Wednesday, April 12, 2017

HAKUNA LISILOWEZEKANA KWA YESU MUNGU

Image may contain: 1 person, text
Ndugu, tukimuamini Mungu kwa mioyo yetu yote hakika yote yanawezekana.
Baba mmoja ambaye mwanawe alikuwa akisumbuliwa na pepo la kifafa alimleta mwanawe kwa wanafunzi wa Yesu nao hawakuweza kumpa suluhisho. Ndipo alipomfuata Yesu na kumwambia ukiweza naomba umponye mwanangu. Yesu alishangaa! Akauliza ukiweza? Akamwambia “ Yote yawezekana kwake aaminiye”
“Lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia. Yesu akamwambia, ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.” (Marko.9:22-23)
Hakuna jambo lililo gumu la kumshinda Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo.
Zekaria 8:6, Bwana wa majeshi alimwambia Musa; “ ingawa hili ni neon lililo gumu mbele za macho ya mabaki ya watu hawa, je, liwe neno gumu mbele za macho yangu?. Hata kama jambo ni gumu na linaonekaka kama halitawezekana mbele za macho yetu sisi wanadamu, Mungu wa Ibrahim Isaack na Yakobo, yaani Mungu wa Israel, anaweza yote. hakuna jambo lililo gumu la kumshinda Mungu wetu.
Mwanzo 18:14, Bwana alimwambia Sara mke wa Ibrahimu kuwa, Jambo gani lililo gumu linalomshinda Bwana? Mungu wetu anaweza yote. Mungu wetu ana nguvu, ni mkuu ni unique, na anaweza mambo yote. hafananishwi na chochote, hashindani na chochote wala yoyote, ni mkuu mno, nguvu zake hazichunguziki, mawazo yake hayachunguziki, na njia zake hazichunguziki.
Hesabu 11:23, Bwana Mungu wetu alimwambia Musa, Je, mkono wa Bwana umepungua urefu wake? Sasa utaona kwamba neno langu litatimizwa kwako au la. (soma mpaka isaya 59:1, kuwa mkono wa bwana si mfupi hata usiweze kuokoa….sikio lake si zito lisiweze kusikia, ila maovu yetu ndo kikwazo…., pamoja na yote hayo, hapa, Mungu alitaka kumwonyesha Musa kuwa hakuna jambo lililo gumu kwake.
Ayubu 42:2, Neno la Bwana kwa kinywa cha Ayubu linasema”najua ya kwamba waweza kufanya mambo yote, na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuiliwa. Hakuna mtu wala kitu chochote kinachoweza kumzuia Mungu kufanya atakacho. Mungu akisema ndiyo hakuna mtu wa kusema hapana, na akisema hapana hakuna wa kusema ndiyo.
Luka 1:37, Malaika alimwambia mariam kuwa, hakuna Neno lisilowezekana kwa Mungu. Kwa Mungu wa ibrahim isaka na Yakobo, Mungu wa kweli aliyeumba mbingu na nchi na vyote vijazavyo, anaweza yote.
Yeremia 32:17, Neno la Bwan alinasema “Aa! Bwana Mungu tazama wewe umeziumba mbingu na nchi kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa, hapana neno gumu usiloliweza.
Efeso 3 :20, Neno la Mungu linasema, Basi, atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu. Mungu anao uwezo wa kufanya mambo makubwa na ya ajabu kuliko yale tuliyowahi kuyaona,kuyaomba au kuyawaza. Mungu aweza kufanya mambo makubwa sana na ya ajabu.
Mathayo 19 :26, Yesu akawakazi macho akawaambia kwa wanadamu hilo haliwezekani, bali kwa Mungu yote yanawezekana. Yesu mwenyewe ndiye alitoa ahadi na ufafanuzi huu hapa kuwa, kwa Mungu yote yanawezekana.
Hivyo, hakuna sababu ya kuwa na hofu tumwombapo Mungu, tunajua kuwa Mungu ano uwezo wa kufanya mambo yote hata yale ambayo sisi tunayaona kama magumu sana.

Marko 10 :27, Yesu akawakazi macho akasema, « kwa wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo, maana yote yanawezekana kwa Mungu ». hakuna jambo liwalo lote lile ambalo Mungu linamshinda.

Shalom

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo. 

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW