Sunday, March 19, 2017

UTATU NI MUNGU

Image may contain: text


Katika Utatu tunafunuliwa kuwa Yesu ni Mungu kama alivyo Baba yake na Roho Mtakatifu.
Ungana nami na tusome Biblia takatifu kwa pamoja.
1. Baba ni Mungu:
Filipo 1:2 “ Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo”.
2. Mwana ni Mungu:
Yohana 1:1:14 Kolosai 2:9
• Hapo mwanzo kulikuwako Neno , naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu ------------, Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba amejaa neema na kweli”.
• Kolosai 2: 9 “ Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu kwa jinsi ya kimwili”.
3. Roho Mtakatifu ni Mungu
Matendo 5:3-4 “ Petro akasema Anania kwa nini shetani amekujaza moyo wako kumwambia uwongo Roho Mtakatifu na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Kilipokuwa kwako hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwishauzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako?.Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu bali Mungu”.
Roho Mtakatifu ni, nafsi ya tatu ya Mungu yenye hisia “emotion”, huhuzunika (Efeso 4:30), hunena, (Ufunuo 2:7), anaweza kuzimishwa ((1Thesalonike 5:19), Hufurahi (Rumi 14:17) .Hivyo Roho Mtakatifu ni Mungu Mwenyewe na wala siyo kitu tu (impersonal) (Yohana 4:24) .
Pia katika kitabu cha Isaya 63:7-10 “ Nitautaja wema wa BWANA, Sifa za BWANA kwa yote aliyotukirimia BWANA; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israel, aliyowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake. Maana alisema, hakika ndiyo watu wangu hawa, wana wasio na hila; akawa Mwokozi (Yehoshua) wao. Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale. Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia , akawa adui , akapigana nao”
Nategemea sasa umesha elewa kuwa, SOMO LA UTATU ni muhimu sana, maana linatufungua macho na kufahamu Uungu wa Yesu, Uungu wa Roho Mtakatifu na Uungu wa Yehova.
Shalom,
Max Shimna Mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW