Monday, April 10, 2017

JE! KUANGALIA PICHA ZA NGONO NI DHAMBI? (SEHEMU YA PILI)

Image may contain: 1 person, sitting and text
Kuangalia picha za ngono "NI DHAMBI" kwa herufi kubwa. Katika Sheria ya Musa ilikuwa mtu anahesabika kuwa ametenda dhambi pale ambapo atakutwa akifanya kitendo hicho au kukiwa na mashahidi wawili au watatu atatakiwa kuhukumiwa sawasawa na Sheria husika.
Kwenye dhambi ya uzinzi mtu alitakiwa apigwe mawe hadi afe sivyo kwa Sheria ya Kristo yenyewe inazungumzia juu ya kitendo cha "kutamani" tu unahesabika kuwa umefanyika DHAMBI (Mathayo 6:27-29, Waebrania 10:28). Tamaa mbaya ni dhambi kama dhambi nyinginezo. Kwa kawaida tamaa huja na ile tamaa huchukua mimba na baadaye huzaa dhambi (Yakobo 1:13-16). Kitendo cha kuangalia picha za ngono hupofusha "FIKRA" nzuri za mtu alizonazo. Mawazo machafu uanza kutawala katika ubongo wako hadi "USHUSHE" huo mzigo ulioko kwenye viungo vyako vya uzazi. Ahaaa ni hatari aiseeee.
Wewe unayengalia picha za ngono Kama ndiyo starehe yako unaiharibi nafsi yako "unakuwa zezeta wa akili" Biblia inasema "taa ya Mwili jicho na jicho lako likiwa safi mwili wako wote utakuwa na nuru. Lakini jicho lako likiwa bovu mwili wako wote utakuwa na giza.."(Mathayo 6:22-23). Kwa wale wanandoa ni "MWIKO" kutumia picha za ngono ili kunogesha kufanya Tendo la Ndoa.
Wewe mume unaye hapo "chombo" unakiona "live" na kimethibitishwa na Mungu mwenyewe sasa hiyo mipicha ya nini? Kila kiungo Mungu alikiweka kwa ajili ya kusudi maalum kama ni mdomo kwa ajili ya kuongea na kupitisha chakula na si kunyonya sehemu za Siri za mwenzi wako. Mungu ameweka sehemu ya "haja kubwa" kwa ajili ya kutolea uchafu uliotengenezwa na tumbo na si kiungo kingine kiende kukoroga "zege" hilo huo ni uchafu(Ufunuo 22:10-15).
Warumi 1:26:27
“Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.”
USIKOSE SEHEMU YA TATU "JINSI YA KUSHINDA DHAMBI YA KUANGALIA PICHA ZA NGONO"
Shalom

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW