Wednesday, March 29, 2017

UNAWAFAHAMU MALAIKA WAKUU SABA WA MUNGU "ARCHANGELS OF GOD? (SEHEMU YA NNE)



SELAPHIEL:

Maana ya Selaphiel ni "Maombi ya Mungu" au "mtu anaye omba kwa Mungu".


Hili jina linaweza pia kuandikwa kama Zerachiel, Selapheal, Salathiel, Selathiel, Sealteal, Seraphiel, Sarakiel, Sariel, Suriel, Suriyel, na Saraqael.


Malaika Mkuu "Archangel Selaphiel" anajulikana kama Malaika wa Maombi. Ni Malaika anaye wasaidia na au wahamasisha watu waombe kwa Mungu. Yaani yeye anakusaidia wewe kupunguza mawazo yako wakati unaomba ili uweze kuomba huku ukiwa unamwazia Muumba wako. [He helps people connect to God through prayer, giving them the focus they need to block out distractions and concentrate on praying].

Malaika Mkuu Selaphiel ametajwa katika Kitabu cha Ufunuo 8 aya ya 3 na 4: Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi. 4 Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika. Vile vile ametajwa kimajina katika kitabu cha Orthodox (3 Ezdras 5:16) na kwenye kitabu aya ya [31:6 cha the apocryphal Jewish and Christian text The Conflict of Adam and Eve].

Wakati wowote unapo jisikia kuomba kuhusu kitu Fulani, basi elewa kuwa Mungu anaweza kuwa ametuma ujumbe kwako kwa kupitia Malaika Mkuu Selaphiel, ambaye anapenda kuhamasisha watu ili waombe.

Zaburi 11 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote. 12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 13 Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.

Somo hili la Malaika ingawa halifundishwi sana Kanisani, ni la muhimu sana maana hawa Malaika wanahusika sana na maisha yetu ya kila siku. Hebu angalia nini hutokea wakati mmoja wetu anapo okoka. Luka 15: 10 Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.


Najua wengi wenu mtasema wapi Yesu alitumia Malaika.

Mathayo 26: 52 Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga. 53 Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?

Umeona hapo. Hata Yesu anasema kuwa angeweza kumwambia Baba yake amtumie zaidi ya Majeshi kumi na wawili ya Malaika. Sasa, kama Yesu anaweza tumia Malaika katika vita hii, je wewe ulisha mwambia Baba aliye Mbinguni akutumie majeshi ya mailaka katika vita vyako? Kumbe ndio maana unakuta Mkristo anaomba kila siku lakini hapati jibu. Ni vyema kama Mkristo sasa uanze kujua jinsi Ufalme wa Mbinguni unavyo fanya kazi na tuachane na “church doctrines” mafundisho ya kikanisa ambayo yameshindwa kukusaidia tokea ulipo okoka.

Hata Shetani alimkumbusha Yesu kuwa angeweza kuomba Malaika waje kumwokoa, ingawa ilkuwa ni mtego.

Soma Mathayo 4: 5 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, 6 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

Wana wa Kiroho wa Mungu pia wanatofautiana katika ngazi na katika uwezo wa utendaji, (Ezekiel 1:9,11; Daniel 10:13; 12:1; Efeso 1:21; Kolosai 1:16; 1 Thesalonike 4:16; Yuda 1:9). Malaika wamepewa uwezo na nguvu ya utendaji (2 Thesalonike1:7); “wanaitwa wenye nguvu na uwezo mwingi” (Zaburi 103:20). Ni “Watakatifu” (Luka 9:26), ni “Wateule” (1 Timotheo 5:21). Hawasitahili kuabudiwa au kusujudiwa (Kol 2:18; Ufunuo 19:10).
Malaika wengine wana mabawa na wengine wanafanana kama sanamu wakiwa na sura za nyuso mbili, ambapo uso mwingine unaweza kuwa ni uso unaofanana na nyuso za wanyama na uso mwingine unaofanana na wanadamu. (Ezekiel 1:4-14; Isaya 6:1-3) wanaweza kubadilika katika maumbile yao na kufanana na maumbile ya kibinadamu wanapoonekana kwa wanadamu (Ebrania 13:2). Wakati wote wana miili ya kung’aa na wanavaa mavazi meupe (Matendo 1:9-11; 22:6-9; 2 Samuel 22:13).
Wanadamu hawaruhusiwi kumwona Mungu, kwa hiyo Malaika wanawasaidia wanadamu katika kumjua Mungu Mmoja wa kweli, (Eloah).

Je, unawafahamu Maseraphi na Makerubi na kazi zao? Usikose sehemu ya Tano kuhusu Malaika Mkuu Michaeli na kazi zake.

Shalom,



Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW