I. Ubatizo ni nini?
Ni ishara ya nje inayoonyesha kuwa mtu ameacha njia zake za zamani na ameanza kumfuata Yesu Kristo.
-Ni ishara ya kufa kuzikwa na kufufuka na Kristo.
Warumi 6:4
Wakolosai 2:12
-Ni ishara ya kufa kuzikwa na kufufuka na Kristo.
Warumi 6:4
Wakolosai 2:12
Maana ya neno “BATIZA”. Neno batiza limetokana na neno la Kiyunani,”BAPTIDZO” lenye maana zamisha au zika kabisa. Hivyo neno batiza maana yake ni zamisha, au zika kabisa.
II. Nani abatizwe?
A. Ni yule aliyeokoka
Matendo 2:38; 8:37; Marko 16:16; Mathayo 28:19
B. Ni mtu mzima
Mathayo 3:13
Matendo 8:36
A. Ni yule aliyeokoka
Matendo 2:38; 8:37; Marko 16:16; Mathayo 28:19
B. Ni mtu mzima
Mathayo 3:13
Matendo 8:36
III. Tubatizwe ubatizo gani?
Ubatizo wa maji mengi.
Mathayo 3:16
Matendo 8:38
Yohana 3:23
Ubatizo wa maji mengi.
Mathayo 3:16
Matendo 8:38
Yohana 3:23
IV. Tubatizweje?
A. Kwa kuzamishwa kwenye maji tele.
Matendo 8:38
Marko 1:10
Yohana 3:23
B. Kuingia majini wawili-Mbatizaji na mbatizwaji.
Matendo 8:38
A. Kwa kuzamishwa kwenye maji tele.
Matendo 8:38
Marko 1:10
Yohana 3:23
B. Kuingia majini wawili-Mbatizaji na mbatizwaji.
Matendo 8:38
V. Je kama kabla ya kuokoka nilishabatizwa, nikiokoka nibatizwe tena?
Kumbuka Ubatizo wa kweli alioagiza Yesu ni mmoja tu wa maji mengi, tena kwa mtu aliyeokoka na awe mtu mzima kama tulivyoona hapo juu. Hivyo hata kama umeambiwa ulibatizwa huko nyuma, ni lazima baada ya kuokoka ubatizwe sasa ubatizo halali Kibiblia maana ule wa mwanzo ulikuwa batili.
Matendo 19:1-7
Matendo 19:1-7
VI. Kwa nini tubatizwe?
A. Ni agizo kutoka kwa Yesu mwenyewe.
Mathayo 28:19
B. Ili kutimiza haki yote.
Mathayo 3:15
C. Ili kuzika mwili wa kale uliokufa.
Warumi 6:4
Wakolosai 2:12
D. Ili kuutangazi ulimwengu kuwa tumeacha mambo ya kale na tumeanza kumfuata Yesu.
A. Ni agizo kutoka kwa Yesu mwenyewe.
Mathayo 28:19
B. Ili kutimiza haki yote.
Mathayo 3:15
C. Ili kuzika mwili wa kale uliokufa.
Warumi 6:4
Wakolosai 2:12
D. Ili kuutangazi ulimwengu kuwa tumeacha mambo ya kale na tumeanza kumfuata Yesu.
2 Wakorintho 5:17
VII. Tubatizwe kwa Jina la nani?
Kwa Jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu
Mathayo 28:19
Kwa Jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu
Mathayo 28:19
VIII. Hitaji la ubatizo.
Maji tele, Mbatizaji na Mbatizwaji.
Yohana 3:23; Mdo 8:38-39; Marko 1:10
IX. Yesu anataka tubatizwe ubatizo aliobatizwa yeye.
- Marko 10:38,39
Maji tele, Mbatizaji na Mbatizwaji.
Yohana 3:23; Mdo 8:38-39; Marko 1:10
IX. Yesu anataka tubatizwe ubatizo aliobatizwa yeye.
- Marko 10:38,39
Tukitaka tuwe marafiki waYesu ni lazima tushike amri zake zote (maagizo yake yote) Yohana 14:14,15
-Raha ya wokovu ni pale tunapotenda yote aliyoagiza Yesu.
-Raha ya wokovu ni pale tunapotenda yote aliyoagiza Yesu.
Ubatizo unaeleza kitambulisho cha waumini kwa kifo cha Kristo, kuzikwa, na kufufuka kwake.
Warumi 6:3-4 inasema, "Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Krisot alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima." Hatua ya kuzamishwa katika maji inadhihirisha kufa na kuzikwa pamoja na Kristo. Hatua ya kutoka nje ya maji yaashiria picha ya ufufuo wa Kristo.
Katika 1 Petro 3:21, Petro alifundisha wazi kwamba ubatizo haukuwa tendo la sherehe ya utakaso wa kimwili, bali ni ahadi kwa dhamiri njema mbele ya Mungu. Ubatizo ni ishara ya kile tayari kimetokea katika moyo na maisha ya mtu ambaye amemwamini Kristo kama mwokozi (Warumi 6:3-5, Wagalatia 3:27, Wakolosai 2:12). Ubatizo ni hatua muhimu ya utii ambayo kila Mkristo anatakiwa kuchukua.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
No comments:
Post a Comment