Monday, April 10, 2017

KITABU CHA MWANZO (SEHEMU YA TATU)

Image may contain: cloud, text and nature
S: Kwenye Mwanzo 1:10, ilikuwaje Mungu aumbe dunia wakati dunia ilikuwa tayari imeishaumbwa kwenye Mwanzo 1:1?
J: Neno la Kiebrania (eres) ni hilo hilo linalotumika sehemu zote. Kama ilivyo kwenye kiingereza, eres inaweza kumaanisha ulimwengu chini ya anga, na inaweza kumaanisha ardhi au nchi kavu. Kwa hiyo Mungu aliiumba sayari kwenye Mwanzo 1:1, na nchi kavu kwenye Mwanzo 1:12. Tazama Encyclopedia of Bible Difficulties uk.65-66.
S: Kwenye Mwanzo 1 na 2, kwa nini inaonekana kana kwamba kuna matukio mawili ya uumbaji?
J: Mwanzo 1 ni uumbaji wa mbingu na nchi, na Mwanzo 2 ni uumbaji wa wanadamu kwenye bustani ya Edeni.
S: Kwenye Mwanzo 1 na sehemu nyingine, kwa nini Mungu anaitwa Elohim, wakati sehemu nyingine tena kama Mwanzo 2 Mungu anaitwa Yahweh?
J: Mungu ana idadi kubwa ya majina kwenye Biblia. Inaonekana kuwa jina Yahweh linaangalia zaidi uhusiano binafsi wa Mungu na sisi tofauti na Elohim, ambalo linaangalia zaidi haki na ukuu wake.
Lilikuwa jambo la kawaida katika jamii za zamani kuwa na majina zaidi ya moja kwa mungu huyohuyo. Hii hapa ni mifano:
Osiris - Wennefer, Khent-amentius, Neb-abdu
Bel - Enlil, Nunamnir
Sin - Nanna
El - Latpan
Baal - Larpan
Elohim is the general name for God and is used in the context of God as creator. It emphasizes that God is distant and powerful. It is used to describe God as the awesome and majestic creator. In our English Bibles, Elohim is translated as God.
Yahweh (the LORD) is God's personal name and is used in the context of God having a relationship with His people. When God goes about creating humanity, it is Yahweh who does this act. When the Lord is personally involved with His people, Yahweh is the proper way to designate Him. In our English Bibles Yahweh is translated as the LORD with all capital letters.
S: Kwenye Mwanzo 1, je Mungu aliweza kuumba dunia kwa siku sita halisi zenye masaa 24 kila moja?
J: Bila kujali kama wanadhani dunia iliumbwa miaka mingi iliyopita au michache, Wakristo wote wanapaswa kujibu swali hili "ndiyo."
Badala ya siku sita, Mwenye enzi angeweza kuiumba kwa muda wa sekunde sita kama angependa kufanya hivyo. Suala hapa si jinsi gani Mungu alipaswa kuumba bali ni jinsi gani Maandiko na ulimwengu vinaonyesha alichagua kuumba.
Kama nyongeza, Maandiko hayasemi siku ina urefu gani kwa Mungu kwenye Mwanzo 1. Kumbukumbu 7:1 inaonyesha kuwa "siku" inaweza kuwa ni kipindi cha muda kinachozidi masaa 24, kama ilivyoeleweka kuwa "siku" za Musa. Zaburi 90:4; 2 Peter 3:8 zinaonyesha kuwa siku za Mungu zinaweza kuwa ndefu sana.
S: Kwenye Mwanzo 1, je kufanana kwa maelezo haya ya uumbaji na yale ya Wababeli kunathibitisha kuwa yote haya yametoka kwenye chanzo kimoja kilichotungwa na watu?
J: Maelezo ya Wababeli yanafanana kwenye ufafanuzi wa kinaganaga lakini karibu ni kinyume kabisa kuhusiana na chanzo. Tofauti na Marduk aliyekuwa anashindana na vurugu za joka kubwa Tiamat, Mungu anaamuru nini kitokee. Kama kuna kitu cha kweli kwenye jamii zisizokuwa za kibiblia jambo hili halipaswi kutushangaza. Isitoshe mtindo wa Mwanzo 1 unaelekea kuwa ni utofauti uliokusudiwa dhidi ya nadharia za kipagani.
USIKOSE SEHEMU YA NNE: Kwenye Mwanzo 1:26 na 3:22, kwa nini neno "tumfanye" linatumiwa kwa Mungu Mmoja wa Kweli?
Shalom,

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW