Saturday, April 15, 2017

NI MANENO GANI YALIANDIKWA KWENYE ANWANI JUU YA KICHWA CHA YESU PALE MSALABANI?


Image may contain: text
Kwenye Mathayo 27:37; Marko 15:26; Luka 23:38 na Yohana 19:19, ni maneno gani hasa yaliyoandikwa kwenye anwani juu ya kichwa cha Yesu?
Kwanza tuangalie mambo matano yanayohusiana na jibu, na kisha majibu mawili.
1. Kwanza kabisa hapakuwa na ujumbe mmoja, lakini kulikuwa na jumbe tatu, kama Yohana 19:29 inavyosema, anwani iliandikwa Kiaramu, Kilatini na Kigiriki.
2. Hivi ndivyo waandishi wa injili wanavyo ripoti:
Mathayo 27:37 inasema, "Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi."
Marko 15:26, "Mfalme wa Wayahudi."
Luka 23:38, "Huyu ndiye Mfalme wa Wayahudi."
Yohana 19:19, "Yesu Mnazareti, Mfalme wa Wayahudi."
3. Waandishi wa kale walikuwa na kawaida ya kufafanua maneno badala ya kunukuu. Ripoti Tulizo nazo hapa ni sahihi, lakini hazina maelezo ya kina. Hivyo, kwa mfano, kama mwandishi mmoja alisema "Huyu ndiye Yesu, Mfalme wa Wayahudi", na mwingine alisema "Mfalme wa Wayahudi", wote wanaweza kuwa wanaripoti maneno yale yale. Mwandishi wa kwanza anaripoti maneno zaidi kuliko yule wa pili.
4. Papias, mwanafunzi wa Mtume Yohana, anaripoti kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa kwanza kwa lugha ya Kiebrania (au Kiaramu?) na kisha ikatafsiriwa kwenye Kigiriki. Waandishi wengine waliandiki Kigiriki. Hivyo, kuna tafsiri kati ya maneno yaliyosemwa na yale yaliyoandikwa na waandishi wa Injili.
5. Bila kujali tofauti zilizopo kati ya anwani hizi tatu, Marko anaelekea kuripoti maneno yaliyopo kwa waandishi wote watatu.
Jibu la Kwanza: Jumbe hizi tatu kwenye lugha tatu tofauti zimeripotiwa kwenye Mathayo, Luka, na Yohana. Marko anaripoti maneno yaliyomo kwa waandishi wote watatu. Pilato huenda hakujua Kiaramu kwa hiyo ujumbe ungeweza kuandikwa kwa Kilatini, na kutafsriwa kwenye Kigiriki na Kiaramu ili kila mtu aweze kuusoma.
Jibu la Pili: Kwa kuwa waandishi wa injili waliripoti maneno yaliyokuwa yametafsiriwa, na mambo kama "Hii ni" yalitokea mara kwa mara kwenye tafsiri, tuna uhakika na ujumbe wa anwani, lakini hatuna uhakika na maneno halisi. Hata hivyo, kitu muhimu hapa ni ujumbe, siyo maneno halisi.
HAKIKA YESU NI MFALME WA WAFALME.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW