Monday, April 10, 2017

UNAWAFAHAMU MALAIKA WAKUU SABA WA MUNGU "ARCHANGELS OF GOD? (SEHEMU YA SABA)


Kiumbe wa roho anayeitwa Mikaeli hatajwi mara nyingi katika Biblia. Hata hivyo, kila mara anatajwa akitenda jambo fulani. Katika kitabu cha Danieli, Mikaeli anapigana na malaika waovu; katika barua ya Yuda, anabishana na Shetani; na katika Ufunuo, anapigana na Ibilisi na malaika wake waovu. Anapoutetea utawala wa Mungu na kupigana na adui za Mungu, Mikaeli anatenda kupatana na maana ya jina lake—“Ni Nani Aliye Kama Mungu?” Lakini Mikaeli ni nani?

Malaika Mikaeli (kwa Kiebrania מִיכָאֵל, Micha'el au Mîkhā'ēl, maana yake Nani kama Mungu; kwa Kigiriki Μιχαήλ, Mikhaḗl; kwa Kiarabu ميخائيل, Mīkhā'īl) anaheshimiwa kama malaika mkuu katika imani ya dini za Uyahudi na Ukristo.

Mikaeli ni malaika mkuu, neno “malaika mkuu” la kigiriki ni ἀρχάγγελος (archaggelos) linalomaanisha “mtawala wa malaika” au “mkuu wa malaika”; kwa uhalisia “mkuu wa wajumbe”.
Katika Biblia ya Kiebrania anatajwa mara tatu katika Kitabu cha Danieli.

Katika Agano Jipya la Biblia ya Kikristo anatajwa katika Waraka wa Yuda na katika Kitabu cha Ufunuo.

Je Malaika wa Bwana anaweza kuwa ndiye malaika mkuu Mikaeli?

Zekaria 3:1-2 inasema, “Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye. Bwana akamwambia Shetani, Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni?”

Hapa tunamwona malaika wa Bwana akimwambia shetani kwamba”Bwana na akukemee”, Ukisoma fungu la 3 utaona Yoshua alikuwa amevaa “mavazi machafu” hii inawakilisha dhambi. Halafu shetani akaja kwa Yoshua akidai kuwa yuko upande wake, na malaika wa Bwana hivyo hivyo, alikuja kumuondolea Yoshua uovu wake, hivyo akamwambia shetani kwamba Bwana na akukemee. Je ni wapi tena tunaona jambo kama hili hili?

Yuda 1:9 inasema, “Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.”

Hapa tunaona kama hilo hilo lilitoke wakati wa Musa, na malaika aliyefanya hivyo ni Mikaeli malaika mkuu; kwa hakika “malaika wa Bwana” ndiye “Mikaeli”.

Danieli 12:1,2 inasema, “Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako;…na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.”

Zingatia Danieli 12:1 inamwita Mikaeli kama “Jemedari Mkuu”, na katika Ufunuo 12:7 “Mikaeli na Malaika zake anapigana na shetani na malaika zake”. Shetani ni mkuu wa malaika zake na malaika zake humwabudu yeye na kutii amri zake; na malaika zake ni jeshi lake, vivyo hivyo Mikaeli ni mkuu wa malaika zake, na malaika zake ni jeshi lake, nao hutii amri zake (Ebrania 1:6-7

Yohana 5:28,29 “Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.”

Ufunuo 12:7 Na vita vikatokea ghafula mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka mkubwa, naye joka mkubwa na malaika zake wakapigana.

Sehemu zote tumeona Mikaeli ni malaika mkuu wa vita. Ukiona mambo hujayapata kama inavyotakiwa maana yake yupo azuiaye mahali amejificha hivyo fanya vita vya kiroho na utafanikiwa kwajina la Yesu.

Yupo saizi ya ibilisi ambaye anaitwa Malaika Mikaeli. Shetani alikuwa malaika lakini alimwasi Mungu na Mikaeli ndiye aliyemshughulikia.

Ukiona mambo kwenye maisha yako yameshindikana usifikiri Mungu hajakusikia maombi yako na amekuacha, kuna kizuizi cha mkuu wa anga mahali ambaye amekuzuia na huyo lazima ashughulikiwe na yale majibu yako yaje kwako kwa jina la Yesu.

Yupo malaika Mikaeli mkuu wa majeshi ya malaika ambaye tunamtumia ili tupigane na huyu mkuu wa anga na wakala zake waliozuia baraka zetu kwa jina la Yesu. Mashetani wote waliojificha kwenye ulimwengu wa rohoni lazima tuwafuate na kuwateketeza kwa jina la Yesu.

Malaika Mikaeli ni kiumbe wa Rohoni na wale waliokuzuia nao ni viumbe wa Rohoni na hakuna jambo gumu la kumshinda Mungu wetu. Mikaeli anajua mbinu za vita na leo tunaungana na majeshi ya malaika Mikaeli ili kupigana na mkuu wa anga la uajemi na mapepo yake.

USIKOSE SEHEMU YA NANE. MALAIKA URIEL NA KAZI ZAKE.......


Shalom,

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW