Tuesday, March 14, 2017

NANI ALIKUWA MUISLAM WA KWANZA?

Image may contain: one or more people and text
UTATA MKUBWA KATIKA KORAN
NANI ALIKUWA MUISLAM WA KWANZA?
Ndugu zanguni:
Leo ningependa tuangalie kiundani kidogo kuhusu, “nani alikuwa Muislam wa Kwanza” kutokana na Koran iliyo teremshwa na Allah.
Kwa mujibu wa vifungu kadhaa katika Quran, Muhammad ni Muislamu kwanza :
Quran 6: 14. Sema: Je, nimchukue rafiki mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mbingu na ardhi, naye ndiye anaye lisha wala halishwi? Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina. 161. Sema: Kwa hakika mimi Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka, Dini iliyo sawa kabisa, ambayo ndiyo mila ya Ibrahim aliye kuwa mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina. 162. Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote. 163. Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu. (Wa ' Ana ' Awwalu Al- Muslimin ). S. 6:161-163
Sema (Ewe Muhammad): Hakika Mimi nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu, kwa kumsafishia Dini Yeye ( tu ). Na nimeamrishwa niwe wa kwanza wa wale ambao ni Waislamu ( kujisalimisha kwake ). S. 39:11-12 Pickthall
Sura hizo hapo juu na aya hizo ulizo zisoma zinapingana vibaya sana na sura zingine katika Koran hiyo hiyo ambazo ziliteremshwa na Allah huyo huyo na kusema Manabii walio tangulia kabla ya Muhammad ndio walikuwa Waislam wa Kwanza.
 Kuran inadai kwamba Adam, Ibrahim, Nuhu, mababu, makabila kumi na mawili ya Israeli, Musa, Yesu nk, hao wote walikuwa waumini wa Allah na walikuwa Waislam, kumbuka hao wote waliishi kabla ya Muhammad ambaye anadai kuwa yeye ni Muislam wa Kwanza:

S. 02:30 , 34-35 , 37
30. Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo yajua. 34. Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote isipo kuwa Iblis, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri. 35. Na tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani, na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu tu; mkawa katika wale walio dhulumu. 37. Kisha Adam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi, na Mola wake Mlezi alimkubalia toba yake; hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba na Mwenye kurehemu. S. 02:30 , 34-35 , 37
163. Hakika Sisi tumekuletea wahyi wewe kama tulivyo wapelekea wahyi Nuhu na Manabii walio kuwa baada yake. Na tulimpelekea wahyi Ibrahim na Ismail na Is-haka na Yaakub na wajukuu zake, na Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, na Daud tukampa Zaburi. S. 4:163
84. Na tukamtunukia (Ibrahim) Is-haq na Yaakub. Kila mmoja wao tulimwongoa. Na Nuhu tulimwongoa kabla. Na katika kizazi chake tulimwongoa Daud na Suleiman na Ayyub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wafanyao wema: S. 6:84
127. Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi. 128. Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma ulio silimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. 129. Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na awafundishe Kitabu na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima. 130. Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipo kuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema 131. Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu wote. 132. Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu. 133. Je! Mlikuwapo yalipo mfikia Yaaqub mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is- hak, Mungu Mmoja tu, na sisi tunasilimu kwake. S. 2:127-133 Shakir
52. Isa alipo hisi kuwa kati yao pana ukafiri alisema: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wanafunzi wake wakasema: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu. Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na shuhudia kwamba sisi hakika ni Waislamu. S. 03:52
67. Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina. S. 3:67 Shakir
113. Wote hao si sawa sawa. Miongoni mwa Watu wa Kitabu wamo watu walio simama baraabara, wanasoma Aya za Mwenyezi Mungu nyakati za usiku, na pia wanasujudu. 114. Wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wanaamrisha mema na wanakataza maovu na wanakimbilia katika mambo ya kheri. Na hao ndio miongoni mwa watenda mema. 115. Na kheri yoyote wanayo ifanya hawatanyimwa malipwa yake. Na Mwenyezi Mungu anawajua wachamngu. S. 3:113-115 Shakir
110. Na pale Mwenyezi Mungu atapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Kumbuka neema yangu juu yako, na juu ya mama yako, nilipo kutia nguvu kwa Roho Takatifu, ukazungumza na watu katika utoto na utuuzimani. Na nilivyo kufunza kuandika na hikima na Taurati na Injili. Na ulipo tengeneza udongo sura ya ndege, kwa idhini yangu, kisha ukapuliza ikawa ndege kwa idhini yangu; na ulipo waponesha vipofu na wakoma kwa idhini yangu; na ulipo wafufua wafu kwa idhini yangu; na nilipo kukinga na Wana wa Israili ulipo wajia na hoja zilizo wazi, na wakasema walio kufuru miongoni mwao: Haya si lolote ila ni uchawi mtupu! 111. Na nilipo wafunulia Wanafunzi kwamba waniamini Mimi na Mtume wangu, wakasema: Tumeamini na shuhudia kuwa sisi ni Waislamu. S. 5:110-111
31. Msinifanyie jeuri, na fikeni kwangu nanyi mmekwisha kuwa wenye kusalimu amri. 32. Akasema: Enyi wahishimiwa! Nipeni shauri katika jambo langu hili, kwani mimi sikati shauri yoyote mpaka mhudhurie 42. Basi (Malkia) alipo fika akaambiwa: Je! Kiti chako cha enzi ni kama hiki? Akasema: Kama kwamba ndicho hichi. (Sulaiman na watu wake wakasema): Na sisi tumepewa ilimu kabla yake (Malkia), na tukawa Waislamu. 44. Akaambiwa: Liingie behewa la hili jumba. Alipo liona alidhani ni maji, na akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake. (Sulaiman) akasema: Hakika hilo ni behewa lilio sakafiwa kwa viyoo! Akasema (Malkia): Mola wangu Mlezi! Mimi nimejidhulumu nafsi yangu, na sasa nanyenyekea pamoja na Sulaiman kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. S. 27:30-31 , 42, 44 Pickthall
Koran inadai kuwa, makundi mbalimbali yaliyo kuwepo kabla ya kuzaliwa Muhammad yaliitwa na kudaiwa kuwa yalikuwa ya Kiislam, Mfano: Tumesoma kuwa Ibrahim ambaye aliishi miaka mingi sana kabla ya Kuzaliwa Muhammad alidaiwa kuwa na yeye alikuwa Muislam, zaidi ya hapo, Koran inadai kuwa, hata wanafunzi wa Yesu nao walikuwa Waislam, ( 3:52 , 67, 5:111 ). Hakika inafahamika kuwa, wote Ibrahimu na wafuasi wa Yesu waliishi muda mrefu kabla ya Muhammad kuzaliwa.
Kwa kweli, Kuran inadai kwamba waamini wote walikuwa kimsingi Waislamu, ingawa hatusomi katika vitabi vingine vya dini kama Biblia ambayo ilikuwepo kabla ya Koran kuwa, Manabii wa Biblia walidai na kukiri kuwa eti wao nao ni Waislamu:
78. Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama inavyo stahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim.
Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qur'ani) pia, ili awe Mtume shahidi juu yenu, na nyinyi muwe mashahidi kwa watu. Basi shikeni Sala na toeni Zaka na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Mlinzi bora kabisa, na Msaidizi bora kabisa S. 22:78
Je, nani alikuwa Muislamu wa Kwanza?
1. Katika Suran 6: 163 Koran inadai kuwa Muhammad ndie Muislam wa kwanza.
2. Katika S. 02:30 , 34-35 , 37 Koran inadai kwamba, ni Ibrahim na waumini walio zaliwa kabla ya Muhammad ndio walikuwa Waislam wa Kwanza.
3. Katika S. 5:110-111 Koran inadai kuwa eti Isa Bin Maryam ndie alikuwa Muislam wa kwanza.
4. Katika S. 2:37 Koran inadai kuwa eti Adam ndie aliye kuwa Muislam wa Kwanza.
SWALI NI HILI:
Nani alikuwa Muislam wa kwanza?
Kwanini Koran ifanye makosa makubwa namna hii na kudai eti Muhammad ndie alikuwa Muislam wa Kwanza?
Waislam wanaweza kudai kuwa kila umma ulitumiwa nabii.
Kama hayo madai ni kweli, basi maswali haya yanahitaji majibu:
1. Nani ni Nabii wa Waafrika?
2. Nani ni Nabii wa Wazungu?
3. Nani ni Nabii wa Wamarekani?
4. Nani ni Nabii wa Wachina?
HAKIKA KUNA UTATA MKUBWA SANA KATIKA KORAN YA ALLAH ILIYO SHINDWA KUTUELEZA NI NANI ALIKUWA MUISLAM WA KWANZA.
Ndugu yangu,
Karibu kwa Yesu Kristo aliye kuja kwa Mataifa Yote.
Matayo 28: 18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Yesu Kristo alikuwa kwa Mataifa yote kama Injili kutokana na Matayo inavyo sema hapo juu. Hakika Msamaha wa dhambi unapatikana kupitia Yesu pekee. Soma: Luka 7 48 Kisha Yesu alimwambia mwanamke, Umesamehewa dhambi zako.
KARIBU SANA KWA YESU KRISTO ALIYE HAI.
Mungu awabairiki sana
Katika Huduma Yake
Max Shimba
Copyright © Max Shimba Ministries 2014

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW