MALAIKA MKUU GABRIEL
Neno "Malaika Mkuu" linatokana na neno la Kiyunani Archangelos, lenye maana ya Mkuu wa Malaika (chief angel), kwa tafsiri ya Krania rav-mal'ákh, linatokana na neno la Kiyunani archein, linalomaanisha kuwa wa kwanza katika cheo au nguvu (to be first in rank or power); na neno angelos linalokaanisha mjumbe (messenger), au muwakilishi wa balozi (envoy).
Neno hili limetumika mara mbili tu katika Agano Jipya katika 1 Wathesalonike 4:16 na katika Yuda 1:9. Ni malaika Wakuu Gabrieli na Mikaeli tu ambao wametajwa kwa majina katika Agano Jipya.
Katika desturi nyingi za kikristo, Malaika Gabrieli anatambuliwa kuwa ni Malaika mkuu, lakini hakuna maandiko ya moja kwa moja yanayoonyesha jambo hili. Ni vema kutambua ya kwamba, neno "Malaika mkuu" linaonekana kutumika tu kwa umoja, na si katika wingi, na pia hutumika tu kumtaja malaika Mikaeli kuwa ndiye Malaika Mkuu.
Malaika waliumbwa katika Roho na ni Roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi Wokovu (Ebrania 1:14). Mungu aliwaumba Wana wake wa Kiroho kabla ya Uumbaji wa nchi (Ayubu 38:4-7). Kuna zaidi ya malaika milioni 100 (Angalia Daniel 7:9-10; Mathayo 26:53; Lk 2:13; Ebrania 12:22; Ufunua 5:11). Malaika wameumbwa katika hali ya mmoja mmoja (individuals) ambao wana uhuru wa kuchagua, ambao ndiyo unahitajika katika kukua kwa tabia.
MAANA YA NENO GABRIEL
Neno au jina “Gabriel” asili yake ni lugha ya kiebrania na maana ni “Mjumbe wa Mungu” katika Biblia jina hili Gabriel limetajwa mara “nne” (4) (Tazama Danieli 8:16 na 9:21, Luka 1:19 na 1:26) kuhusu malaika Gabriel mara nyingi Biblia inaonyesha kuwa Mungu anamtuma ili alete habari njema zinazohusu wokovu wa wanadamu na hutoa maneno ya kuwafariji wale aliowatokea akisema “usiogope”katika Biblia limetajwa mara (366) aidha tunaposoma Biblia tunaona pia malaika huyu anaitwa malaika wa Bwana (The angel of the Lord) Neno hili katika biblia limetajwa mara (65) katika aya zipatazo (61) iwapo sehemu hizo zote zinahusika na malaika Gabriel basi malaika huyo atakuwa ametajwa mara nyingi.
MALAIKA GABRIEL ALIYETUMWA NA MUNGU YEHOVA ANASEMA HIVI…
Malaika akajibu akamwambia Mimi ni Gabriel, nisimamaye mbele za Mungu, nimetumwa niseme nawe na kukupasha habari hizi njema (Tazama Luka 1:19)
Kwa mujibu wa aya hii malaika Gabriel anaeleza kuwa husimama mbele za Mungu hivyo ni wazi kuwa cheo chake ni mjumbe asimamaye mbele ya Mungu.
MALAIKA GABRIEL WA MUNGU YEHOVA ALIFUNDISHA HIVI..
Luka 1:26-35 Nanukuu aya ya 35 tu:
Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako na nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli. Kwa sababu hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu “Mwana wa Mungu”
Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako na nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli. Kwa sababu hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu “Mwana wa Mungu”
MAFUNDISHO YAO KUHUSU ROHO MTAKATIFU KUPITIA MALAIKA GABRIEL
Luka 1:34-35 “Malaika Gabriel anamwambia Mariam hivi…
34. Mariam akamwambia malaika litakuaje neno hili maana sijui mume? 35. Malaika akajibu akamwambia Roho Mtakatifu atakujilia juu yako na nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli- Roho Mtakatifu ni Mungu (Matendo 5:3-4) Na wala siyo malaika ndio maana malaika alisema atakujilia.

MALAIKA GABRIEL ANAPOWATOKEA WATU ANAFANYA HIVI…
Luka 1:19 Alijitambulisha Kwa kusema, “Mimi ni Gabriel.”
Daniel 8:15-16 Au muhusika ambaye alimtokea hujulishwa kwanza
Daniel 8:17-21, Luka 1:13, 30…
Daniel 8:15-16 Au muhusika ambaye alimtokea hujulishwa kwanza
Daniel 8:17-21, Luka 1:13, 30…
Gabriel anamsadia mtu pale anapopatwa na hofu na anasema usiogope. Tabia za malaika Gabriel ni huruma na kumfahamisha mtu kwa upole.
Katika tukio la lingine ni wakati Danieli alipokuwa akiomba na Gabrieli akarushwa upesi akanigusa….. akaongea nami, aliendelea kutabiri wakati wa kuja kwa mara ya kwanza kwa Masihi Yesu Kristo (Daniel 9: 21-27).
Kwa hiyo Wayahudi walikuwa wakitazamia sana wakati wa kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulipokaribia ; kuonekana dhahiri kwa Grabriel tena kulizidishia matazamio kwanza kwa Zakaria kuhani aliyekuwa zamu hekaluni na kisha kwa Mariamu aliyekuwa ameposwa na Yusufu. Kwa Zakaria , malaika akamwambia "mimi ni Gabrieli nisimamaye mbele za Mungu, nami nimetumwa niseme nawe" (Luka 1:19).
Tunaona kuwa Malaika anao uwezo wa kusimama mbele ya uso wa BWANA, jambo ambalo wanadamu hawawezi, hivyo Malaika hutumwa kufanya yote yaliyo mapenzi ya Mungu. Hapa ujumbe wake ilikuwa kutangaza muujiza wa kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji.
Miezi sita baadaye, Gabrieli alimtokea Mariamu; ambaye alikuwa ni wa ukoo wa Mfalme Daudi.Maombi yake Mariamu; malaika alisema, uliyepewa neema na Mungu,nawe utakuwa mama wa Masihi anayetarajiwa. Gabriel alimwambia kuwa atapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na mtoto wake ataitwa Yesu, Mwokozi, naye atakuwa Mwana wa Mungu na atakalia kiti cha enzi cha Daudi (Luka 1: 26-33).
Malaika Mkuu Gabriel:
• Alitafsiri maono ya Danieli (Dan. 8:16, 26; 9:20-27)
• Alitangaza juu ya kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji (Lk. 1:11-20)
• Alitangaza kuzaliwa kwa Yesu (Lk. 1:26-38).
• Alitangaza juu ya kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji (Lk. 1:11-20)
• Alitangaza kuzaliwa kwa Yesu (Lk. 1:26-38).
Katika kitabu cha Henoko kinataja majina ya Malaika wakuu sita:
Mikaeli (Mkuu wa sehemu mhimu sana ya wanadamu) Gabriel (Mkuu wa Bustani na wa Makerubi), Urieli Malaika Mkuu wa dunia na watu wakali) na Raphaeli (Malaika Mkuu wa Roho za wanadamu), Ragueli (ambaye analipiza kisasi juu ya dunia na mwangaza) na Saragaeli (Malaika Mkuu wa watoto wa wanadamu, ambao Roho zao wametenda dhambi).

Kitabu cha Henoko, sura ya 20, R.H Charles, 2002).
Malaika hawa pia wanaitwa Malaika Walinzi.
Malaika katika Agano Jipya:
Tunaona ya kwamba Malaika walimhudumia Yesu wakati alipokuwa katika nchi (duniani) (Mathayo 4:11, Luka 22:43). Malaika alimtokea Yusufu na kumwarifu habari za kuzaliwa kwake Yesu (Mathayo. 1:20, Luka 1:26-38). Malaika walikuwepo katika ufufuo wa Yesu (Mathayo 28:2-8; Yahana 20:12). Na walizungumzia wakati wa kupaa kwakeYesu Kristo (Matendo 1:9-11). Malaika wanatoa huduma za Kiroho kwa watu wa Mungu (Ebrania 1:14; Mathayo. 18:10; Matendo 5:19; 8:26; 10:3; 12:7; 27:23). Malaika hufurahi mwenye dhambi anapotubu (Luka 15:10).

Katika Agano Jipya, Kristo kama mwanadamu bado alitenda kama mtu aliye mdhihirisha na kumfunua Mungu. Na alitenda kwa ukamilifu akifuata asili ya Mungu na tabia ya Mungu. Kama Mpatanishi kati ya Mungu na Wanadamu, kumwona Yesu ni sawa na kumwona Mungu, na kusikia na kumtii Yesu ni kumsikia na kutii Mungu (Eloah). Maneno aliyozungumza hayakuwa maneno yake mwenyewe bali maneno ya Mungu yaliyotoka kwa Mungu. (Yahana 14:8-10)
Usikose SEHEMU YA NNE INAYO HUSU Archangel Selaphiel.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment