Friday, April 7, 2017

MASWALI NA MAJIBU KITABU CHA MWANZO (SEHEMU YA KWANZA)

Image may contain: cloud, sky and text
Nitaanza kuielezea Biblia kutoka kitabu cha Mwanzo mpaka Ufunuo aya kwa aya. Naomba tushirikiane na Mungu atubariki sana.
Swali (S): Kwenye Mwanzo, tunajuaje kuwa Kitabu cha Mwanzo kinatakiwa kuwa kwenye Biblia?
Jibu (J): Pamoja na sababu nyingine, kwa sababu Yesu na watu wengine wengi kwenye Biblia walithibitisha ukweli wa Agano la Kale na walikielezea Kitabu cha Mwanzo kuwa ni Maandiko (Matakatifu).
S: Kwenye Mwanzi, ni nani aliyejibu maswali ya Kitabu cha Mwanzo?
J: Kwa kadri nijuavyo, mtu wa kwanza kuandika majibu ya maswali yahusuyo kitabu cha Mwanzo ni Philo, Myahudi wa Kiyunani (Kigiriki) wa Alexandria aliyeishi kutoka karibu mwaka 20 KK hadi 50BK. Leo hii tunayo tafsiri ya Kiarmenia ya kazi yake. Aliandika kazi yake yenye sehemu tatu, Questions and Answers on Genesis (Maswali na Majibu kuhusu Mwanzo). Tumetunza majibu yake kwa maswali 244 toka Mwanzo 1 hadi 17, kwa mujibu wa mtazamo wa Myahudi mcha Mungu ambaye aliathiriwa sana na falsafa za Kigiriki za Plato.
S: Kwenye Mwanzo 1, kwa kuwa vitu vingine vinapaswa kuwa kweli, kama 1 = 1, na 1 + 1 = 2, je Mungu aliumba hesabu na namba? Angeweza kuviumba kwa njia nyingine tofauti?
J: Mungu aliumba kilakitu; hata hivo, marudiorudio (tautology), kitu ambacho ni kweli sawa na maana yake ilivyo kama vitu vyekundu vina rangi nyekundu, si kitu. Tunaweza kukisia kuwa Mungu aliumba "kila kitu" kwenye hesabu na hii si marudiorudio.
S: Kwenye Mwanzo 1, kwa kuwa Mungu aliumba kila kitu, je aliumba giza, uovu, na mashimo ardhini? Kama aliumba uovu, haonyeshi kuwa mzuri mkamilifu. Kama sivyo, yeyote aliyeumba anaonyesha kuwa muumbaji pia.
J: Mungu aliiumba vitu vyote. Giza si kitu, bali ni kutokuwepo au upungufu wa mwanga. Uovu si kitu, bali kutokuwepo au kupotoa mambo mema. Mashimo, giza, na maovu hayakuumbwa moja kwa moja na Mungu, lakini yametokea kama marudiorudio, au "matokeo ya maisha" ya mada, mwanga na mambo mema. Hivyohivyo, kivuli si kitu kinachojitegemea, kikiwa na mada, nishati, au roho. Hata hivyo, mimea inaweza kufa kwenye kivuli.
S: Kwenye Mwanzo 1, kwa kuwa Mungu aliumba kila kitu kikiwa kizuri, kwa nini radi, milipuko ya magonjwa na majanga mengine hutokea?
J: Kila kitu kilikuwa kizuri mwanzoni. Lakini Warumi 8:20-22 inaonyesha kuwa tokea wakati wa anguko, dunia "ilitiishwa chini ya ubatili" pia. Ulimwengu wote upo chini ya utawala wa mwovu(1 Yohana 5:19), na mkuu wa dunia hii ni Shetani kwa mujibu wa Yohana 12:31; 14:30.
S: Kuna hoja gani ya umbo na muundo wa ulimwengu kwenye Mwanzo 1?
J: Kwanza, ifuatayo ni njia rahisi na yenye mantiki rahisi yenye kuelezea.
Huwezi kupata kitu bila kuwa na kitu (kingine). Kila kitu kilichoumbwa kilihitajika kuumbwa. Hata vitu vya kwanza kuumbwa vilihitajikwa kuumbwa na kitu/mtu mwingine ambaye aliisha kuwepo. Kwa hiyo, panatakiwa kuwa na kitu au mtu ambaye hajaumbwa na anaishi milele.
Yafuatayo ni maelezo makali; maana ni zangu mwenyewe.
Tunadhani kuwa kila mtu anaufahamu wa kutosha kuweza kuwa na maana inayofaa ya mantiki, kupingana na kutopingana, tukio, mchakato, "ndani ya", kitu, mkusanyiko, muda, mada, nishati, roho, chanzo, kilichosababishwa na, na matokeo.
Uwepo halisi kunafafanuliwa, katika makala hii, kuwa ni kuwepo kwenye ulimwengu huu, kuwa na uwezo wa kuathiriwa na kitu mojawapo hapa ulimwenguni, au kuwa na uwezo wa kuathiri kitu kimojawapo hapa ulimwenguni. Huu ni ufafanuzi mfinyu sana wa kuwepo/kuishi, kwani unashindwa kuhusisha mawazo, mienendo, na mambo mengine. Kwa hiyo, hebu na tuuite uwepo "halisi" na tufanye majadiliano yetu hapa yakomee kwenye uwepo halisi.
Kitu halisi kinafafanuliwa hapa kuwa ni kitu au mkusanyiko au mada, nishati, roho, au mchanganyiko wenye kuwa na uwepo halisi. Ukweli wa kimantiki, ukinzani wa kimantiki, na ushahidi wa kihesabu havichukuliwa kuwa vitu hapa.
Uwepo wa kimelea, kama kitu cha ndani, unafafanuliwa kuwa ni uwepo halisi wa vitu ambavyo si vitu halisi. Mashimo, giza, upungufu, kutokuwa sahihi, na maovu si mada, nishati, au roho, lakini kama ambavyo kivuli kinaweza kuua mimea ambayo inahitaji jua, au upungufu au chakula unavyoweza kuua mtu, vivuli na upungufu wa chakula vina uwepo halisi licha ya kutokuwa vitu halisi.
Ulimwengu unafafanuliwa hapa kuwa ni mkusanyiko wa vitu halisi ambavyo vipo kiuhalisi. Tazama kuwa katika ufafanuzi huu, ulimwengu unajitosheleza, na Mungu (tuchulie kuwa Mungu yupo, ni Roho na anaweza akaathiri vitu) yupo ulimwenguni.
Kutokwepo (nothing) kunafafanuliwa kuwa ni kitu ambacho hakijawahi kabisa kuwepo, au ambacho hakijawahi kuwa na uwepo wa kweli/kihalisi wakati wowote ule. Kwa maneno mengine, kabla hakijaumbwa [au baaday ya kuharibiwa], kitu halisi hakipo ulimwenguni, hakiuathiri ulimwengu, na hakiathiriki na ulimwengu.
Uumbaji unafafanuliwa hapa kuwa ni tukio au mchakato wa kufanya kitu halisi kipya. Kuumba kunatofautishwa na "kubadilisha", ambako hakuhitaji chanzo chochote mbali ya kitu chenyewe. Kuumba kitu halisi kipya kunaweza kuhusisha kubadilisha au kuharibu kitu halisi kilichowahi kuwepo, lakini hakulazimiki kufanya hivyo. Hata hivyo, angalia sehemu inayofuata.
Hakuna kitu kinachoweza kuwepo kutokana na kitu kisichokwepo. Kitu chochote halisi kilichoumbwa kinahitaji chanzo cha kuumbwa kwake. Kwa maneno mengine, hakuna kitu kinachoweza kuumbwa isipokuwa kitu/vitu vinginie vimekiumba.
Hakuna kitu kinachoweza kujiumba chenyewe. Hakuna kitu kinachoweza kujiumba chenyewe. Ingawa vitu halisi vinaweza kujibadilisha wakati mwingine, au kujiharibu vyenyewe, hakuna kitu kinachoweza kuwa chanzo cha kuumbwa kwake.
Chanzo cha kwanza. Ingawa vitu halisi vilivyoumbwa vinaweza kuumba vitu vingine halisi vilivyombwa, mwisho wa siku patahitajika kuwa na chanzo cha kwanza. Kwa maneno mengine, kwenye mlolongo wa vyanzo, chanzo walau kimoja kinatakiwa kuvitangulia vyanzo vingine vyote.
Kisichoumbwa. Kwa vile chanzo walau kimoja hakitakiwa kuwa na chanzo kilichokitangulia, na kila kiumbe kinahitaji chanzo, kuna kitu halisi walau kimoja ambacho hakijaumbwa na kimekuwepo toka milele iliyopita, kwa sababu kuna kitu halisi walau kimoja ambacho hakijaumbwa.
Mhutasari: Kila kitu halisi ambacho kinaishi ama kina wakati au kipindi fulana=i ambacho kiliwahikuishi, vinginevyo hakijawahi kuishi. Kama kimewahi kuishi, basi kuna kitu halisi ambacho ni chanzo cha kuwepo kwake.
Mipaka: Hoja hii haithibitishi kwamba chanzo cha kwanza ni kitu chenye uhai, au kwamba kuna chanzo kimoja tu ambacho hakijaumbwa, au kwamba vyanzo vyovyote ambavyo havijaumbwa bado vinaishi. Kitu ambacho hoja hii inasema ni kwamba kuna walau kitu kimoja halisi (nafsi iliyo hai au kitu kisichokuwa nafsi) ambacho kimekuwepo milele bila kuumbwa.
Moja ya waandishi wa kwanza aliyeiona hoja ya muundo na umbo la ulimwengu na kusema kuwa Mungu ni chanzo cha kwanza alikuwa Philo, Myahudi aliyeishi Alexandria, Misri, toka mwaka 15/20 KK hadi mwaka 50BK. R. C. Sproul na Norm Geisler wameandika kazi nyingi na nzuri kuhusiana na hoja ya muundo na umbo la ulimwengu.
USIKOSE SEHEMU YA PILI:
SWALI: Hoja kuwa "kushindwa kuelezeka kirahisi kwa ulimwengu kunaonyesha kuwa ni lazima kuwe na muumba" inaonekana nzuri, hadi inapochukuliwa kwenye hitimisho lake la kimantiki. Vipi kuhusu ugumu wa Mungu kueleweka? Kama kitu chenye utatanishi kinahitaji muumba basi Mungu lazima ahitaji muumba mkubwa zaidi, na kwa jinsi hiyohiyo na kuendelea. Je hoja hii inaishia wapi? Hoja hii inaishia na "kurudi nyuma kusikokuwa na ukomo," na hakuna jibu kwa hili? Ama je lipo?
Shalom
Max Shimba Ministries

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW