Friday, April 7, 2017

UNAWAFAHAMU MALAIKA WAKUU SABA WA MUNGU "ARCHANGELS OF GOD? (SEHEMU YA TANO)

Image may contain: text
Kabla ya kuendelea na somo letu, na kuzungumza kuhusu MALAIKA MICHAEL, hebu tujikumbushe kidogo kuhusu Malaika katika Agano la Kale.
MALAIKA KATIKA AGANO LA KALE WALIFANYA NINI?
Mjumbe muhimu anayetumwa na Mungu anayeitwa “Malaika wa Bwana”, au “Malaika wa Mungu” katika Biblia za Kingereza. Majina haya yenye vyeo hivi huitwa Malaika Maalumu (au wajumbe) ambao wanamwakilisha Mungu.
Wakati malaika wa Yehova alikuwa pamoja nao, ilimaanisha ya kwamba Mungu alikuwa yuko pia pamoja nao. Malaika alisema na kutenda kwa niaba ya Mungu Mmoja wa kweli.
Malaika wa Yehova ambaye mara kwa mara alishughulika na wanadamu, alimwakilisha Mungu wa kweli ambaye Waisraeli walimwabudu.
Hebu tuangalie matukio mengine mengi, ambayo Malaika huyu, alionekana na kuzungumza na wanadamu katika nyakati za zamani.
• Malaika alizungumza na Hajiri mara mbili (Mwanzo 16:7-13; 21:17-18)
• Malaika alizungumza na Ibrahim (Mwanzo 12:1-3; 22:11-18).
• Malaika alizungumza na Yakobo katika ndoto (Mwa. 28:11-21; na 31:11-13; Angalia pia Mwa. 32:24-30).
• Malaika alimtokea na kuzungumza na Musa (Kutoka 3:1-6; 24:12-16).
• Malaika katika mawingu (Kutoka. 13:21; 14:24)
• Malaika akiwa kama mhifadhi, Mlinzi na Mwokoaji (Zaburi 34:7; 35:5-6).

Mtume Paulo alisema ndiye aliyewavusha wana wa Israel katika bahari (1 Korintho 10:1-4). Paulo pia anamtambulisaha Malaika wa Mungu katika Wagalatia 4:14.

Matukio mengine ambayo Malaika aliwatokea Wanadamu;
• Baalamu na Malaika (Hesabu 22:22-35)
• Yoshua na Malaika (Yos. 5:15)
• Gidioni na Malaika (Amu. 6:12-24)
• Wazazi wa Samsoni na Malaika (Amu. 13:2-20)
• Daudi na Malaika (2 Samuel 24:16-17)
• Eliya na Malaika (1 Falme 19:5-12 na 2 Falme 1:15)
• Malaika na Daniel (Daniel 3:24-25, 28)
• Malaika na Zekaria (Zekiel 1:9,13-14,18-21; 2:3; 4:1,4-5; 5:5,10)
USIKOSE SEHEMU YA SITA. MAKERUBI NA MASERAFI NA KAZI ZOA...
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

WHAT DOES IT MEAN "THE WORD OF GOD IS GOD"?

 WHAT DOES IT MEAN "THE WORD OF GOD IS GOD"? Dr. Maxwell Shimba explains: The Word and the Divine Nature – A Comprehensive Exposit...

TRENDING NOW