Monday, April 10, 2017

JE, MUNGU ALIMUUMBA SHETANI?

Image may contain: text

Mungu aliwaumba viumbe wote wakiwa Wakamilifu, lakini walikuwa na uhuru wa kuchagua Kumtii Mungu au Kutomtii Mungu. Tunajua ya kwamba wengine kati yao walitenda dhambi, na Biblia inawataja kama “Malaika walioanguka” (Mwanzo 6:2,4; Yuda. 1:6)
LUSIFA ALIKUWA NANI?
Lusifa alikuwa amejaa hekima na alikuwa Mkamilifu katika uzuri wote, lakini aliingia katika majivuno na kuwa asiyefaa kitu na kugeuka kuendelea katika njia ya dhambi, (Ezekieli 28:12-15). Alifikiri angeweza kujiinua juu ya Kiti cha Enzi cha Mungu (Isaya 14:12-14). Maasi yake yalishindwa na kutupwa chini, duniani katika nchi (Luka 10:18; pia katika Ufunuo 12:7,9).
MWANZO WA JINA LA SHETANI:
Lusifa alishawishi theluthi ya malaika kumfuata katika maasi yake. Ambao alifukuzwa nao na jina lake likabadilika na kuitwa shetani, yule joka mkubwa (Ibilisi) na malaika waliofuatana naye wanajulikana kama pepo wachafu (demons). Wote wanajulikana kama “Jeshi lililoanguka”
Biblia inamfafanua Shetani kuwa kiumbe halisi ambaye yuko katika makao ya roho. (Ayubu 1:6) Inatueleza kuhusu sifa zake za ukatili kutia ndani matendo yake ya uovu. (Ayubu 1:13-19; 2:7, 8; 2 Timotheo 2:26) Pia inasimulia mazungumzo kati ya Shetani na Mungu na pia kati yake na Yesu.—Ayubu 1:7-12; Mathayo 4:1-11.
MAANA YA JINA LA SHETANI:
Jina hilo ni la kumfafanua, na linamaanisha “Mpinzani; Adui; Mshtaki.” Alikuja kuitwa Shetani kwa sababu alichagua kumpinga Mungu.
Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata itakapokuja ile hukumu (1 Petro 3:18-20; 2 Petro 2:4-5; Yuda 1:6). Mapepo wengine wachafu, huzunguka zunguka katika dunia hii wakitafuta watu ili wawameze (Ayubu 1:6-12; Lk 8:30-32).
JE, UMEJIULIZA HIVI?
 Shetani alitoka wapi?—Ayubu 38:4-7; Yohana 8:44.
 Shetani huathiri ulimwengu kadiri gani?—Yohana 12:31; 1 Yohana 5:19; Ufunuo 12:9.
 Tunaweza kufanya nini ili kujilinda kutokana na mbinu za uovu za Shetani?—1 Petro 5:8-10.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW