Tuesday, April 25, 2017

NABII YULE NI NANI?


Kwanza tuanze kwa kutafuta maana ya neno Nabii.
Neno nabii (kwa Kiebrania נביא nevì, kwa wingi נְבִיאִים nevi'ìm, kwa Kiarabu نبي) linatumika kumtajia binadamu anayesema kwa niaba ya Mungu, hasa kwa kusudi la kuelekeza wenzake wafuate imani na maadili sahihi.
Katika lugha nyingi, mtu huyo anaitwa kwa jina linalotokana na neno la Kigiriki προφήτης [prophētēs], maana yake "anayesema mbele", yaani hadharani (mbele ya wasikilizaji), au kabla ya (jambo kutokea).
Katika matumizi ya kawaida, neno hilo linatumika hasa kwa mtu ambaye anatabiri jambo, bila ya kujali asili ya maarifa yake.
KATIKA UYAHUDI:
Katika Tanakh (Biblia ya Kiebrania) tunakuta vitabu vingi vinavyojumlishwa katika jina "manabii", kuanzia Yoshua hadi Malaki. Katika Ukristo baadhi ya vitabu hivyo vinahesabiwa kuwa "vitabu vya historia", kumbe kile cha Danieli kinapangwa kati ya "manabii wakuu" pamoja na Isaya, Yeremia na Ezekieli, wakati Wayahudi wanacho kati ya "maandiko (mengine)".
KATIKA UKRISTO:
Ukristo unakubali manabii wote wa Agano la Kale, lakini upande wa Agano Jipya ni wachache wanaoitwa hivyo, kwa mfano Agabo anayetajwa katika Matendo ya Mitume.
Kwa jumla ni kwamba Wakristo wote wanahesabiwa kuwa manabii kutokana na wajibu wa kutangaza Neno la Mungu kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.
KATIKA UISLAM:
Katika Islam mtume Muhammad anapewa nafasi ya pekee kati ya manabii wengi waliotumwa kwa binadamu wa nyakati na mahali tofauti. Ndiye anayesadikiwa na Waislamu wengi kuwa nabii wa mwisho na wa kudumu ("mhuri wa manabii" - khātim al-nabiyyīn (Kurani, XXXIII:40).
Uislamu unakubali manabii wa Biblia pamoja na wengine wasiotajwa katika kitabu hicho, kama vile Mwarabu Salih.
KATIKA DINI NYINGINE:
Dini nyingine zinatokana na mafundisho ya mtu anayehesabiwa nabii, kama vile:
Zarathustra (Uajemi, 628 KK - 551 KK).
Mahavira (Vardhamana) (India, 599 KK - 527 KK).
Mani (Manes) (Uajemi, (216 - 277).
Bab (Siyyid Mírzá 'Alí-Muhammad) (Uajemi, 1819 - 1850).
Bahaullah (Mirza Hosaynali Nuri) (Uajemi, 1817 - 1892).
SASA baada ya kujifunza maana ya neno nabii na jinsi imani na dini zinavyo lielewa hilo neno nabii. Turudi kwenye mada yetu ya Nabii Yule.
Yohana 1: 19 Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani? 20 Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo. 21 Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La. 22 Basi wakamwambia, U nani? Tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako? 23 Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.
Kumbe Yohana si Nabii yule maana amesha kataa kwenye aya hapo juu kuwa yeye sie. Basi, ni nani huyu ambaye ni Nabii yule?
SASA TUANZE KUANGALIA NA KUJIBU SIFA TATU ZILIZO NDANI YA YOHANA 1:19-23.
Kwenye aya hizo kumetaja watu watatu nao ni:
(1) KRISTO
(2) ELIYA
(3) NABII YULE
(1) KRISTO:
Yohana 4:25 Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote. 26 Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye.
Kwenye Yohana 4:25 hapo juu tumesoma kuwa Yesu ndie Kristo. Hivyo basi, nnani ni Kristo kama alivyo ulizwa Yohana kwenye Yohana 1-19-23 tumesha mjua ni YESU KRISTO. Je, Nabii yule ni nani basi, Ni Eliya?
kabla hatujamwangalia na kumjua ni nani kwa mujibu wa maandiko, tuwatazame wale walioenda kumuuliza Yohana wao wenyewe Walitoka wapi?
Yohana 1:24 Nao wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa Mafarisayo. 25 Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule?
26 Yohana akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi. 27 NDIYE YULE ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake.
Wale watu walikuwa wametoka kwa Mafarisayo, wakawa wanamshangaa Yohana ni vipi abatize wakati yeye siyo Kristo siyo Eliya wala Nabii yule? Kumbe Nabii yule atakuwa anabatiza watu.
Swali la hawa waliotumwa linatufungua macho na kutuonyesha yafuatayo:
1. Wao walijua atakaenza kubatiza ni Kristo na Nabii yule.
2. Yohana akawajibu amesimama yule wasiyemjua, huyo ambae atakuja nyuma yake ndiye Nabii yule ndiye Kristo.
SASA TUMSOME TENA, YOHANA, NI NANI ALIMAANISHA KUWA NI NABII YULE?
Yohana 1:29 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 30 HUYU NDIE NILIYENENA HABARI ZAKE ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana ALIKUWA KABLA YANGU.
Yohana anawafundisha waliotumwa kuwa, Yesu ndie aliye kuwa amaanisha na ndie YULE ajaye baada yake.
Yohana 7:25 Basi baadhi ya watu wa Yerusalemu wakasema, Je! Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue? 26 Na kumbe! Anena waziwazi, wala hawamwambii neno! Yamkini hao wakuu wanajua hakika ya kuwa huyu ndiye Kristo? 27 Lakini huyu twamjua atokako; bali Kristo atakapokuja hakuna ajuaye atokako.
Hapo juu tunajifunza kuwa, walu hawakujua kuwa Kristo ndie yule yule Nabii YULE, wao walijua kuwa Nabii Yule na Kristo Yesu ni wawili tofauti.
Je, madai yao ni kweli, kuwa Nabii Yule na Yesu ni wawili tofauti?
Swali la Kujiuliza Je! ni kweli Yesu ndiye NABII yule?
BIBLIA INAKUJIBU KUWA YESU NI NABII YULE:
Yohana 6:11 Basi Yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia walioketi; na kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka. 12 Nao waliposhiba, aliwaambia wanafunzi wake, Kusanyeni vipande vilivyobaki, kisipotee cho chote. 13 Basi wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili, vipande vya mikate mitano ya shayiri vilivyowabakia wale waliokula. 14 Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, HAKIKA HUYU NI NABII YULE ajaye ulimwenguni.
Naam, tumesha jibiwa kwa kutumia Biblia hiyohiyo kuwa Yesu ni Nabii yule. Maana sifa zote za Nabii Yule zinaonekana kwa Yesu.
Kumbukumbu la Torati 18:18 Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.
Ukisoma katika kijarida cha NABII ALIYE KUWA AKAMA MUSA http://www.maxshimbaministries.org/…/nabii-aliye-kama-musa-… utagundua kuwa, huyo Nabii ni Yesu.
Yohana 3:14 Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;
15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.
Maandiko yanazidi kutuonyesha kuwa aliye mfano wa Musa ni YESU.
Waebrania 4:1 Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu, 2 aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu.
NABII YULE NI YESU KRISTO:
Yohana 7:37 Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. 38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. 39 Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa. 40 Basi wengine katika mkutano walipoyasikia maneno hayo, walisema, HAKIKA HUYU NDIE NABII YULE.
Baada ya kumsikia katika huo mkutano, walizna kukiri wenye kuwa YESU NI NABII YULE.
Mathayo 21:10 Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu? 11 Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.
Nimemaliza kwa aya kadhaa kusadia ujumbe huu kuwa, YESU NDIE NABII YULE.
Barikiwa sana na tuendelee kujifunza neno la Mungu.
Shalom,
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW