Monday, April 10, 2017

JE! KUANGALIA PICHA ZA NGONO NI DHAMBI? (SEHEMU YA TATU)

Image may contain: one or more people, people sitting, shoes, indoor and text
JINSI YA KUSHINDA DHAMBI YA KUANGALIA PICHA ZA NGONO
PICHA ZA NGONO zinavutia sana kuziangalia ila zina maangamizo makubwa sana katika maisha yako. Lazima ufikie mahali kukata shauri ndani ya Moyo wako kuambatana na Mungu. Kusudi kubwa la shetani kuachilia mambo yake ya NGONO kwenye mitandao ili apate wafuasi wengi zaidi. Hakuna kitu unachoweza kukifanya katika simu za Android wengine wasikitambue. Kila unalolipitia na kuliangalia kwa Siri siku ya siku litaletwa hukumuni na Mungu mwenyewe (Warumi 2:16, Mhubiri 12:14)
USHAURI WAKIVITENDO:
I) Yatie Nuru macho yako - Zaburi 13:3, 19:8 - Yaruhusu macho yako yaingiziwe nuru na Yesu. Chukua muda wa kutosha kuingiza PICHA zinazomhusu Mungu zaidi. Angalia wahubiri mbalimbali.
II) Tazama mambo ya Adili(mema) - Zaburi 17:2-3 - Kuna nguvu kubwa sana tunapokuwa tunaangalia mambo mema. Vipindi vizuri vya neno la Mungu. PICHA zinazojenga siyo zinazoharibu fikra zetu.
III) Kumuomba Mungu afumbue macho yako - Zaburi 119:18, 146:8- Maombi ni muhimu ili kufanya macho yako kuona kusudi la Mungu na Kutambua uwepo wa shetani katika PICHA ZA NGONO.
IV) Weka maneno ya Mungu Mbele za macho yako - Mithali 4:20-21
Wakati wote soma neno la Mungu kupitia kifaa chochote cha ki-electronic ili uweze kumjua Mungu zaidi.
V) Macho yako yatazame Mbele - Mithali 4:25-27
Kutazama Mbele maana yake uwe na maono. Maono ni PICHA au TASWIRA ya Mbele ya maisha yako. Yeremia aliulizwa unaona nini naye akasema "anaona ufito wa mlozi" anaona kitu kizuri (Yeremia 1:11-12).
VI) Pendezwa na njia za Mungu - Mithali 23:26
Kuanzia sasa anza kupendezwa na njia za Mungu katika maisha yako. Acha kuzifuata njia zako katika kuufurahisha mwili wako wa PICHA zisizofaa.
VII) Tafuta watumishi wa Mungu ili wakufundishe - Isaya 48:17, 30:20-21
Kuna mambo ambayo yanatupa shida katika maisha yetu ni vizuri kuwaona waalimu ili watusaidie jinsi ya kutoka katika mtego huo.
VIII) Omba rehema na neema ya Yesu - Waebrania 4:16
Tunahitaji neema ya Mungu ili kushinda Hali hiyo ya kupenda KUANGALIA PICHA ZA NGONO na pia kufunguliwa kutoka katika vifungo hivyo vya pepo wa tamaa na mahaba.
Mungu atakubariki ukipeleka ujumbe huu kwa wengine.
TUMEFIKIA MWISHO WA SOMO LETU KUHUSU DHAMBI YA PICHA ZA NGONO.
Barikiwa sana.
Shalom,

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW