kutumia uwezo wako, lakini mambo bado hayakai vizuri. Labda umepoteza kazi na madeni yanakuzidi kila siku. Leo ningependa kukukumbusha kuwa, Yesu Kristo tunae mwanini ni MWEZA WA YOTE. Hakika hakuna jambo asilo liweza na hakuna jambo ambalo hakulimaliza pale Msalabani. AMINI NA YOTE YANAWEZEKANA. USIKATE TAMAA MAANA BARAKA ZAKO ZIPO MLANGONI NA ZINAKUSUBIRI.
AMINI NA YOTE YANAWEZEKANA.
Shalom,
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment